Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yoshua 7:11 - Swahili Revised Union Version

11 Israeli wamefanya dhambi, naam, wamelivunja agano langu nililowaagiza; naam, wametwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; tena wameiba, tena wameficha na kuvitia pamoja na vitu vyao wenyewe.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

11 Waisraeli wametenda dhambi, maana wamelivunja agano langu nililowaamuru washike; wamevichukua baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu viangamizwe; wameviiba na kudanganya, wakaviweka pamoja na vitu vyao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

11 Waisraeli wametenda dhambi, maana wamelivunja agano langu nililowaamuru washike; wamevichukua baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu viangamizwe; wameviiba na kudanganya, wakaviweka pamoja na vitu vyao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

11 Waisraeli wametenda dhambi, maana wamelivunja agano langu nililowaamuru washike; wamevichukua baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu viangamizwe; wameviiba na kudanganya, wakaviweka pamoja na vitu vyao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

11 Israeli ametenda dhambi. Wamekiuka agano langu nililowaamuru kulishika. Wamechukua baadhi ya vitu vilivyotengwa kwa ajili ya kuangamizwa; wameiba, wamesema uongo, na wameviweka pamoja na mali yao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

11 Israeli ametenda dhambi. Wamekiuka agano langu nililowaamuru kulishika. Wamechukua baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu, wameiba, wamesema uongo, wameviweka pamoja na mali zao.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

11 Israeli wamefanya dhambi, naam, wamelivunja agano langu nililowaagiza; naam, wametwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; tena wameiba, tena wamevificha na kuvitia pamoja na vitu vyao wenyewe.

Tazama sura Nakili




Yoshua 7:11
24 Marejeleo ya Msalaba  

kwa sababu hawakuitii sauti ya BWANA, Mungu wao, bali waliyavunja maagano yake, mambo yote ambayo Musa mtumishi wa BWANA aliwaamuru, wasikubali kuyasikiliza, wala kuyatenda.


Naye alipofika kilimani, alivichukua kutoka mikononi mwao, akaviweka nyumbani; akawaacha wale watu kuondoka, nao wakaenda zao.


Tena dunia imetiwa unajisi kwa watu wanaoikaa; kwa maana wameziasi sheria, wameibadili amri, wamelivunja agano la milele.


Si kwa mfano wa agano lile nililolifanya na baba zao, katika siku ile nilipowashika mkono, ili kuwatoa katika nchi ya Misri; ambalo agano langu hilo walilivunja, ingawa nilikuwa mume kwao, asema BWANA.


Lakini wao wamelivunja hilo agano kama Adamu; huko wamenitenda mambo ya hiana.


Mtu awaye yote akiasi na kufanya dhambi naye hakukusudia, katika mambo matakatifu ya BWANA; ndipo atakapomletea BWANA sadaka yake ya hatia, kondoo dume mkamilifu katika kundi lake; sawasawa na hesabu utakayomwandikia katika shekeli za fedha, kwa shekeli ya mahali patakatifu, kuwa sadaka ya hatia;


Je! Hawa wote hawatapiga mfano juu yake, na mithali ya kusimanga juu yake, wakisema, Ole wake yeye aongezaye kisicho mali yake! Hata lini? Na ole wake yeye ajitwikaye mzigo wa rehani!


Nitaituma itokee, asema BWANA wa majeshi, nayo itaingia katika nyumba ya mwizi, na katika nyumba ya yeyote aapaye kwa uongo kwa jina langu; nayo itakaa katika nyumba yake, na kuiteketeza, pamoja na boriti zake na mawe yake.


Wakamwambia, Ni ya Kaisari. Akawaambia, Basi, mpeni Kaisari yaliyo ya Kaisari, na Mungu yaliyo ya Mungu.


Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe.


Ikiwa ameonekana katikati yako, ndani ya malango yako mojawapo, upewayo na BWANA, Mungu wako, mtu mume au mke afanyaye yaliyo maovu machoni pa BWANA, Mungu wako, kwa kuvunja maagano yake,


Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, maana vitu vyote ni tupu na kuwekwa wazi machoni pake yeye ambaye tunapaswa kuwajibika kwake.


Hapo mtakapolivunja agano la BWANA, Mungu wenu, alilowaamuru, na kwenda kuitumikia miungu mingine, na kujiinamisha mbele yao, ndipo hasira ya BWANA itakapowaka juu yenu, nanyi mtaangamia upesi katika nchi hii njema aliyowapa.


Lakini Waisraeli walifanya dhambi katika kitu kilichowekwa wakfu; maana Akani, mwana wa Karmi, mwana wa Zabdi, mwana wa Zera, wa kabila la Yuda, alitwaa baadhi ya vitu vilivyowekwa wakfu; hasira ya BWANA ikawaka juu ya Waisraeli.


BWANA akamwambia Yoshua, Haya! Inuka, mbona umeanguka kifudifudi hivi?


Basi hasira ya BWANA ikawaka juu ya Israeli, naye akasema, Kwa kuwa taifa hili limelivunja agano langu nililowaamuru baba zao, wala hawakuisikiliza sauti yangu;


Ndipo Sauli akasema, Karibieni hapa, enyi wakuu wote wa watu; mjue na kuona dhambi hii ya leo imekuwa katika kosa gani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo