Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Yoshua 17:18 - Swahili Revised Union Version

18 lakini hiyo nchi ya vilima itakuwa ni yako; maana, ijapokuwa sasa ni msitu, wewe utaufyeka, na kuimiliki yote hadi mwisho wake; kwa kuwa wewe utawafukuza hao Wakanaani, wajapokuwa wana magari ya chuma, wajapokuwa ni wenye uwezo.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 bali pia nchi ya milima itakuwa yenu. Ingawa sasa ni msitu, mtaifyeka na kuimiliki yote toka upande huu hadi upande mwingine. Mtawaondoa Wakanaani, hata kama wana magari ya chuma na ni wenye nguvu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 bali pia nchi ya milima itakuwa yenu. Ingawa sasa ni msitu, mtaifyeka na kuimiliki yote toka upande huu hadi upande mwingine. Mtawaondoa Wakanaani, hata kama wana magari ya chuma na ni wenye nguvu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 bali pia nchi ya milima itakuwa yenu. Ingawa sasa ni msitu, mtaifyeka na kuimiliki yote toka upande huu hadi upande mwingine. Mtawaondoa Wakanaani, hata kama wana magari ya chuma na ni wenye nguvu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 bali pia nchi hii ya vilima yenye msitu. Ifyekeni, nayo mipaka yake itakuwa yenu umbali mtakaoweza kufika. Ingawa Wakanaani wana magari ya vita ya chuma, na wana nguvu, mtaweza kuwafukuza humo.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 bali pia nchi hii ya kilima yenye msitu. Ifyekeni, nayo mipaka yake itakuwa yenu umbali mtakaoweza kufika. Ingawa Wakanaani wana magari ya chuma, nao wana nguvu, mwaweza kuwafukuza humo.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

18 lakini hiyo nchi ya vilima itakuwa ni yako; maana, ijapokuwa sasa ni msitu, wewe utaufyeka, na kuimiliki yote hadi mwisho wake; kwa kuwa wewe utawafukuza hao Wakanaani, wajapokuwa wana magari ya chuma, wajapokuwa ni wenye uwezo.

Tazama sura Nakili

Yoshua 17:18
18 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini upinde wake ukakaa imara, Mikono yake ikapata nguvu, Kwa mikono ya Mwenye Enzi wa Yakobo; Kwa jina la mchungaji, yeye mwamba wa Israeli,

Hivyo watu wakatoka waende nyikani ili kupigana na Israeli; na vita vikatokea ndani ya msitu wa Efraimu.

Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani awezaye kutupinga?

Lakini katika mambo hayo yote sisi ni zaidi ya washindi, kupitia kwake yeye aliyetupenda.

Mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe wake mume, enzi ni yake; Na pembe zake ni pembe za nyati; Kwa hizo atayasukuma mataifa yote, hata ncha za nchi; Nao ni makumi ya maelfu ya Efraimu, Nao ni maelfu ya Manase.

Hata tunathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?

na watu wote wenye kukaa nchi za vilima kutoka Lebanoni hadi Misrefoth-maimu, maana, hao Wasidoni wote; hao wote nitawafukuza watoke mbele ya wana wa Israeli; lakini wewe uwape Israeli kuwa ni urithi wao, kama nilivyokuamuru.

kisha mpaka ulipigwa kutoka juu ya mlima huo hadi kufika chemchemi ya maji ya Neftoa kisha ukatokea hata miji ya kilima cha Efroni; kisha mpaka ulipigwa hadi kufika Baala (ndio Kiriath-yearimu);

Kisha Yoshua alinena na nyumba ya Yusufu, maana, ni Efraimu na Manase, akawaambia, Wewe u taifa kubwa la watu, nawe una uwezo mwingi; hutapata sehemu moja tu;

Nao wakaweka Kedeshi katika Galilaya katika nchi ya vilima ya Naftali, na Shekemu katika nchi ya vilima ya Efraimu, na Kiriath-arba (ndio Hebroni) katika nchi ya vilima ya Yuda.

Palikuwa na mtu mmoja wa Rama, Msufi, wa nchi ya milima milima ya Efraimu, jina lake akiitwa Elkana, mwana wa Yerohamu, mwana wa Elihu, mwana wa Tohu, mwana wa Sufu, Mwefraimu

Tufuate:

Matangazo

Matangazo