Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Zekaria 8:4 - Swahili Revised Union Version

4 BWANA wa majeshi asema hivi, Wazee wanaume na wazee wanawake watakaa tena katika njia za Yerusalemu, kila mtu akiwa ana mkongojo wake mkononi, kwa kuwa ni mzee sana.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema: Wazee, wanaume kwa wanawake, wataonekana tena wamekaa kwenye barabara za Yerusalemu, kila mmoja na mkongojo wake kwa sababu ya kuishi miaka mingi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema: Wazee, wanaume kwa wanawake, wataonekana tena wamekaa kwenye barabara za Yerusalemu, kila mmoja na mkongojo wake kwa sababu ya kuishi miaka mingi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nasema: Wazee, wanaume kwa wanawake, wataonekana tena wamekaa kwenye barabara za Yerusalemu, kila mmoja na mkongojo wake kwa sababu ya kuishi miaka mingi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Kwa mara nyingine tena wanaume na wanawake walioshiba umri wataketi katika barabara za Yerusalemu, kila mmoja akiwa na mkongojo wake mkononi kwa sababu ya umri wake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Hili ndilo asemalo bwana Mwenye Nguvu Zote: “Kwa mara nyingine tena wazee wanaume kwa wanawake walioshiba umri wataketi katika barabara za Yerusalemu, kila mmoja akiwa na mkongojo wake mkononi kwa sababu ya umri wake.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

4 BWANA wa majeshi asema hivi, Wazee wanaume na wazee wanawake watakaa tena katika njia za Yerusalemu, kila mtu akiwa ana mkongojo wake mkononi, kwa kuwa ni mzee sana.

Tazama sura Nakili

Zekaria 8:4
12 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Ayubu akafa, akiwa mzee sana mwenye kujawa na siku.

Utafika kaburini mwenye umri mtimilifu, Kama mganda wa ngano ulivyo wakati wake.

atakapoinuka tena na kuenenda nje kwa kutegemea fimbo, ndipo hapo yule aliyempiga ataachwa; ila atamlipa kwa ajili ya hayo majira yake yaliyompotea, naye atamwuguza hata apone kabisa.

Ndipo bikira atafurahi katika kucheza, na vijana na wazee pamoja; maana nitageuza masikitiko yao kuwa furaha, nami nitawafariji, na kuwafurahisha waache huzuni zao.

Na Yuda, na miji yake yote, watakaa humo pamoja; wakulima, nao waendao huku na huko pamoja na makundi yao.

naye akamwambia, Nenda mbio ukamwambie kijana huyu, na kusema, Yerusalemu utakaliwa na watu, kama vijiji visivyo na kuta, kwa sababu ya wingi wa watu na mifugo iliyomo ndani yake.

Bali ninyi mmeufikia mlima Sayuni, na mji wa Mungu aliye hai, Yerusalemu wa mbinguni, na majeshi ya malaika elfu nyingi,

Angalia, siku zinakuja, nitakapoukata mkono wako, na mkono wa watu wa ukoo wa baba yako, hata nyumbani mwako hapatakuwako mzee.

Nawe utayatazama mateso ya maskani yangu, katika utajiri wote watakaopewa Israeli; wala nyumbani mwako hapatakuwako mzee milele.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo