Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 21:7 - Swahili Revised Union Version

7 Kwa kuwa mfalme humtumainia BWANA, Na kwa fadhili zake Aliye Juu hatatikisika.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Mfalme anamtumainia Mwenyezi-Mungu; kwa fadhili za Mungu Mkuu atakuwa salama.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Mfalme anamtumainia Mwenyezi-Mungu; kwa fadhili za Mungu Mkuu atakuwa salama.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Mfalme anamtumainia Mwenyezi-Mungu; kwa fadhili za Mungu Mkuu atakuwa salama.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Kwa kuwa mfalme anamtumaini Mwenyezi Mungu; kwa upendo usiokoma wa Aliye Juu Sana hatatikiswa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Kwa kuwa mfalme anamtumaini bwana; kwa upendo usiokoma wa Aliye Juu Sana hatatikiswa.

Tazama sura Nakili




Zaburi 21:7
17 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini mimi nimezitumainia fadhili zako; Moyo wangu na uufurahie wokovu wako.


Nimemweka BWANA mbele yangu daima, Kwa kuwa yuko kuliani mwangu, sitaondoshwa.


BWANA ni jabali langu, na boma langu, na mwokozi wangu, Mungu wangu, mwamba wangu ninayemkimbilia, Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, na ngome yangu.


Ee BWANA, unihukumu mimi, Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu, Nami nimemtumaini BWANA bila wasiwasi.


Jifungie upanga wako pajani, wewe uliye hodari, Utukufu ni wako na fahari ni yako.


Nitakaa katika hema yako milele, Na kupata kimbilio chini ya mbawa zako.


Jina lake na lidumu milele, Pindi ling'aapo jua, umaarufu wake uwepo; Mataifa yote na wabarikiwe katika yeye, Na kumwita heri.


Nitafurahi na kukushangilia; Nitaliimbia sifa jina lako, Wewe Uliye juu.


Atasema, BWANA ndiye kimbilio langu na ngome yangu, Mungu wangu nitakayemtumaini.


Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuangamizwa.


Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa, kama anamtaka; kwa maana alisema, Mimi ni Mwana wa Mungu.


Na tena, Nitakuwa nimemtumaini yeye. Na tena, Tazama, mimi nipo hapa na watoto niliopewa na Mungu.


Naye Daudi akafadhaika sana; kwa sababu watu walikuwa wakisema kwamba apigwe kwa mawe, kwa maana hao watu wote walisononeka, kila mtu kwa ajili ya wanawe na binti zake; lakini Daudi alijitia nguvu katika BWANA, Mungu wake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo