Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

1 Samueli 18:13 - Swahili Revised Union Version

Kwa ajili ya hayo Sauli akamwondosha kwake, akamfanya awe kamanda wake juu ya askari elfu moja; naye akatoka na kuingia mbele ya watu.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Hivyo, Shauli akamwondoa na kumfanya kiongozi wa wanajeshi 1,000. Naye Daudi akawaongoza vyema vitani.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Hivyo, Shauli akamwondoa na kumfanya kiongozi wa wanajeshi 1,000. Naye Daudi akawaongoza vyema vitani.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Hivyo, Shauli akamwondoa na kumfanya kiongozi wa wanajeshi 1,000. Naye Daudi akawaongoza vyema vitani.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Kwa hiyo Sauli akamwondoa Daudi mbele yake na kumpa kuwa kiongozi wa watu elfu moja, naye Daudi akatoka na kuingia akiongoza vikosi katika vita.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Kwa hiyo Sauli akamwondoa Daudi mbele yake na kumpa kuwa kiongozi wa watu elfu moja, naye Daudi akatoka na kuingia akiongoza vikosi katika vita.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Kwa ajili ya hayo Sauli akamwondosha kwake, akamfanya awe kamanda wake juu ya askari elfu moja; naye akatoka na kuingia mbele ya watu.

Tazama sura
Tafsiri zingine

1 Samueli 18:13
7 Marejeleo ya Msalaba  

Zamani za kale, hapo Sauli alipokuwa mfalme juu yetu, wewe ndiwe uliyewaongoza Israeli wakitoka nje kwenda, na kurudi vitani. Naye BWANA akakuambia, Wewe utawalisha watu wangu Israeli, nawe utakuwa mkuu juu ya Israeli.

BWANA atakulinda utokapo na uingiapo, Tangu sasa na hata milele.

Naye Sauli akasema, Mwambieni Daudi hivi, Mfalme hataki mahari yoyote, ila anataka govi mia moja za Wafilisti, ili ajilipize kisasi adui za mfalme. Basi Sauli alidhani kumwangamiza Daudi kwa mkono wa Wafilisti.

Naye Sauli akawaambia watumishi wake waliomzunguka, Sikieni sasa, enyi Wabenyamini; je! Huyu mwana wa Yese atawapa ninyi kila mmoja mashamba, na mashamba ya mizabibu, atawafanya kuwa wakuu wa watu maelfu, na wakuu wa watu mamia;

Naye atawaweka kwake kuwa wakuu juu ya maelfu, na makamanda juu ya hamsini hamsini; na wengine atawaweka walime shamba lake, na kuvuna mavuno yake, na kufanyiza zana zake za vita, na vyombo vya magari yake.