Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yoshua 19:51 - Swahili Revised Union Version

51 Hizi ndizo nchi, ambazo Eleazari kuhani, na Yoshua huyo mwana wa Nuni, pamoja na hao vichwa vya nyumba za mababa ya makabila ya Waisraeli, walizigawanya kwa njia ya kupiga kura, ziwe urithi, huko Shilo mbele ya BWANA, hapo mlangoni mwa hema ya kukutania. Basi hivyo wakamaliza kazi ya kuigawanya hiyo nchi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

51 Basi, kuhani Eleazari na Yoshua, mwana wa Nuni, pamoja na viongozi wa makabila ya Waisraeli waligawa sehemu hizo kwa kura mbele ya Mwenyezi-Mungu mlangoni mwa hema la mkutano huko Shilo. Basi, wakakamilisha kuigawa nchi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

51 Basi, kuhani Eleazari na Yoshua, mwana wa Nuni, pamoja na viongozi wa makabila ya Waisraeli waligawa sehemu hizo kwa kura mbele ya Mwenyezi-Mungu mlangoni mwa hema la mkutano huko Shilo. Basi, wakakamilisha kuigawa nchi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

51 Basi, kuhani Eleazari na Yoshua, mwana wa Nuni, pamoja na viongozi wa makabila ya Waisraeli waligawa sehemu hizo kwa kura mbele ya Mwenyezi-Mungu mlangoni mwa hema la mkutano huko Shilo. Basi, wakakamilisha kuigawa nchi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

51 Haya ndio maeneo ambayo kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa koo za makabila ya Israeli waliyagawanya kwa kura huko Shilo mbele za Mwenyezi Mungu, penye ingilio la Hema la Kukutania. Hivyo wakamaliza kuigawanya nchi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

51 Haya ndiyo maeneo ambayo kuhani Eleazari, Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa koo za kabila za Israeli waliyoyagawanya kwa kura huko Shilo mbele za bwana penye ingilio la Hema la Kukutania. Hivyo wakamaliza kuigawanya nchi.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

51 Hizi ndizo nchi, ambazo Eleazari kuhani, na Yoshua huyo mwana wa Nuni, pamoja na hao vichwa vya nyumba za mababa wa makabila ya Waisraeli, walizigawanya kwa njia ya kupiga kura, ziwe urithi, huko Shilo mbele za BWANA, hapo mlangoni pa hema ya kukutania. Basi hivyo wakamaliza kazi ya kuigawanya hiyo nchi.

Tazama sura Nakili




Yoshua 19:51
18 Marejeleo ya Msalaba  

Fimbo ya enzi haitaondoka katika Yuda, Wala mfanya sheria kati ya miguu yake, Hata atakapokuja Yeye, mwenye milki, Ambaye mataifa watamtii.


Akaiacha maskani ya Shilo, Hema aliyoiweka katikati ya wanadamu;


Akawaambia, Hakika mtakinywea kikombe changu; lakini kuketi mkono wangu wa kulia na mkono wangu wa kushoto, sina amri kuwapa, bali watapewa waliowekewa tayari na Baba yangu.


Kisha Mfalme atawaambia wale walioko katika mkono wake wa kulia, Njooni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu;


kama vile ulivyompa mamlaka juu ya watu wote, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele.


Na alipokwisha kuwaangamiza mataifa saba katika nchi ya Kanaani akawapa nchi yao iwe urithi kwa muda wa miaka kama mia nne na hamsini;


Kisha hizi ndizo nchi ambazo wana wa Israeli walizitwaa katika nchi ya Kanaani, ambazo Eleazari kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni, na vichwa vya nyumba za mababa wa makabila ya Israeli, waliwagawanyia,


Kisha mkutano mzima wa wana wa Israeli walikutana pamoja hapo Shilo, wakasimamisha hema ya kukutania huko; nayo nchi ilikuwa imeshindwa mbele zao.


Kisha Yoshua akapiga kura kwa ajili yao hapo mbele za BWANA katika Shilo; huko Yoshua akawagawanyia wana wa Israeli hiyo nchi sawasawa na mafungu yao.


Kisha BWANA akanena na Yoshua, na kumwambia,


Kisha wakasema, Angalieni, iko sikukuu ya BWANA mwaka baada ya mwaka katika Shilo, mji ulio upande wa kaskazini mwa Betheli, upande wa mashariki mwa hiyo njia kuu iendeayo kutoka Betheli kwenda Shekemu, nao ni upande wa kusini mwa Lebona.


kaeni macho; kisha tazameni, kisha hao binti za Shilo watakapotoka ili wacheze katika hiyo michezo, basi tokeni mizabibuni, na kila mtu na ajishikie mke katika hao binti za Shilo, kisha mrudi katika nchi ya Benyamini.


Na mtu huyo alikuwa akikwea kutoka mjini kwake mwaka kwa mwaka, ili kuabudu, na kumtolea BWANA wa majeshi dhabihu katika Shilo. Na wale wana wawili wa Eli, Hofni na Finehasi, makuhani wa BWANA, walikuwako huko.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo