Ikawa, Ahiya alipoisikia sauti ya miguu yake, akiingia mlangoni, alisema, Karibu, mkewe Yeroboamu; mbona wajifanya kuwa mwingine maana nimetumwa kwako wewe, mwenye maneno mazito.
1 Samueli 15:16 - Swahili Revised Union Version Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Ngoja, nami nitakuambia neno aliloniambia BWANA usiku huu. Naye akamwambia, Haya, sema. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Samueli akamkatiza Shauli, “Nyamaza! Nitakuambia jambo aliloniambia Mwenyezi-Mungu leo usiku.” Shauli akasema, “Niambie.” Biblia Habari Njema - BHND Samueli akamkatiza Shauli, “Nyamaza! Nitakuambia jambo aliloniambia Mwenyezi-Mungu leo usiku.” Shauli akasema, “Niambie.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Samueli akamkatiza Shauli, “Nyamaza! Nitakuambia jambo aliloniambia Mwenyezi-Mungu leo usiku.” Shauli akasema, “Niambie.” Neno: Bibilia Takatifu Samweli akamwambia Sauli, “Ngoja! Nami nitakuambia lile Mwenyezi Mungu aliloniambia usiku huu.” Sauli akajibu, “Niambie.” Neno: Maandiko Matakatifu Samweli akamwambia Sauli, “Ngoja! Nami nitakuambia lile bwana aliloniambia usiku huu.” Sauli akajibu, “Niambie.” BIBLIA KISWAHILI Ndipo Samweli akamwambia Sauli, Ngoja, nami nitakuambia neno aliloniambia BWANA usiku huu. Naye akamwambia, Haya, sema. |
Ikawa, Ahiya alipoisikia sauti ya miguu yake, akiingia mlangoni, alisema, Karibu, mkewe Yeroboamu; mbona wajifanya kuwa mwingine maana nimetumwa kwako wewe, mwenye maneno mazito.
Mfalme akamwambia, Mara ngapi nikuapishe usiniambie neno ila yaliyo kweli, kwa jina la BWANA?
Basi Yeremia, nabii, akamwambia Sedekia, mfalme wa Yuda, maneno hayo yote katika Yerusalemu,
Basi sasa simameni, ili niwahutubie mbele za BWANA, kwa kutaja matendo yote ya haki ya BWANA, aliyowatendea ninyi na baba zenu.
Sauli akasema, Wamewaleta kutoka kwa Waamaleki; maana watu waliwaacha hai kondoo na ng'ombe walio wazuri, ili wawatoe dhabihu kwa BWANA, Mungu wako, nao waliosalia tumewaangamiza kabisa.
Basi Samweli akasema, Ingawa ulikuwa mdogo machoni pako mwenyewe, je! Hukufanywa kuwa kichwa cha makabila ya Israeli? Naye BWANA akakutia mafuta uwe mfalme wa Israeli.
Hata walipokuwa wakishuka kuelekea viunga vya mji, Samweli akamwambia Sauli, Mwambie mtumishi atutangulie, naye akitangulia, wewe nawe simama hapa kwa muda, ili nikuambie neno la Mungu.