Nawe ukingoja siku tatu, shuka upesi ufike kuko huko ulikojificha, siku ya shughuli ile; nawe kaa karibu na kile kichuguu kule.
1 Samueli 20:20 - Swahili Revised Union Version Nami nitapiga mishale mitatu kandokando yake, kana kwamba ninapiga shabaha. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mimi nitapiga mishale mitatu kandokando kana kwamba ninalenga shabaha fulani. Biblia Habari Njema - BHND Mimi nitapiga mishale mitatu kandokando kana kwamba ninalenga shabaha fulani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mimi nitapiga mishale mitatu kandokando kana kwamba ninalenga shabaha fulani. Neno: Bibilia Takatifu Nitapiga mishale mitatu kando yake, kana kwamba nilienda kulenga shabaha. Neno: Maandiko Matakatifu Nitapiga mishale mitatu kando yake, kama kwamba nilikwenda kulenga shabaha. BIBLIA KISWAHILI Nami nitapiga mishale mitatu kandokando yake, kana kwamba ninapiga shabaha. |
Nawe ukingoja siku tatu, shuka upesi ufike kuko huko ulikojificha, siku ya shughuli ile; nawe kaa karibu na kile kichuguu kule.
Kisha, angalia, nitamtuma mtoto na kumwambia, Nenda ukaitafute mishale. Hapo nikimwambia yule mtoto, Tazama, mishale iko upande wako huu, itwae; basi uje, maana iko amani kwako, wala hapana hatari, BWANA aishivyo.
Akamwambia mtoto wake, Piga mbio, ukaitafute mishale niipigayo. Na yule mtoto alipokuwa akipiga mbio, akapiga mshale, ukapita juu yake.