Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Yoshua 22:25 - Swahili Revised Union Version

25 Kwa kuwa yeye BWANA ameufanya huu mto wa Yordani uwe mpaka katikati yetu nanyi, enyi wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, hamna fungu katika BWANA; basi hivyo wana wenu wangeweza kuwafanya wana wetu waache kumwabudu BWANA.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Hamwoni kwamba Mwenyezi-Mungu ameweka mto wa Yordani kuwa mpaka kati yenu na sisi? Nyinyi makabila ya Reubeni na kabila la Gadi hamna fungu lolote lenu kwa Mwenyezi-Mungu.’ Hivyo watoto wenu wangeweza baadaye kusababisha watoto wetu waache kumwabudu Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Hamwoni kwamba Mwenyezi-Mungu ameweka mto wa Yordani kuwa mpaka kati yenu na sisi? Nyinyi makabila ya Reubeni na kabila la Gadi hamna fungu lolote lenu kwa Mwenyezi-Mungu.’ Hivyo watoto wenu wangeweza baadaye kusababisha watoto wetu waache kumwabudu Mwenyezi-Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Mwenyezi Mungu ameifanya Yordani kuwa mpaka kati yetu na ninyi, ninyi Wareubeni na Wagadi! Hamna fungu kwa Mwenyezi Mungu.’ Kwa hiyo wazao wenu wanaweza wakawasababisha wazao wetu wakaacha kumcha Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 bwana ameifanya Yordani kuwa mpaka kati yetu na ninyi, ninyi Wareubeni na Wagadi! Hamna fungu kwa bwana.’ Kwa hiyo wazao wenu wanaweza wakawasababisha wazao wetu wakaacha kumcha bwana.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

25 Kwa kuwa yeye BWANA ameufanya huu mto wa Yordani uwe mpaka katikati yetu nanyi, enyi wana wa Reubeni, na wana wa Gadi, hamna fungu katika BWANA; basi hivyo wana wenu wangeweza kuwafanya wana wetu waache kumwabudu BWANA.

Tazama sura Nakili

Yoshua 22:25
13 Marejeleo ya Msalaba  

Basi ilitukia ya kwamba kulikuwapo mtu asiyefaa, jina lake akiitwa Sheba, mwana wa Bikri, Mbenyamini; naye akapiga tarumbeta, akasema, Sisi hatuna sehemu katika Daudi, wala hatuna urithi katika mwana wa Yese; nendeni kila mtu hemani kwake, enyi Israeli.

Basi Israeli wote walipoona ya kuwa mfalme hakuwasikia, hao watu walimjibu mfalme, wakasema, Tuna sehemu gani katika Daudi? Wala hatuna urithi katika mwana wa Yese. Haya! Nendeni zenu hemani kwenu, enyi Israeli; sasa itunze nyumba yako mwenyewe, Ee Daudi. Hivyo Israeli wakaenda zao hemani kwao.

Naye atawatoa Israeli kwa ajili ya makosa ya Yeroboamu, aliyoyakosa, ambayo kwa hayo amewakosesha Israeli.

kwa sababu ya makosa yake Yeroboamu aliyoyakosa, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli; kwa sababu ya chukizo lake alilomchukiza BWANA, Mungu wa Israeli, hata kumghadhibisha.

Ndipo nikawajibu, nikawaambia, Mungu wa mbinguni, yeye atatufanikisha; kwa hiyo sisi, watumishi wake, tutaondoka na kujenga; lakini ninyi hamna sehemu, wala haki, wala kumbukumbu, katika Yerusalemu.

BWANA ndiye fungu la posho langu, Na la kikombe changu; Wewe unayaamua maisha yangu.

Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu.

au kama sisi tumefanya jambo hili kwa hofu kuwa, katika siku zijazo wana wenu huenda wakanena na wana wetu na kusema, Ninyi mna uhusiano gani na BWANA, Mungu wa Israeli?

Kwa ajili ya hayo tulisema, Natujijengee madhabahu, si kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa, wala kwa sadaka yoyote;

bali iwe ushahidi kati yetu nanyi, tena kati ya vizazi vyetu baada yetu, kwamba sisi tunamhudumia BWANA kwa njia ya sadaka zetu za kuteketezwa, na kwa dhabihu zetu, na kwa sadaka zetu za amani; ili kwamba wana wenu wasiwaambie wana wetu katika siku zijazo, Ninyi hamna fungu katika BWANA.

Basi sasa, nakusihi, bwana wangu, mfalme, na asikie maneno ya mtumishi wake. Ikiwa ni BWANA aliyekuchochea juu yangu, na akubali sadaka; bali ikiwa ni wanadamu, na walaaniwe mbele za BWANA; kwa sababu wamenifukuza leo, nisishikamane na urithi wa BWANA, wakisema, Nenda, ukatumikie miungu mingine.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo