Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Yoshua 6:26 - Swahili Revised Union Version

26 Naye Yoshua akawaapisha kiapo wakati ule, akasema, Na alaaniwe na BWANA mtu yule atakayeinuka na kutaka kuujenga tena mji huu wa Yeriko; atakayeweka msingi wake mzaliwa wake wa kwanza na afe. Tena atakayesimamisha malango yake mtoto wake wa kiume aliye mdogo na afe.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Wakati huo Yoshua alitamka apizo rasmi mbele ya watu akisema, “Atakayeujenga tena mji wa Yeriko, na alaaniwe na Mungu, Yeyote atakayeweka msingi wa mji huo, mzaliwa wake wa kwanza na afe. Yeyote atakayejenga lango la mji huo, mwanawe kitinda mimba na afe.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Wakati huo Yoshua alitamka apizo rasmi mbele ya watu akisema, “Atakayeujenga tena mji wa Yeriko, na alaaniwe na Mungu, Yeyote atakayeweka msingi wa mji huo, mzaliwa wake wa kwanza na afe. Yeyote atakayejenga lango la mji huo, mwanawe kitinda mimba na afe.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Wakati ule Yoshua akatamka kiapo hiki akasema, “Na alaaniwe mbele za Mwenyezi Mungu mtu atakayeinuka kuujenga tena mji huu wa Yeriko: “Kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza wa kiume ataiweka misingi yake; kwa gharama ya mtoto wake wa mwisho atayaweka malango yake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Wakati ule Yoshua akatamka kiapo hiki akasema, “Aliyelaaniwa mbele za bwana ni mtu atakayeinuka kuujenga tena mji huu wa Yeriko: “Kwa gharama ya mzaliwa wake wa kwanza wa kiume ataiweka misingi yake; kwa gharama ya mtoto wake wa mwisho atayaweka malango yake.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

26 Naye Yoshua akawaapisha kiapo wakati ule, akasema, Na alaaniwe na BWANA mtu yule atakayeinuka na kutaka kuujenga tena mji huu wa Yeriko; atakayeweka msingi wake mzaliwa wake wa kwanza na afe. Tena atakayesimamisha malango yake mtoto wake wa kiume aliye mdogo na afe.

Tazama sura Nakili

Yoshua 6:26
9 Marejeleo ya Msalaba  

Katika siku zake, Hieli Mbetheli akajenga Yeriko; akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, na kuyaweka malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo Segubu; sawasawa na neno la BWANA alilolinena kwa Yoshua mwana wa Nuni.

Mfalme akamwambia, Mara ngapi nikuapishe usiniambie neno ila yaliyo kweli, kwa jina la BWANA?

Eliya akamwambia, Tafadhali, kaa hapa, Elisha; maana BWANA amenituma niende mpaka Yeriko. Akasema, Kama BWANA aishivyo, na roho yako iishivyo, sitakuacha. Nao wakafika Yeriko.

Ijapokuwa Edomu asema, Tumepondwapondwa, lakini tutarudi na kupajenga mahali palipoachwa hali ya ukiwa; BWANA wa majeshi asema hivi, Wao watajenga, bali mimi nitaangusha; na watu watawaita, Mpaka wa uovu, na, Watu ambao BWANA anawaghadhabikia milele.

Lakini, Yesu akanyamaza. Kuhani Mkuu akamwambia, Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu.

Baadhi ya Wayahudi wenye kutangatanga, nao ni wapunga pepo, wakajaribu kutaja jina la Bwana Yesu juu yao waliopagawa na pepo wachafu, wakisema, Nawaapisha kwa Yesu, yule anayehubiriwa na Paulo.

kisha uliteremka kutoka Yanoa hadi Atarothi, na Naara, kisha ukafika Yeriko, na kutokea hapo penye mto wa Yordani.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo