na jina lake mkewe Sauli aliitwa Ahinoamu, binti Ahimaasi. Tena, jina la jemadari wa jeshi lake aliitwa Abneri, mwana wa Neri, aliyekuwa baba mdogo wa Sauli.
1 Samueli 14:51 - Swahili Revised Union Version Na Kishi, babaye Sauli, na Neri, babaye Abneri, walikuwa wana wa Abieli. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Baba wa Shauli alikuwa Kishi na baba wa Abneri alikuwa Neri mwana wa Abieli. Biblia Habari Njema - BHND Baba wa Shauli alikuwa Kishi na baba wa Abneri alikuwa Neri mwana wa Abieli. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Baba wa Shauli alikuwa Kishi na baba wa Abneri alikuwa Neri mwana wa Abieli. Neno: Bibilia Takatifu Babaye Sauli, yaani Kishi, na Neri baba yake Abneri walikuwa wana wa Abieli. Neno: Maandiko Matakatifu Babaye Sauli yaani, Kishi na Neri baba yake Abneri walikuwa wana wa Abieli. BIBLIA KISWAHILI Na Kishi, babaye Sauli, na Neri, babaye Abneri, walikuwa wana wa Abieli. |
na jina lake mkewe Sauli aliitwa Ahinoamu, binti Ahimaasi. Tena, jina la jemadari wa jeshi lake aliitwa Abneri, mwana wa Neri, aliyekuwa baba mdogo wa Sauli.
Daudi akainuka, akafika mahali pale alipotua Sauli; Daudi akapaangalia mahali alipolala Sauli, na Abneri, mwana wa Neri, jemadari wa jeshi lake; naye Sauli alikuwa amelala kati ya magari, na hao watu wamepiga hema zao wakimzunguka.
Basi, kulikuwa na mtu mmoja wa Benyamini, jina lake akiitwa Kishi, mwana wa Abieli, mwana wa Serori, mwana wa Bekorathi, mwana wa Afia, mwana wa Mbenyamini, mtu shujaa, mwenye nguvu.
Basi Sauli akajibu, akasema, Je! Mimi si Mbenyamini, mtu wa kabila iliyo ndogo kuliko kabila zote za Israeli? Na jamaa yangu nayo si ndogo kuliko jamaa zote za kabila la Benyamini? Kwa nini basi, kuniambia hivyo?