Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zekaria 10:1 - Swahili Revised Union Version

1 Mwombeni BWANA mvua wakati wa masika, naam, BWANA aletaye mawingu ya mvua, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi shambani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Mwombeni Mwenyezi-Mungu awape mvua za masika. Mwenyezi-Mungu ndiye aletaye mawingu ya mvua; ndiye awapaye watu mvua za rasharasha, na kustawisha mimea shambani kwa ajili ya wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Mwombeni Mwenyezi-Mungu awape mvua za masika. Mwenyezi-Mungu ndiye aletaye mawingu ya mvua; ndiye awapaye watu mvua za rasharasha, na kustawisha mimea shambani kwa ajili ya wote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Mwombeni Mwenyezi-Mungu awape mvua za masika. Mwenyezi-Mungu ndiye aletaye mawingu ya mvua; ndiye awapaye watu mvua za rasharasha, na kustawisha mimea shambani kwa ajili ya wote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Mwombeni Mwenyezi Mungu mvua wakati wa vuli; ndiye Mwenyezi Mungu atengenezaye mawingu ya tufani. Huwapa watu manyunyu ya mvua, pia mimea ya shambani kwa ajili ya kila mtu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Mwombeni bwana mvua wakati wa vuli; ndiye bwana atengenezaye mawingu ya tufani. Huwapa watu manyunyu ya mvua, pia mimea ya shambani kwa ajili ya kila mtu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

1 Mwombeni BWANA mvua wakati wa masika, naam, BWANA aletaye mawingu ya mvua, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi shambani.

Tazama sura Nakili




Zekaria 10:1
31 Marejeleo ya Msalaba  

Basi Eliya Mtishbi, wa wageni wa Gileadi, akamwambia Ahabu, Kama BWANA, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye ninasimama mbele zake, hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii, ila kwa neno langu.


Walikuwa wakiningojea kama kungojea mvua; Wakafunua vinywa vyao sana kama mvua ya masika.


Huinywesha milima toka juu angani; Nchi umeitosheleza kwa mazao ya kazi zako.


Ndiye apandishaye mvuke toka miisho ya nchi; Huifanyia mvua umeme; Hutoa upepo katika ghala zake.


Umeijia nchi na kuisitawisha, Umeitajirisha sana; Mto wa Mungu umejaa maji; Wawapa watu nafaka Maana ndiwe uitengenezaye ardhi.


Atashuka kama mvua juu ya majani yaliyokatwa, Kama manyunyu yainyweshayo nchi.


Kuna uhai katika nuru ya uso wa mfalme, Na fadhili zake ni kama wingu la masika.


Naye atatoa mvua juu ya mbegu zako, upate kuipanda nchi hii; na mkate wa mazao ya nchi, nayo itasitawi na kuzaa tele; katika siku hiyo ng'ombe wako watakula katika malisho mapana.


Kwa maana nitamimina maji juu yake aliye na kiu, na vijito vya maji juu ya mahali pakavu; nitamwaga roho yangu juu ya wazao wako, na baraka yangu juu yao utakaowazaa;


nami nitaliharibu; wala halitapogolewa wala kulimwa, bali litamea mbigili na miiba; nami nitayaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake.


Atoapo sauti yake, pana mshindo wa maji mbinguni, Naye hupandisha mawingu toka ncha za nchi; Huifanyia mvua umeme, Huutoa upepo katika hazina zake.


Je! Katika vitu vya ubatili vya mataifa, kiko kitu kiwezacho kuleta mvua? Je! Mbingu zaweza kutoa manyunyu? Je! Si wewe, Ee BWANA, Mungu wetu? Kwa sababu hiyo tutakungoja; kwa kuwa wewe umevifanya vitu hivi vyote.


Wala hawasemi mioyoni mwao, Basi, na tumche BWANA, Mungu wetu, aletaye mvua, mvua ya mwaka, na mvua ya vuli, kwa wakati wake; na kutuwekea majuma ya mavuno yaliyoamriwa.


Atoapo sauti yake pana kishindo cha maji mbinguni, Naye hupandisha mawingu toka ncha za nchi; Huifanyia mvua umeme, Huutoa upepo katika hazina zake.


Nami nitawafanya wao, na mahali palipo pande zote za mlima wangu, kuwa baraka, nami nitaleta manyunyu kwa wakati wake; yatakuwako manyunyu ya baraka.


Bwana MUNGU asema hivi, Tena kwa ajili ya jambo hili nitaulizwa na nyumba ya Israeli, ili niwatendee; nami nitawaongeza kwa watu kama kundi la kondoo.


Jipandieni katika haki, vuneni kwa fadhili; uchimbueni udongo wa mashamba yenu, kwa maana wakati umewadia wa kumtafuta BWANA, hata atakapokuja na kuwanyeshea haki.


Nasi na tujue, naam, tukaendelee kumjua BWANA; kutokea kwake ni yakini kama asubuhi; naye atatujia kama mvua, kama mvua ya vuli iinyweshayo nchi.


Tena nimeizuia mvua msiipate, ilipobaki miezi mitatu kabla ya mavuno; nami nimenyesha mvua juu ya mji mmoja, nikaizuia mvua isinyeshe juu ya mji mwingine; sehemu moja ilipata mvua, na sehemu isiyopata mvua ilikauka.


Na hayo mabaki ya Yakobo yatakuwa kati ya kabila nyingi mfano wa umande utokao kwa BWANA, mfano wa manyunyu katika nyasi; yasiyowategemea watu, wala kuwangojea wanadamu.


Tena siku ile hamtaniuliza neno lolote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lolote atawapa kwa jina langu.


Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu.


Na mbingu zako zilizo juu ya kichwa chako zitakuwa shaba, na nchi iliyo chini yako itakuwa chuma.


Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo