Biblia Todo Logo
Mistari ya Biblia
- Matangazo -


99 Mistari ya Biblia kuhusu Haki ya Kijamii

99 Mistari ya Biblia kuhusu Haki ya Kijamii

Rafiki yangu, umewahi kujiuliza Mungu anataka nini kutoka kwetu? Biblia inatuambia katika Mika 6:8, "Ee mwanadamu, yeye amekuonyesha yaliyo mema, na BWANA anataka nini kwako: Kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako." Fikiria hilo. Kutenda haki si tu kufanya yaliyo sawa, bali ni kupenda rehema pia. Ni kuonyesha huruma na upendo kwa wengine kama vile Mungu anavyotuonyesha sisi. Na muhimu zaidi, ni kwenda kwa unyenyekevu na Mungu.

Tunajua Mungu anachukia dhambi. Yeye ni mtakatifu, na dhambi ni kinyume cha utakatifu wake. Tukifikiria ghadhabu ya Mungu dhidi ya dhambi, inatusaidia kuchukia dhambi pia. Hii ndiyo njia ya kuelekea utakatifu.

Kumcha Mungu siyo kuogopa adhabu tu, bali ni heshima kubwa kwake. Ni kutambua ukuu wake, utakatifu wake, na nguvu zake. Ni kumwabudu na kumsifu kama Mfalme wa wafalme. Ni yeye atakayetukomboa kutoka katika ghadhabu yake siku moja.

Lakini haki ya Mungu siyo tu kuhusu ghadhabu. Katika Isaya 42:1, tunasoma kuhusu mtumishi wa Mungu atakayeleta haki kwa mataifa. Haki hii siyo ya kulipiza kisasi, bali ni haki inayoleta uponyaji, uhuru, na amani. Ni haki inayotukumbusha upendo mkubwa wa Mungu kwetu.


Mika 6:8

Mungu amekuonesha yaliyo mema, ewe mtu; anachotaka Mwenyezi-Mungu kwako ni hiki: Kutenda mambo ya haki, kupenda kuwa na huruma, na kuishi kwa unyenyekevu na Mungu wako.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 56:1

Mwenyezi-Mungu asema: “Zingatieni haki na kutenda mema, maana nitawaokoeni hivi karibuni, watu wataona wazi kwamba ninawakomboeni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 1:17

jifunzeni kutenda mema. Tendeni haki, ondoeni udhalimu, walindeni yatima, teteeni haki za wajane.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Walawi 19:15

“Unapotoa hukumu uamue kwa haki; usimpendelee maskini wala kumwogopa mwenye cheo. Bali ni lazima kumwamua jirani kwa haki.

Sura   |  Matoleo Nakili
Amosi 5:24

Lakini acheni haki itiririke kama maji, uadilifu uwe kama mto usiokauka.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 10:1-2

Ole wao wanaotunga sheria zisizo za haki, watu wanaopitisha sheria za kukandamiza. Kama nimefaulu kuunyosha mkono wangu dhidi ya falme zenye sanamu za miungu kubwa kuliko sanamu za Yerusalemu na Samaria; je, nitashindwa kuutenda Yerusalemu na sanamu zake, kama nilivyoutenda Samaria na sanamu zake?” Wakati Mwenyezi-Mungu atakapomaliza kazi zake zote mlimani Siyoni na mjini Yerusalemu, atamwadhibu mfalme wa Ashuru, kwa sababu ya majivuno na kiburi chake. Maana mfalme wa Ashuru alisema: “Kwa nguvu zangu mwenyewe nimetenda hayo, na kwa hekima yangu, maana mimi ni mwerevu! Nimeondoa mipaka kati ya mataifa, nikazipora hazina zao; kama fahali nimewaporomosha walioketia viti vya enzi. Kama mtu anyoshaye mkono kwenye kiota, ndivyo nilivyochukua mali yao; kama mtu aokotavyo mayai yaliyoachwa kiotani, ndivyo nilivyowaokota duniani kote, wala hakuna mtu aliyeweza kupiga bawa, au aliyefungua kinywa kunipigia kelele.” Lakini Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Je, shoka litajigamba dhidi ya anayelitumia? Msumeno waweza kujivuna dhidi ya mwenye kukata nao? Ni kana kwamba fimbo ingeweza kumwinua anayeishika, au mkongojo kumwinua mwenye kuutumia!” Kwa hiyo, Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi, atawaletea askari wao ugonjwa wa kuwakondesha, na fahari yao itateketezwa kama kwa moto. Mungu aliye mwanga wa Israeli atakuwa kama moto, Mtakatifu wa Israeli atakuwa mwali wa moto ambao kwa siku moja utateketeza kila kitu: Miiba yake na mbigili zake pamoja. Misitu yake ya fahari na mashamba yake mazuri, Mwenyezi-Mungu atayaangamiza yote; itakuwa kama mtu aliyemalizwa na ugonjwa. Miti itakayobaki msituni mwake itakuwa michache sana hata mtoto mdogo ataweza kuihesabu. Huwanyima maskini haki zao, na kuwaibia maskini wa watu wangu maslahi yao. Wajane wamekuwa nyara kwao; yatima wamekuwa mawindo yao.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 16:20

Mtazingatia haki tu, ili mpate kuishi na kuimiliki nchi mnayopewa na Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zekaria 7:9

“Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema: Amueni kwa haki, muwe na upole na huruma nyinyi kwa nyinyi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 27:19

“ ‘Alaaniwe mtu yeyote anayepotosha haki ya mgeni au yatima au mjane’. Na watu wote wataitika, ‘Amina!’

