Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Zaburi 136:1 - Swahili Revised Union Version

1 Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Mshukuruni Mwenyezi-Mungu kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake zadumu milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Mshukuruni Mwenyezi-Mungu kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake zadumu milele.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Mshukuruni Mwenyezi-Mungu kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake zadumu milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Mshukuruni Mwenyezi Mungu, kwa kuwa ni mwema. Fadhili zake zadumu milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Mshukuruni bwana, kwa kuwa ni mwema. Fadhili zake zadumu milele.

Tazama sura Nakili




Zaburi 136:1
16 Marejeleo ya Msalaba  

Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele.


na pamoja nao Hemani na Yeduthuni, na wale wengine waliochaguliwa, waliotajwa majina yao, ili kumshukuru BWANA, kwa kuwa fadhili zake ni za milele;


Naye alipokwisha kufanya shauri na watu, akawaweka wale watakaomwimbia BWANA, na kumsifu katika uzuri wa utakatifu, wakitoka mbele ya jeshi, na kusema, Mshukuruni BWANA; kwa maana fadhili zake ni za milele.


Wana wa Israeli wote walipoona ule moto ukishuka, utukufu wa BWANA ulipokuwa katika nyumba, wakasujudu kifudifudi mpaka sakafuni, wakaabudu, wakamshukuru BWANA, wakisema, Kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake ni za milele.


Makuhani wakasimama kwenye nafasi zao walipoagizwa; Walawi nao pamoja na vinanda vya BWANA, alivyovifanya Daudi mfalme, ili kumshukuru BWANA, kwa maana fadhili zake ni za milele, hapo aliposifu Daudi kwa mikono yao; nao makuhani wakapiga panda mbele yao; nao Israeli wote wakasimama.


Wakaimbiana, wakimhimidi BWANA, na kumshukuru, wakasema, Kwa kuwa ni mwema, kwa maana fadhili zake kwa Israeli ni za milele. Kisha watu wote wakapaza sauti zao, na kupiga kelele, walipomhimidi BWANA, kwa sababu msingi wa nyumba ya BWANA umekwisha kuwekwa.


Maana BWANA ni mwema; Rehema zake ni za milele; Na uaminifu wake katika vizazi vyote.


Bali fadhili za BWANA ni kwa wamchao Tangu milele hata milele, Na haki yake ni kwa vizazi vyote;


Haleluya. Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake, Wajulisheni watu matendo yake.


Haleluya. Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.


Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.


Haleluya. Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.


Wewe U mwema na mtenda mema, Unifundishe amri zako.


itasikika tena sauti ya furaha na sauti ya shangwe, sauti ya bwana arusi na sauti ya bibi arusi, sauti yao wasemao Mshukuruni BWANA wa majeshi, maana BWANA ni mwema, rehema zake ni za milele; na sauti zao waletao sadaka za shukrani nyumbani kwa BWANA. Kwa kuwa nitawarudisha wafungwa wa nchi hii kama kwanza, asema BWANA.


Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi Kwa hao wanaomcha.


jilindeni katika upendo wa Mungu, huku mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo, hata mpate uzima wa milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo