1 Samueli 17:16 - Swahili Revised Union Version Kwa siku arubaini yule Mfilisti alijitokeza na kusimama mbele asubuhi na jioni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa muda wa siku arubaini, asubuhi na jioni, yule Mfilisti Goliathi alijitokeza hadharani, akasimama na kuwakejeli wanajeshi wa Israeli. Biblia Habari Njema - BHND Kwa muda wa siku arubaini, asubuhi na jioni, yule Mfilisti Goliathi alijitokeza hadharani, akasimama na kuwakejeli wanajeshi wa Israeli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa muda wa siku arubaini, asubuhi na jioni, yule Mfilisti Goliathi alijitokeza hadharani, akasimama na kuwakejeli wanajeshi wa Israeli. Neno: Bibilia Takatifu Kwa siku arobaini huyo Mfilisti alikuwa akija mbele kila siku asubuhi na jioni na kujionesha. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa siku arobaini huyo Mfilisti alikuwa akija mbele kila siku asubuhi na jioni na kujionyesha. BIBLIA KISWAHILI Kwa siku arobaini yule Mfilisti alijitokeza na kusimama mbele asubuhi na jioni. |
Basi Daudi alikuwa akienda kwa Sauli na kurudi ili awalishe kondoo za baba yake huko Bethlehemu.
Ndipo Yese akamwambia Daudi mwanawe, Haya! Sasa wapelekee ndugu zako efa ya bisi, na mikate hii kumi, ipeleke upesi kambini kwa ndugu zako;