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 31:9

Sema kwa ajili yao na kuamua kwa haki, linda haki za maskini na fukara.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 31:8-9

Lakini wewe, lazima useme kwa ajili ya wote walio bubu; na kutetea haki za wote wasiojiweza. Sema kwa ajili yao na kuamua kwa haki, linda haki za maskini na fukara.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 82:3-4

Wapeni wanyonge na yatima haki zao; tekelezeni haki za wanaoonewa na fukara. Waokoeni wanyonge na maskini, waokoeni makuchani mwa wadhalimu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yeremia 22:3

Mimi Mwenyezi-Mungu nasema hivi: Tendeni mambo ya haki na uadilifu. Mwokoeni mikononi mwa mdhalimu mtu yeyote aliyenyanganywa mali zake. Msiwatendee vibaya au ukatili wageni, yatima na wajane wala msimwage damu ya mtu asiye na hatia mahali hapa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 103:6

Mwenyezi-Mungu huhukumu kwa haki; huwajalia wanaodhulumiwa haki zao.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 22:22

Msimtese mjane au yatima.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 146:7-9

Yeye huwapatia wanaoonewa haki zao, huwapa wenye njaa chakula. Mwenyezi-Mungu huwapa wafungwa uhuru, huwafungua macho vipofu. Mwenyezi-Mungu huwainua waliokandamizwa; huwapenda watu walio waadilifu. Mwenyezi-Mungu huwalinda wageni, huwategemeza wajane na yatima; lakini huipotosha njia ya waovu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 4:18

“Roho wa Bwana yu juu yangu, kwani ameniweka wakfu niwaletee maskini Habari Njema. Amenituma niwatangazie mateka uhuru wao, na vipofu watapata kuona tena; amenituma niwakomboe wanaoonewa,

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 25:40

Mfalme atawajibu, ‘Kweli nawaambieni, kila kitu mlichomtendea mmojawapo wa hawa ndugu zangu wadogo, mlinitendea mimi.’

Sura   |  Matoleo Nakili
Yakobo 1:27

Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 21:15

Haki ikitekelezwa watu wema hufurahi, lakini watu waovu hufadhaishwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 72:1-4

Ee Mungu, umjalie mfalme uamuzi wako, umpe mwanamfalme uadilifu wako; Wafalme wa Tarshishi na visiwa wamlipe kodi, wafalme wa Sheba na Seba wamletee zawadi. Wafalme wote wa dunia wamheshimu, watu wa mataifa yote wamtumikie. Anamkomboa fukara anayemwomba, na maskini asiye na wa kumsaidia. Anawahurumia watu dhaifu na fukara, anayaokoa maisha yao wenye shida. Anawatoa katika udhalimu na ukatili, maana maisha yao ni ya thamani kubwa kwake. Mfalme na aishi maisha marefu; apokee zawadi ya dhahabu kutoka Sheba; watu wamwombee kwa Mungu daima, na kumtakia baraka mchana kutwa. Nchi na izae nafaka kwa wingi, vilima vijae mavuno kama ya Lebanoni, na watu mijini wastawi kama nyasi. Jina la mfalme litukuke daima; fahari yake idumu pindi liangazapo jua. Kwake mataifa yote yabarikiwe; watu wote wamwite mbarikiwa! Atukuzwe Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, ambaye peke yake hufanya miujiza. Jina lake tukufu na litukuzwe milele; utukufu wake ujae ulimwenguni kote! Amina, Amina! atawale taifa lako kwa haki, na maskini wako kwa uadilifu. Mwisho wa sala za Daudi, mwana wa Yese. Milima ilete fanaka kwa watu wako, vilima vijae uadilifu. Mfalme awatetee wanyonge wa taifa, awasaidie watoto wa fukara, na kuwaangamiza watu wadhalimu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 58:6-7

“La! Mfungo ninaotaka mimi ni huu: Kuwafungulia waliofungwa bila haki, kuziondoa kamba za utumwa, kuwaachia huru wanaokandamizwa, na kuvunjilia mbali udhalimu wote! Mfungo wa kweli ni kuwagawia wenye njaa chakula chako, kuwakaribisha nyumbani kwako maskini wasio na makao, kuwavalisha wasio na nguo, bila kusahau kuwasaidia jamaa zenu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mhubiri 3:16-17

Zaidi ya hayo, nimegundua duniani kwamba, mahali pa haki na uadilifu, uovu unatawala. Basi, nikasema moyoni mwangu, “Haidhuru! Mungu atawahukumu waadilifu, hali kadhalika na waovu, maana amepanga wakati maalumu kwa kila jambo na kwa kila kazi.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 12:19

Wapenzi wangu, msilipize kisasi, bali mwachieni Mungu jambo hilo; maana Maandiko Matakatifu yasema: “Kulipiza kisasi ni shauri langu; mimi nitalipiza, asema Bwana.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Wagalatia 6:2

Saidianeni kubeba mizigo yenu na hivyo mtatimiza sheria ya Kristo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 10:17-18

Ee Mwenyezi-Mungu, wapokea dua za mnyonge; wampa moyo na kumtegea sikio. Utawatendea haki yatima na wanaodhulumiwa, binadamu aliye udongo asiweze tena kuleta hofu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 23:6

“Usiipotoshe haki anayostahili maskini katika kesi yake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 61:8

“Mimi Mwenyezi-Mungu napenda haki; nachukia unyanganyi na uhalifu. Nitawatuza watu wangu kwa uaminifu, nitafanya nao agano la milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 14:31

Anayemdhulumu maskini anamtukana Muumba wake, lakini amwoneaye huruma mhitaji anamtukuza Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 37:28

maana Mwenyezi-Mungu hupenda uadilifu, wala hawaachi waaminifu wake. Huwalinda hao milele; lakini wazawa wa waovu wataangamizwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 7:12

“Yote mnayotaka watu wawatendee nyinyi, watendeeni wao vivyo hivyo. Hii ndiyo maana ya sheria ya Mose na mafundisho ya manabii.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 24:17

“Msipotoshe haki za wageni na yatima. Wala msichukue vazi la mjane kuwa rehani.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 29:7

Mwadilifu anajua haki za maskini, lakini mtu mwovu hajui mambo hayo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 6:31

Jinsi mnavyotaka watu wawatendee nyinyi, watendeeni wao vivyo hivyo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:119

Waovu wote wawaona kuwa takataka, kwa hiyo mimi napenda maamuzi yako.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Yohana 3:17

Basi, mtu akiwa na mali za hapa duniani, halafu akamwona ndugu yake ana shida, lakini akawa na moyo mgumu bila kumwonea huruma, anawezaje kusema kwamba anampenda Mungu?

Sura   |  Matoleo Nakili
Waebrania 13:16

Msisahau kutenda mema na kusaidiana, maana hizi ndizo tambiko zinazompendeza Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 37:21

Mtu mwovu hukopa bila kurudisha; lakini mwadilifu hutoa kwa ukarimu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 17:15

Kumsamehe mwenye hatia na kumwadhibu asiye na hatia yote mawili ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mika 3:1-2

Sasa sikilizeni enyi wakuu wa wazawa wa Yakobo, sikilizeni, enyi watawala wa wazawa wa Israeli! Nyinyi ndio mnaopaswa kujua mambo ya haki. Nyinyi mnajenga mji wa Siyoni kwa damu, naam, mji wa Yerusalemu kwa dhuluma. Waamuzi hufanya kazi yao kwa rushwa, makuhani wake hufundisha kwa malipo, manabii hutabiri kwa fedha. Hata hivyo hujidai kumtegemea Mwenyezi-Mungu, wakisema, “Mwenyezi-Mungu, si yupo pamoja nasi? Hatutapatwa na madhara yoyote!” Haya! Kwa sababu yenu, Siyoni utalimwa kama shamba, Yerusalemu utakuwa magofu, nao mlima wa hekalu utakuwa msitu. Lakini nyinyi mnachukia mema na kupenda maovu. Mnawachuna ngozi watu wangu, na kubambua nyama mifupani mwao.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 145:9

Mwenyezi-Mungu ni mwema kwa wote, ni mwenye huruma kwa viumbe vyake vyote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 13:1-4

Kila mtu anapaswa kuwatii wenye mamlaka katika serikali; maana mamlaka yote hutoka kwa Mungu; nao wenye mamlaka wamewekwa na Mungu. Ampendaye jirani yake hamtendei vibaya. Basi, upendo ni utimilifu wa sheria. Zaidi ya hayo, nyinyi mnajua tumo katika wakati gani: Sasa ndio wakati wa kuamka usingizini; naam, wokovu wetu uko karibu zaidi sasa kuliko wakati ule tulipoanza kuamini. Usiku unakwisha na mchana unakaribia. Basi, tutupilie mbali mambo yote ya giza, tukajitwalie silaha za mwanga. Na tuishi kwa adabu kama inavyostahili wakati wa mchana, na wala sio kwa ulafi na ulevi, uchafu na uasherati, ugomvi na wivu. Bwana Yesu Kristo awe vazi lenu; msishughulikie tena tamaa zenu za maumbile na kuziridhisha. Anayepinga mamlaka ya viongozi anapinga agizo la Mungu; nao wafanyao hivyo wanajiletea hukumu wenyewe. Maana, watawala hawasababishi hofu kwa watu wema, ila kwa watu wabaya. Basi, wataka usimwogope mtu mwenye mamlaka? Fanya mema naye atakusifu; maana yeye ni mtumishi wa Mungu anayefanya kazi kwa faida yako. Lakini ukifanya mabaya, basi, huna budi kumwogopa, maana anao kweli uwezo wa kuadhibu. Yeye ni mtumishi wa Mungu, kuwaonesha ghadhabu yake wale watendao maovu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 42:1-4

“Tazameni mtumishi wangu ninayemtegemeza; mteule wangu ambaye moyo wangu umependezwa naye. Nimeiweka roho yangu juu yake, naye atayaletea mataifa haki. Mwimbieni Mwenyezi-Mungu wimbo mpya! Dunia yote iimbe sifa zake: Bahari na vyote vilivyomo, nchi za mbali na wakazi wake; jangwa na miji yake yote ipaaze sauti, vijiji vya wakazi wa Kedari vimsifu, wakazi wa Sela waimbe kwa shangwe; wapaaze sauti kutoka mlimani juu. Wote wakaao nchi za mbali, na wamtukuze na kumsifu Mwenyezi-Mungu. Mwenyezi-Mungu ajitokeza kama shujaa; kama askari vitani ajikakamua kupigana. Anapaza sauti kubwa ya vita, na kujionesha mwenye nguvu dhidi ya maadui zake. Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Kwa muda mrefu sasa nimenyamaza, nimekaa kimya na kujizuia; lakini sasa nitalia kama mama anayejifungua, anayetweta pamoja na kuhema. Nitaharibu milima na vilima, na majani yote nitayakausha. Mito ya maji nitaigeuza kuwa nchi kavu, na mabwawa ya maji nitayakausha. “Nitawaongoza vipofu katika njia wasiyoifahamu, nitawaongoza katika njia ambazo hawazijui. Mbele yao giza nitaligeuza kuwa mwanga, na mahali pa kuparuza patakuwa laini. Huo ndio mpango wangu wa kufanya, nami nitautekeleza. Wote wanaotegemea sanamu za miungu, wote wanaoziambia: Nyinyi ni miungu yetu; watakomeshwa na kuaibishwa. “Sikilizeni enyi viziwi! Tazameni enyi vipofu, mpate kuona! Nani aliye kipofu ila mtumishi wangu? Nani aliye kiziwi kama mjumbe ninayemtuma? Ni nani aliye kipofu kama huyu niliyemweka wakfu, au kipofu kama mtumishi wa Mwenyezi-Mungu? Hatalia wala hatapiga kelele, wala hatapaza sauti yake barabarani. Nyinyi mmeona mambo mengi, lakini hamwelewi kitu. Masikio yenu yako wazi, lakini hamsikii kitu!” Mwenyezi-Mungu, kwa ajili ya uaminifu wake, alipenda kukuza mwongozo wake na kuutukuza. Lakini hawa ni watu walioibiwa mali na kuporwa! Wote wamenaswa mashimoni, wamefungwa gerezani. Wamekuwa kama mawindo bila mtu wa kuwaokoa, wamekuwa nyara na hakuna asemaye, “Waokolewe!” Je, mtatega sikio kusikia kitu hiki? Nani kati yenu atakayesikiliza vizuri yatakayotukia? Ni nani aliyewatia Waisraeli mikononi mwa adui zao? Nani aliyewaacha wanyanganywe mali zao? Ni Mwenyezi-Mungu ambaye tumemkosea! Wazee wetu walikataa kuzifuata njia zake, wala hawakuzitii amri zake. Kwa hiyo aliwamwagia hasira yake kali, akawaacha wakumbane na vita vikali. Hasira yake iliwawakia kila upande, lakini wao hawakuelewa chochote; iliwachoma, lakini hawakutilia jambo hilo maanani. Mwanzi uliochubuka hatauvunja, utambi ufukao moshi hatauzima; ataleta haki kwa uaminifu. Yeye hatafifia wala kufa moyo, hata atakapoimarisha haki duniani. Watu wa mbali wanangojea mwongozo wake.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 82:2-3

“Mpaka lini mtaendelea kuhukumu bila haki na kuwapendelea watu waovu? Wapeni wanyonge na yatima haki zao; tekelezeni haki za wanaoonewa na fukara.

Sura   |  Matoleo Nakili
Amosi 6:12

Je, farasi waweza kupiga mbio miambani? Je, watu huilima bahari kwa ng'ombe? Lakini nyinyi mmeigeuza haki kuwa sumu, na tunda la uadilifu kuwa uchungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 58:9

Ndipo mtakapoomba, nami Mwenyezi-Mungu nitawaitikia; mtalia kwa sauti kuomba msaada, nami nitajibu, ‘Niko hapa!’ “Kama mkiiondoa dhuluma kati yenu, mkiacha kudharau wengine na kusema maovu,

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 10:30-37

Yesu akamjibu, “Mtu mmoja alikuwa anashuka kutoka Yerusalemu kwenda Yeriko. Alipokuwa njiani, alivamiwa na majambazi, wakamnyanganya mali yake na kumpiga, wakamwacha amelala pale nusu mfu. Kumbe, kuhani mmoja akawa anapita barabara ileile, akamwona, akapita kando. Hali kadhalika na Mlawi mmoja, alipofika mahali hapo akamwona, akapita kando. Lakini Msamaria mmoja aliyekuwa anasafiri, alifika pale yule mtu alipokuwa, naye alipomwona, alimwonea huruma. Akamwendea, akamtibu majeraha yake kwa kumtia mafuta na divai na kuyafunga; halafu akampandisha juu ya punda wake, akampeleka katika nyumba moja ya wageni akamwuguza. Kesho yake akatoa fedha dinari mbili akampa yule mwenye nyumba, akamwambia, ‘Mwuguze mtu huyu; na chochote utakachotumia zaidi, nitakulipa nitakaporudi.’” Kisha Yesu akauliza, “Kati ya hao watatu, ni yupi aliyeonesha kuwa jirani yake yule aliyevamiwa na majambazi?” Yule mwalimu wa sheria akamjibu, “Ni yule aliyemwonea huruma.” Yesu akamwambia, “Nenda ukafanye vivyo hivyo.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 20:10

Mizani ya udanganyifu na vipimo vya udanganyifu, vyote ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 34:15

Mwenyezi-Mungu huwaangalia waadilifu, na kusikiliza malalamiko yao;

Sura   |  Matoleo Nakili
Mhubiri 5:8-9

Usishangae ukiona katika nchi watu fukara wanakandamizwa, wananyimwa haki zao na maslahi yao. Kila mwenye cheo anayewadhulumu wanyonge yupo chini ya mkuu mwingine, na juu ya hao wote kuna wakuu zaidi. Hata hivyo, mfalme akijishughulisha na kilimo ni manufaa kwa wananchi wote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 23:23

Ole wenu waalimu wa sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnatoza watu sehemu moja ya kumi, hata juu ya majani yenye harufu nzuri, bizari na jira, na huku mnaacha mambo muhimu ya sheria kama vile haki, huruma na imani. Haya ndio hasa mliyopaswa kuyazingatia bila kusahau yale mengine.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 2:6-8

Siku hiyo Mungu atamlipa kila mmoja kufuatana na matendo yake. Wale wanaozingatia kutenda mema, kutafuta utukufu na heshima ya Mungu na kutokufa, watapata uhai wa milele. Lakini wale wengine wenye ubinafsi, wenye kukataa mambo ya haki na kufuata uovu, wataangukiwa na ghadhabu na hasira ya Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 9:7-8

Lakini Mwenyezi-Mungu anatawala milele; ameweka kiti chake cha enzi apate kuhukumu. Anauhukumu ulimwengu kwa haki; anayaamua mataifa kwa unyofu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 21:22-25

“Wanaume wakipigana na kumwumiza mwanamke mjamzito, hata mimba yake ikaharibika bila madhara mengine zaidi, yule aliyemwumiza atatozwa faini kama atakavyodai mumewe mwanamke huyo na kama mahakimu watakavyoamua. Lakini kama yatakuwapo madhara mengine, basi, lazima amlipe uhai kwa uhai, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu, kuchomwa moto kwa kuchomwa moto, jeraha kwa jeraha, na pigo kwa pigo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 54:14

Utaimarika katika uadilifu, utakuwa mbali na dhuluma, nawe hutaogopa kitu; utakuwa mbali na hofu, maana haitakukaribia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 5:6

Heri wenye njaa na kiu ya kufanya atakavyo Mungu, maana watashibishwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wagalatia 5:13

Nyinyi ndugu, mliitwa muwe watu huru. Lakini uhuru huo usiwe kisingizio cha kutawaliwa na tamaa za kidunia; ila mnapaswa kutumikiana kwa upendo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:137

Ee Mwenyezi-Mungu, wewe ni mwadilifu; na hukumu zako ni za haki.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 14:13

Basi, tuache kuhukumiana, bali tuazimie kutokuwa kamwe kikwazo kwa ndugu au kumsababisha aanguke katika dhambi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 12:18

“Tazama mtumishi wangu niliyemteua, mpendwa wangu anipendezaye moyoni. Nitaiweka roho yangu juu yake, naye atatangaza hukumu yangu kwa mataifa yote.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 119:164

Nakusifu mara saba kila siku, kwa sababu ya maagizo yako adili.

Sura   |  Matoleo Nakili
1 Timotheo 6:17

Waamuru watu walio matajiri katika mambo ya maisha ya sasa, wasijivune, wasiweke tumaini lao katika mali isiyoweza kutegemewa; bali wamtegemee Mungu, ambaye kwa ukarimu hutupatia vitu vyote tuvifurahie.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 23:1-2

“Usitoe habari za uongo. Usishirikiane na mtu mwovu ili kuwa shahidi mbaya. “Kwa muda wa miaka sita utapanda mashamba yako na kuvuna mazao yake. Lakini mnamo mwaka wa saba, utayaacha mashamba yako bila kupanda mbegu, ili maskini miongoni mwa watu wako wapate chakula kilichosalia humo, na wanyama wa porini wale. Utafanya vivyo hivyo katika shamba lako la mizabibu na la mizeituni. “Kwa siku sita utafanya kazi zako, lakini siku ya saba utapumzika, ili ng'ombe wako na punda wako pia wapate kupumzika; na watumwa wako na watumishi wa kigeni wapate kustarehe. Yazingatie yote niliyokuambia. Usiyataje hata kidogo majina ya miungu mingine; hayo yasisikike kinywani mwako. “Mara tatu kila mwaka mtafanya sikukuu kwa heshima yangu. Mtaadhimisha sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu: Kama nilivyowaagiza, mtakula mikate isiyotiwa chachu kwa siku saba wakati uliopangwa katika mwezi wa Abibu, kwa sababu katika mwezi huo mlitoka Misri. Mtu yeyote asije mbele yangu mikono mitupu. Mtaadhimisha sikukuu ya mavuno ya kwanza ya kazi zenu na ya mavuno ya mashamba yenu. Mtaadhimisha sikukuu ya kukusanya mavuno mwishoni mwa mwaka mnapokusanya mazao ya kazi zenu. Mara tatu kwa mwaka wanaume wote watakusanyika mbele zangu mimi Bwana Mwenyezi-Mungu. “Usinitolee damu ya tambiko yangu pamoja na mkate uliotiwa chachu, wala usiyaache mafuta ya sikukuu yangu yabaki mpaka asubuhi. “Mazao ya kwanza ya ardhi yako utayaleta nyumbani kwangu mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wako. “Usimchemshe mwanakondoo au mwanambuzi katika maziwa ya mama yake. Usifuate genge la watu kutenda uovu, wala usijumuike na genge la watu kutoa ushahidi mahakamani ili kupotosha haki.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 18:1-8

Basi, Yesu aliwasimulia mfano kuonesha kwamba ni lazima kusali daima bila kukata tamaa. “Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali: Mmoja Mfarisayo, na mwingine mtozaushuru. Huyo Mfarisayo akasimama, akasali kimoyomoyo: ‘Ee Mungu, nakushukuru kwa vile mimi si kama watu wengine: Walafi, wadanganyifu au wazinzi. Nakushukuru kwamba mimi si kama huyu mtozaushuru. Nafunga mara mbili kwa juma, natoa zaka sehemu ya kumi ya pato langu.’ Lakini yule mtozaushuru, akiwa amesimama kwa mbali bila hata kuinua macho yake mbinguni, ila tu akijipiga kifua kwa huzuni, alisema: ‘Ee Mungu, unionee huruma mimi mwenye dhambi.’ Nawaambieni, huyu mtozaushuru alirudi nyumbani akiwa amesamehewa. Lakini yule mwingine, sivyo. Kwa maana kila anayejikweza atashushwa, na kila anayejishusha atakwezwa.” Watu walimletea Yesu watoto wadogo ili awawekee mikono yake. Wanafunzi walipowaona, wakawazuia kwa maneno makali. Lakini Yesu akawaita kwake akisema: “Waacheni hao watoto waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana ufalme wa Mungu ni kwa ajili ya watu kama hawa. Nawaambieni kweli, mtu yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hataingia katika ufalme huo.” Kiongozi mmoja, Myahudi, alimwuliza Yesu, “Mwalimu mwema, nifanye nini ili niweze kuupata uhai wa milele?” Yesu akamwambia, “Mbona waniita mwema? Hakuna aliye mwema ila Mungu peke yake. Alisema: “Katika mji mmoja kulikuwa na hakimu ambaye hakuwa anamcha Mungu wala kumjali binadamu. Unazijua amri: ‘Usizini; Usiue; Usiibe; Usitoe ushahidi wa uongo; Waheshimu baba yako na mama yako.’” Yeye akasema, “Hayo yote nimeyazingatia tangu ujana wangu.” Yesu aliposikia hayo, akamwambia, “Unatakiwa bado kufanya kitu kimoja: Uza kila kitu ulicho nacho, wagawie maskini hiyo fedha, nawe utakuwa na hazina yako mbinguni; halafu njoo unifuate.” Lakini huyo mtu aliposikia hayo, alihuzunika sana kwa sababu alikuwa tajiri sana. Yesu alipoona akihuzunika hivyo, akasema, “Jinsi gani ilivyo vigumu kwa matajiri kuingia katika ufalme wa Mungu! Naam, ni rahisi zaidi kwa ngamia kupita katika tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu.” Wale watu waliposikia hayo, wakasema, “Nani basi, atakayeokolewa?” Yesu akajibu, “Yasiyowezekana kwa binadamu, yanawezekana kwa Mungu.” Naye Petro akamwuliza, “Na sisi, je? Tumeacha vitu vyote tukakufuata!” Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, mtu yeyote aliyeacha nyumba au mke au ndugu au wazazi au watoto kwa ajili ya ufalme wa Mungu, Katika mji huohuo, kulikuwa pia na mama mmoja mjane ambaye alimwendea huyo hakimu mara nyingi akimwomba amtetee apate haki yake kutoka kwa adui yake. atapokea mengi zaidi wakati huu wa sasa, na uhai wa milele wakati ujao.” Yesu aliwachukua kando wale kumi na wawili, akawaambia, “Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu na huko kila kitu kilichoandikwa na manabii kuhusu Mwana wa Mtu kitakamilishwa. Kwa maana atakabidhiwa kwa watu wa mataifa nao watamtendea vibaya na kumtemea mate. Watampiga mijeledi na kumuua; lakini siku ya tatu atafufuka.” Lakini wao hawakuelewa jambo hilo hata kidogo; walikuwa wamefichwa maana ya maneno hayo, na hawakutambua yaliyosemwa. Wakati Yesu alipokaribia Yeriko, kulikuwa na mtu mmoja kipofu ameketi njiani akiomba. Aliposikia umati wa watu ukipita aliuliza, “Kuna nini?” Wakamwambia, “Yesu wa Nazareti anapita.” Naye akapaza sauti akisema, “Yesu, Mwana wa Daudi, nihurumie!” Wale watu waliotangulia wakamkemea wakimwambia anyamaze; lakini yeye akazidi kupaza sauti: “Mwana wa Daudi, nihurumie!” Kwa muda mrefu huyo hakimu hakupenda kumtetea huyo mjane; lakini, mwishowe akajisemea: ‘Ingawa mimi simchi Mungu wala simjali binadamu, Yesu alisimama, akaamuru wamlete mbele yake. Yule kipofu alipofika karibu, Yesu akamwuliza, “Unataka nikufanyie nini?” Naye akamjibu, “Bwana, naomba nipate kuona.” Yesu akamwambia, “Ona! Imani yako imekuponya.” Na mara huyo kipofu akapata kuona, akamfuata Yesu akimtukuza Mungu. Watu wote walipoona hayo, wakamsifu Mungu. lakini kwa vile huyu mjane ananisumbua, nitamtetea; la sivyo ataendelea kufika hapa, na mwisho atanichosha kabisa!’” Basi, Bwana akaendelea kusema, “Sikieni jinsi alivyosema huyo hakimu mbaya. Je, ndio kusema Mungu hatawatetea wale aliowachagua, ambao wanamlilia mchana na usiku? Je, atakawia kuwasikiliza? Nawaambieni atawatetea upesi. Hata hivyo, je, kutakuwako na imani duniani wakati Mwana wa Mtu atakapokuja?”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 72:12-14

Anamkomboa fukara anayemwomba, na maskini asiye na wa kumsaidia. Anawahurumia watu dhaifu na fukara, anayaokoa maisha yao wenye shida. Anawatoa katika udhalimu na ukatili, maana maisha yao ni ya thamani kubwa kwake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 28:5

Waovu hawajui maana ya haki, lakini wamchao Mwenyezi-Mungu wanaielewa kabisa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yakobo 2:14-17

Ndugu zangu, kuna faida gani mtu kusema ana imani, lakini haonyeshi kwa vitendo? Je, hiyo imani yawezaje kumwokoa? Tuseme kaka au dada hana nguo au chakula. Yafaa kitu gani nyinyi kuwaambia hao: “Nendeni salama mkaote moto na kushiba,” bila kuwapatia mahitaji yao ya maisha? Vivyo hivyo, imani peke yake bila matendo imekufa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 109:31

kwa maana yeye humtetea maskini, humwokoa wakati anapohukumiwa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 58:10-11

mkiwapa chakula kwa ukarimu wenye njaa, mkitosheleza mahitaji ya wenye dhiki, mwanga utawaangazia nyakati za giza, giza lenu litakuwa kama mchana. Mimi Mwenyezi-Mungu nitawaongozeni daima, nitatosheleza mahitaji yenu wakati wa shida. Nitawaimarisha mwilini, nanyi mtakuwa kama bustani iliyomwagiliwa maji, kama chemchemi ya maji ambayo maji yake hayakauki kamwe.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 3:11

Akawajibu, “Aliye na nguo mbili amgawie yule asiye na nguo; aliye na chakula afanye vivyo hivyo.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 15:1-2

Nani ee Mwenyezi-Mungu atakayekaa hemani mwako? Nani atakayeishi juu ya mlima wako mtakatifu? Ni mtu aishiye bila lawama, atendaye daima yaliyo mema, asemaye ukweli kutoka moyoni;

Sura   |  Matoleo Nakili
Kumbukumbu la Torati 10:18

Huwapa haki yatima na wajane; huwapenda wageni na kuwapa chakula na nguo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 7:1-2

“Msiwahukumu wengine, msije nanyi mkahukumiwa na Mungu; Au je, akimwomba samaki, atampa nyoka? Kama basi nyinyi, ingawa ni waovu, mwajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, hakika Baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi: Atawapa mema wale wanaomwomba. “Yote mnayotaka watu wawatendee nyinyi, watendeeni wao vivyo hivyo. Hii ndiyo maana ya sheria ya Mose na mafundisho ya manabii. “Ingieni kwa kupitia mlango mwembamba. Kwa maana njia inayoongoza kwenye maangamizi ni pana, na mlango wa kuingilia humo ni mpana; waendao njia hiyo ni wengi. Lakini njia inayoongoza kwenye uhai ni nyembamba, na mlango wa kuingilia humo ni mwembamba; ni watu wachache tu wanaoweza kuigundua njia hiyo. “Jihadharini na manabii wa uongo. Wao huja kwenu wakionekana kama kondoo kwa nje, lakini kwa ndani ni mbwamwitu wakali. Mtawatambua kwa matendo yao. Je, watu huchuma zabibu katika miti ya miiba, au tini katika mbigili? La! Basi, mti mzuri huzaa matunda mazuri, na mti mbaya huzaa matunda mabaya. Mti mzuri hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri. Kila mti usiozaa matunda mazuri utakatwa na kutupwa motoni. kwa maana jinsi mnavyowahukumu wengine, ndivyo nanyi mtakavyohukumiwa; na kipimo kilekile mnachotumia kwa wengine ndicho Mungu atakachotumia kwenu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 12:10

Pendaneni kindugu; kila mmoja amfikirie kwanza mwenzake kwa heshima.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 97:2

Mawingu na giza nene vyamzunguka; uadilifu na haki ni msingi wa utawala wake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 22:16

Anayemdhulumu maskini atamfanya afaidike mwishowe, anayewapa matajiri zawadi ataishia kuwa maskini.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 30:18

Hata hivyo, Mwenyezi-Mungu anangoja awafadhili, atainuka na kuwaonea huruma. Maana, Mwenyezi-Mungu ni Mungu atendaye haki. Heri wote wale wanaomtumainia.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 5:9

Heri wenye kuleta amani, maana wataitwa watoto wa Mungu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 82:4

Waokoeni wanyonge na maskini, waokoeni makuchani mwa wadhalimu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 14:17

Maana ufalme wa Mungu si shauri la kula na kunywa, bali unahusika na kuwa na uadilifu, amani na furaha iletwayo na Roho Mtakatifu.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 31:8-9

Wewe hukuniacha nitiwe mikononi mwa maadui zangu; umenisimamisha mahali pa usalama. Unionee huruma, ee Mwenyezi-Mungu, niko taabuni; macho yangu yamechoka kwa huzuni, nimeishiwa nguvu mwilini na rohoni.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 3:27-28

Usimnyime mtu anayehitaji msaada, ikiwa unao uwezo wa kufanya hivyo. Usimwambie jirani yako aende zake hadi kesho, hali wewe waweza kumpa anachohitaji leo.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 32:16-17

Haki itadumu katika nchi iliyokuwa nyika, uadilifu utatawala katika mashamba yenye rutuba. Kutokana na uadilifu watu watapata amani, utulivu na usalama utadumu milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 25:45

Naye atawajibu, ‘Nawaambieni kweli, kila mlipokataa kumtendea mambo haya mmojawapo wa hawa wadogo, mlikataa kunitendea mimi.’

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 19:7-9

Sheria ya Mwenyezi-Mungu ni kamilifu, humpa mtu uhai mpya; masharti ya Mwenyezi-Mungu ni thabiti, huwapa hekima wasio na makuu. Kanuni za Mwenyezi-Mungu ni sawa, huufurahisha moyo; amri ya Mwenyezi-Mungu ni safi, humwelimisha mtu. Kumcha Mwenyezi-Mungu ni jambo jema, na la kudumu milele; maagizo ya Mwenyezi-Mungu ni sawa, yote ni ya haki kabisa.

Sura   |  Matoleo Nakili
Kutoka 22:21-24

“Msimdhulumu mgeni wala kumtesa, maana nanyi pia mlikuwa wageni nchini Misri. Msimtese mjane au yatima. Kama mkiwadhulumu hao nao wakanililia, hakika nitakisikiliza kilio chao, na hasira yangu itawaka, nami nitawaueni kwa upanga, na wake zenu watakuwa wajane na watoto wenu yatima.

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 31:8

Lakini wewe, lazima useme kwa ajili ya wote walio bubu; na kutetea haki za wote wasiojiweza.

Sura   |  Matoleo Nakili
Isaya 49:25

Mwenyezi-Mungu ajibu: “Naam! Hata nyara za shujaa zitachukuliwa, mateka wa mtu katili wataokolewa. Mimi mwenyewe nitawakabili maadui zako, mimi mwenyewe nitawaokoa watoto wako.

Sura   |  Matoleo Nakili
Mika 2:1-2

Ole wao wanaopanga kutenda maovu wanaolala usiku wakiazimia uovu! Mara tu kunapopambazuka, wanayatekeleza kwani wanao uwezo. Inukeni mwende zenu! Hapa hamna tena pa kupumzika! Kwa utovu wenu wa uaminifu maangamizi makubwa yanawangojea! Kama mtu angetokea akatamka maneno matupu ya uongo na kusema: ‘Nawatabirieni divai na pombe kwa wingi’, mhubiri wa namna hiyo angependwa na watu hawa! “Lakini kweli nitawakusanya nyote enyi watu wa Yakobo, naam, nitawakusanya enyi Waisraeli mliobaki, niwalete pamoja kama kondoo katika zizi, kama kundi kubwa la kondoo malishoni; nanyi mtakuwa kundi la watu wengi.” Yule atakayetoboa njia atawatangulia, nao watalivunja lango la mji na kutoka nje, watapita na kutoka nje. Mfalme wao atawatangulia; Mwenyezi-Mungu mwenyewe atawatangulia. Hutamani mashamba na kuyatwaa; wakitaka nyumba, wananyakua. Huwadhulumu wenye nyumba na jamaa zao, huwanyang'anya watu mali zao.

Sura   |  Matoleo Nakili
Waroma 13:10

Ampendaye jirani yake hamtendei vibaya. Basi, upendo ni utimilifu wa sheria.

Sura   |  Matoleo Nakili
Luka 4:19

na kutangaza mwaka wa neema ya Bwana.”

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 146:6-7

aliyeumba mbingu na dunia, bahari na vyote vilivyomo. Yeye hushika ahadi yake milele. Yeye huwapatia wanaoonewa haki zao, huwapa wenye njaa chakula. Mwenyezi-Mungu huwapa wafungwa uhuru,

Sura   |  Matoleo Nakili
Mathayo 23:23-24

Ole wenu waalimu wa sheria na Mafarisayo, wanafiki! Mnatoza watu sehemu moja ya kumi, hata juu ya majani yenye harufu nzuri, bizari na jira, na huku mnaacha mambo muhimu ya sheria kama vile haki, huruma na imani. Haya ndio hasa mliyopaswa kuyazingatia bila kusahau yale mengine. Viongozi vipofu! Mnatoa nzi katika kinywaji, lakini mnameza ngamia!

Sura   |  Matoleo Nakili
Methali 29:14

Mfalme anayewaamua maskini kwa haki, atauona utawala wake umeimarika milele.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wagalatia 6:9

Basi, tusichoke kutenda mema; maana tusipolegea tutavuna mavuno kwa wakati wake.

Sura   |  Matoleo Nakili
Zaburi 37:5-6

Mkabidhi Mwenyezi-Mungu maisha yako; mtumainie yeye naye atafanya kitu. Ataufanya wema wako ungae kama mwanga, na uadilifu wako kama jua la adhuhuri.

Sura   |  Matoleo Nakili
Yakobo 4:17

Basi, mtu ambaye hafanyi lile jambo jema analojua kwamba anapaswa kulifanya, anatenda dhambi.

Sura   |  Matoleo Nakili
Wafilipi 2:3

Msifanye chochote kwa moyo wa fitina au kwa majivuno ya bure; muwe na unyenyekevu nyinyi kwa nyinyi, na kila mmoja amwone mwenzake kuwa bora kuliko yeye mwenyewe.

Sura   |  Matoleo Nakili

Maombi kwa Mungu

Ee Mungu wangu wa milele, mkuu na mwenye nguvu, wewe pekee ndiye unayestahili utukufu na heshima yote! Baba Mtakatifu, wewe ni mwema na hukumu zako ni za haki duniani, kwani wewe humpendelei mtu yeyote na kwa hakika haki yako si kama ya wanadamu. Bwana nisaidie kuelewa kwamba si jukumu langu kuhukumu wala kutoa hukumu, bali wewe pekee ndiye Mwamuzi. Pia nakuomba ulinde familia yangu, kanisa lako, jirani yangu na utende haki kwetu wakati wote. Mapenzi yako ni tuwe waadilifu, kwani chochote nitakachopanda ndicho nitakachovuna, neno lako linasema: "Usitende dhuluma katika hukumu, wala usimpendelee maskini wala kumfurahisha tajiri; kwa haki utamhukumu jirani yako." Bwana, nifundishe kutenda haki, nisaidie kufanya yaliyo mema kwa wengine, ili katika wakati huu mgumu uliojaa uovu na dhuluma, nijifunze kuweka tumaini langu lote kwako, ili nijue ya kuwa wewe ndiye mwamuzi wangu na mtetezi wangu. Uniokoe nisimuunge mkono asiye mwadilifu na kumshangilia mwovu, usiruhusu kinywa changu na moyo wangu kumsifu mwovu. Bwana, hakuna haki kubwa kama yako, kwani wewe pekee ndiye mwema, mwadilifu na bila ubaya wowote, uliwahesabia haki matajiri na maskini, weusi na wazungu, wajane na yatima. Bwana, asante, kwako utukufu na heshima. Kwa jina la Yesu, Amina!
Tufuate:

Matangazo


Matangazo