Naye huyo mbebaji silaha akamjibu, Fanya yote yaliyomo moyoni mwako; angalia, mimi hapa ni pamoja nawe, moyo wangu ni kama moyo wako.
1 Samueli 14:8 - Swahili Revised Union Version Ndipo Yonathani akasema, Tazama, sisi tutavuka kwa watu hawa, na kujidhihirisha kwao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yonathani akamwambia, “Tutavuka kuwaendea wale watu ili wapate kutuona. Biblia Habari Njema - BHND Yonathani akamwambia, “Tutavuka kuwaendea wale watu ili wapate kutuona. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yonathani akamwambia, “Tutavuka kuwaendea wale watu ili wapate kutuona. Neno: Bibilia Takatifu Yonathani akasema, “Basi njoo; tutavuka kuwaelekea hao watu na kuacha watuone. Neno: Maandiko Matakatifu Yonathani akasema, “Basi njoo; tutavuka kuwaelekea hao watu na kuacha watuone. BIBLIA KISWAHILI Ndipo Yonathani akasema, Tazama, sisi tutavuka kwa watu hawa, na kujidhihirisha kwao. |
Naye huyo mbebaji silaha akamjibu, Fanya yote yaliyomo moyoni mwako; angalia, mimi hapa ni pamoja nawe, moyo wangu ni kama moyo wako.
Nao wakituambia hivi, Ngojeni, hadi sisi tuwafikie; ndipo tusimame pale pale mahali petu, tusiwaendee.