Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zekaria 7:14 - Swahili Revised Union Version

14 Lakini nitawatawanya kwa kimbunga kikali katikati ya mataifa yote wasiyoyajua. Basi nchi walioacha ikawa ya ukiwa, hata hapakuwa na mtu aliyeipitia akienda wala akirudi; maana waliifanya nchi iliyopendeza kuwa ukiwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

14 Nami niliwatawanya kwa kimbunga kati ya mataifa yote ambayo hawakuyajua. Hivyo nchi waliyoiacha ikabaki tupu; hapakuwa na mtu yeyote aliyekaa humo; naam, nchi hiyo ya kupendeza ikawa ukiwa.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

14 Nami niliwatawanya kwa kimbunga kati ya mataifa yote ambayo hawakuyajua. Hivyo nchi waliyoiacha ikabaki tupu; hapakuwa na mtu yeyote aliyekaa humo; naam, nchi hiyo ya kupendeza ikawa ukiwa.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

14 Nami niliwatawanya kwa kimbunga kati ya mataifa yote ambayo hawakuyajua. Hivyo nchi waliyoiacha ikabaki tupu; hapakuwa na mtu yeyote aliyekaa humo; naam, nchi hiyo ya kupendeza ikawa ukiwa.’”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

14 ‘Niliwatawanya kwa upepo wa kisulisuli miongoni mwa mataifa yote, mahali ambapo walikuwa wageni. Nchi ikaachwa ukiwa nyuma yao kiasi kwamba hakuna aliyeweza kuingia au kutoka. Hivi ndivyo walivyoifanya ile nchi iliyokuwa imependeza kuwa ukiwa.’ ”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

14 ‘Niliwatawanya kwa upepo wa kisulisuli miongoni mwa mataifa yote, mahali ambapo walikuwa wageni. Nchi ikaachwa ukiwa nyuma yao kiasi kwamba hakuna aliyeweza kuingia au kutoka. Hivi ndivyo walivyoifanya ile nchi iliyokuwa imependeza kuwa ukiwa.’ ”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

14 Lakini nitawatawanya kwa kimbunga kikali katikati ya mataifa yote wasiyoyajua. Basi nchi waliyoiacha ikawa ukiwa, hata hapakuwa na mtu aliyeipitia akienda wala akirudi; maana waliifanya nchi iliyopendeza kuwa ukiwa.

Tazama sura Nakili




Zekaria 7:14
35 Marejeleo ya Msalaba  

ili kulitimiza neno la BWANA kwa kinywa cha Yeremia, hata nchi itakapofurahia sabato zake; kwa maana siku zote ilipokaa ukiwa ilishika sabato, kutimiza miaka sabini.


Kabla ya masufuria yenu kupata moto wa miiba, Ataipeperusha kama chamchela, Iliyo mibichi na iliyo moto.


Mataifa wananguruma kama ngurumo ya maji mengi; Lakini atawakemea, nao watakimbia mbali sana, Watafukuzwa kama makapi milimani mbele ya upepo, Na kama mavumbi vuruvuru mbele ya tufani.


Ufunuo juu ya nyika kando ya bahari. Kama tufani za Negebu zikaribiavyo kwa kasi, inakuja kutoka kwa nyika, toka nchi itishayo.


Na kwa kuwa umeachwa na kuchukiwa, Hata ikawa hapana mtu aliyepita ndani yako, Nitakufanya kuwa fahari ya milele, Furaha ya vizazi vingi.


Maana BWANA atakuja na moto, na magari yake ya vita kama upepo wa kisulisuli; ili atoe malipo ya ghadhabu yake kwa moto uwakao, na maonyo yake kwa miali ya moto.


Wachungaji wengi wameliharibu shamba langu la mizabibu, wamelikanyaga fungu langu chini ya miguu yao, wamefanya fungu langu zuri kuwa jangwa la ukiwa.


Tazama, tufani ya BWANA, yaani, ghadhabu yake, imetokea; ni kimbunga cha tufani; itapasuka, na kuwaangukia waovu vichwani.


Tazama, tufani ya BWANA, yaani, ghadhabu yake, imetokea tufani ya kudumu; itawaangukia waovu vichwani.


Ndipo hao wakuu wakamwambia Baruku, Nenda ukajifiche, wewe na Yeremia, wala mtu asipajue mlipo.


Kwa sababu hiyo ghadhabu yangu, na hasira yangu, zilimwagika, nazo ziliwaka katika miji ya Yuda, na katika njia kuu za Yerusalemu, na miji hiyo imeachwa ukiwa, na kuharibika, kama ilivyo leo.


Angalia, nitaleta taifa juu yenu litokalo mbali sana, Ee nyumba ya Israeli, asema BWANA; ni taifa hodari, ni taifa la zamani sana, taifa ambalo hujui lugha yake, wala huyafahamu wasemayo.


katika mwaka wa ishirini na tatu wa Nebukadneza, Nebuzaradani, mkuu wa askari walinzi, akawachukua mateka katika Wayahudi watu mia saba na arubaini na watano; jumla ya watu hao wote ni watu elfu nne na mia sita.


ukawaambie watu wa nchi, Bwana MUNGU asema hivi, kuhusu habari zao wakaao Yerusalemu, na katika nchi ya Israeli; Watakula chakula chao kwa kukitunza sana, na maji yao watayanywa kwa ushangao, nchi yao iwe ukiwa, kwa kukosa vitu vyote viijazavyo, kwa sababu ya udhalimu wao wote wakaao ndani yake.


Nami nitakutawanya kati ya mataifa, na kukutapanya kati ya nchi mbalimbali; nami nitauteketeza uchafu wako, ili ukutoke.


Kwa sababu hiyo baba za watu watawala wana wao kati yako, nao wana watawala baba zao; nami nitafanya hukumu ndani yako, na hao wote waliosalia kwako nitawatawanya kwa pepo zote.


Na katika moja ya pembe hizo ilitokea pembe ndogo, iliyokua sana, upande wa kusini, na upande wa magharibi, na upande wa nchi ya uzuri.


Mungu wangu atawatupilia mbali, kwa sababu hawakumsikiliza; nao watakuwa watu wa kutangatanga kati ya mataifa.


Moto unaunguza vikali mbele yao; na nyuma yao miali ya moto inateketeza; hiyo nchi inafanana na bustani ya Edeni mbele yao, na nyuma yao imekuwa jangwa tupu; naam, hakuna aliyeokoka asipatikane nao.


Nami nitaleta wanyama wakali kati yenu, ambao watawanyang'anya watoto wenu, na kuwaharibu wanyama wenu wa kufugwa, na kuwapunguza hesabu yenu; na njia zenu zitakuwa ni ukiwa.


Nanyi nitawatapanyatapanya katika mataifa, nami nitaufuta upanga nyuma yenu; na nchi yenu itakuwa ni ukiwa, na miji yenu maganjo.


lakini nitawasha moto katika ukuta wa Raba, nao utayateketeza majumba yake; pamoja na kupiga kelele siku ya vita, pamoja na tufani katika siku ya chamchela;


BWANA si mwepesi wa hasira, ana uweza mwingi, wala hatamhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; BWANA ana njia yake katika kisulisuli na tufani, na mawingu ni mavumbi ya miguu yake.


Ukakichoma kichwa cha mashujaa wake kwa fimbo zao wenyewe; Wakaja kama kisulisuli ili kunitawanya; Kama wakifurahi kuwameza maskini kwa siri.


Nimekatilia mbali mataifa, minara yao ina ukiwa; nimeziharibu njia kuu zao, hata hapana mmoja apitaye; miji yao imeangamizwa; hamna mtu hata mmoja, wala hapana akaaye huko.


Haya! Haya! Ikimbieni nchi ya kaskazini, asema BWANA; kwa maana mimi nimewatawanya ninyi kama pepo nne za mbinguni, asema BWANA.


Neno la BWANA wa majeshi likanijia, kusema,


Naye BWANA ataonekana juu yao, Na mshale wake utatoka kama umeme; Na Bwana MUNGU ataipiga tarumbeta, Naye atakwenda kwa pepo za kisulisuli za kusini.


Matunda ya nchi yako, na taabu yako yote, vitaliwa na taifa usilolijua; utaonewa tu, na kupondwa chini daima;


BWANA atakuletea taifa juu yako kutoka mbali, kutoka ncha ya dunia, kama arukavyo tai; taifa usiloufahamu ulimi wake;


BWANA atakutawanya katika mataifa yote, tokea ncha hii ya dunia hata ncha hii ya dunia; nawe huko utatumikia miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako, nayo ni miti na mawe.


Na BWANA atawatawanya kati ya mataifa, nanyi mtasalia watu wachache kati ya makabila, mtakakopelekwa mbali na BWANA.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo