Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Yoshua 8:31 - Swahili Revised Union Version

31 Kama Musa, mtumishi wa BWANA, alivyowaamuru wana wa Israeli, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Torati ya Musa, madhabahu ya mawe yasiyochongwa, ambayo mtu hakutumia juu yake chombo cha chuma; nao wakatoa juu yake sadaka za kuteketezwa kwa BWANA, na kuchinja sadaka za amani.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

31 kama Mose mtumishi wa Mwenyezi-Mungu alivyowaagiza Waisraeli, kadiri ilivyoandikwa katika kitabu cha sheria ya Mose kwamba itakuwa madhabahu iliyojengwa kwa mawe ambayo hayakuchongwa, wala kuguswa na chombo chochote cha chuma. Juu ya madhabahu hiyo walimtolea Mwenyezi-Mungu tambiko za kuteketezwa na sadaka za amani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

31 kama Mose mtumishi wa Mwenyezi-Mungu alivyowaagiza Waisraeli, kadiri ilivyoandikwa katika kitabu cha sheria ya Mose kwamba itakuwa madhabahu iliyojengwa kwa mawe ambayo hayakuchongwa, wala kuguswa na chombo chochote cha chuma. Juu ya madhabahu hiyo walimtolea Mwenyezi-Mungu tambiko za kuteketezwa na sadaka za amani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

31 kama Musa mtumishi wa Mwenyezi Mungu alivyokuwa amewaamuru Waisraeli. Akaijenga sawasawa na ilivyoandikwa katika Kitabu cha Torati ya Musa: madhabahu ya mawe yasiyochongwa, ambayo juu yake hakuna chombo cha chuma kilichotumika. Hapo juu yake wakamtolea Mwenyezi Mungu sadaka za kuteketezwa na kutoa sadaka za amani.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

31 kama Musa mtumishi wa bwana alivyokuwa amewaamuru Waisraeli. Akaijenga sawasawa na ilivyoandikwa katika Kitabu cha Torati ya Musa: madhabahu ya mawe yasiyochongwa, ambayo juu yake hakuna chombo cha chuma kilichotumika. Hapo juu yake wakamtolea bwana sadaka za kuteketezwa na kutoa sadaka za amani.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

31 Kama Musa, mtumishi wa BWANA, alivyowaamuru wana wa Israeli, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Torati ya Musa, madhabahu ya mawe yasiyochongwa, ambayo mtu hakutumia juu yake chombo cha chuma; nao wakatoa juu yake sadaka za kuteketezwa kwa BWANA, na kuchinja sadaka za amani.

Tazama sura Nakili

Yoshua 8:31
16 Marejeleo ya Msalaba  

ila hakuwaua watoto wa hao wauaji; kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Torati ya Musa, kama alivyoamuru BWANA, akisema, Mababa wasife kwa makosa ya wana, wala wana wasife kwa makosa ya mababa; lakini kila mtu atakufa kwa kosa lake mwenyewe.

Naye Hilkia, kuhani mkuu, akamwambia Shafani, mwandishi, Nimekiona kitabu cha Torati katika nyumba ya BWANA. Hilkia akampa Shafani kile kitabu, naye akakisoma.

Lakini watoto wao hakuwaua, ila alifanya kulingana na hayo yaliyoandikwa katika Torati, katika kitabu cha Musa, kama BWANA alivyoamuru, akisema, Wazazi wasiuawe kwa ajili ya dhambi ya watoto wao wala watoto wasiuawe kwa ajili ya dhambi ya wazazi; lakini kila mtu atakufa kwa dhambi yake mwenyewe.

Wakaziondoa sadaka za kuteketezwa, wawape watu kama makundi yalivyo kwa kufuata nyumba za nasaba zao, ili wamtolee BWANA, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Musa. Nao ng'ombe wakawafanya vivyo hivyo.

Wakawaweka makuhani katika sehemu zao, wakawaweka na Walawi katika zamu zao, kwa ajili ya huduma ya Mungu, iliyokuwako Yerusalemu; kama ilivyoandikwa katika chuo cha Musa.

Siku hiyo walisoma katika kitabu cha Musa masikioni mwa watu; na ndani yake yalionekana maneno haya yameandikwa, ya kwamba Mwamoni na Mmoabi wasiingie katika kusanyiko la Mungu milele;

Yethro mkwewe Musa akamletea Mungu sadaka ya kuteketezwa na dhabihu; na Haruni akaja, na wazee wote wa Israeli, wale chakula pamoja na mkwewe Musa mbele za Mungu.

akapeleka vijana wa wana wa Israeli, waliotoa sadaka za kuteketezwa, wakamchinjia BWANA sadaka za amani za ng'ombe.

Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje?

Na iwe, siku mtakayovuka Yordani kwenda nchi akupayo BWANA, Mungu wako, ujisimamishie mawe makubwa, ukayatalize matalizo,

Kisha, andika juu ya mawe hayo maneno ya torati hii yote, waziwazi sana.

Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda kulingana na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo