Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 32:1 - Swahili Revised Union Version

1 Heri aliyesamehewa dhambi, Na kuondolewa makosa yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Heri yake mtu aliyesamehewa kosa lake, mtu ambaye dhambi yake imeondolewa kabisa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Heri yake mtu aliyesamehewa kosa lake, mtu ambaye dhambi yake imeondolewa kabisa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Heri yake mtu aliyesamehewa kosa lake, mtu ambaye dhambi yake imeondolewa kabisa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Heri mtu aliyesamehewa makosa yake, ambaye dhambi zake zimefunikwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Heri mtu yule ambaye amesamehewa makosa yake, ambaye dhambi zake zimefunikwa.

Tazama sura Nakili




Zaburi 32:1
27 Marejeleo ya Msalaba  

Daudi akamwambia Nathani, Nimemfanyia BWANA dhambi. Nathani akamwambia Daudi, BWANA naye ameiondoa dhambi yako; hutakufa.


wala usiusitiri uovu wao, wala isifutwe dhambi yao, mbele zako; kwa maana wamekukasirisha mbele ya hao wanaojenga.


Akusamehe maovu yako yote, Akuponya magonjwa yako yote,


Heri washikao hukumu, Na kutenda haki sikuzote.


Heri kila mtu amchaye BWANA, Aendaye katika njia yake.


Heri aliyemfanya BWANA kuwa tumaini lake, Wala hakuwaelekea wenye kiburi, Wala hao wanaogeukia uongo.


Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu.


Moyo wangu umefurika kwa jambo jema, Mimi nasema niliyomfanyia mfalme; Ulimi wangu ni kama kalamu ya mwandishi stadi.


Kwa nini kujisifia uovu, Ewe jabari? Wema wa Mungu upo sikuzote.


Mpumbavu husema moyoni, Hakuna Mungu; Ni wafisadi, na wametenda mambo ya kuchukiza, Hakuna atendaye mema.


Ee Mungu, uisikilize sala yangu, Wala usijifiche nikuombapo rehema.


Ee BWANA wa majeshi, Heri mwanadamu anayekutumaini Wewe.


Umeusamehe uovu wa watu wako, Umezisitiri hatia zao zote.


Heri watu wale waijuao sauti ya shangwe, Ee BWANA, waendao, katika nuru ya uso wako.


Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama damu, zitakuwa kama sufu.


Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.


Nimeyafuta makosa yako kama wingu zito, na dhambi zako kama wingu; unirudie; maana nimekukomboa.


Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Baryona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.


Lakini yeye alisema, Afadhali, heri walisikiao neno la Mungu na kulishika.


Heri wazifuao nguo zao, ili wawe na haki ya kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo