Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yoshua 14:6 - Swahili Revised Union Version

6 Wakati huo wana wa Yuda walimwendea Yoshua hapo Gilgali; na Kalebu, mwana wa Yefune, huyo Mkenizi, akamwambia, Wewe wajua hilo neno BWANA alilomwambia Musa, huyo mtu wa Mungu, katika habari zangu, na katika habari zako wewe, tulipokuwa katika Kadesh-barnea.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Siku moja watu wa kabila la Yuda walimwendea Yoshua huko Gilgali. Kalebu mwana wa Yefune, ambaye alikuwa Mkenizi, akamwambia Yoshua, “Bila shaka unakumbuka jinsi Mwenyezi-Mungu alivyomwambia Mose, mtu wa Mungu, juu yangu na wewe tulipokuwa Kadesh-barnea:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Siku moja watu wa kabila la Yuda walimwendea Yoshua huko Gilgali. Kalebu mwana wa Yefune, ambaye alikuwa Mkenizi, akamwambia Yoshua, “Bila shaka unakumbuka jinsi Mwenyezi-Mungu alivyomwambia Mose, mtu wa Mungu, juu yangu na wewe tulipokuwa Kadesh-barnea:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Siku moja watu wa kabila la Yuda walimwendea Yoshua huko Gilgali. Kalebu mwana wa Yefune, ambaye alikuwa Mkenizi, akamwambia Yoshua, “Bila shaka unakumbuka jinsi Mwenyezi-Mungu alivyomwambia Mose, mtu wa Mungu, juu yangu na wewe tulipokuwa Kadesh-barnea:

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Kisha watu wa Yuda wakamwendea Yoshua huko Gilgali, naye Kalebu mwana wa Yefune yule Mkenizi, akamwambia, “Unajua jambo ambalo Mwenyezi Mungu alimwambia Musa mtu wa Mungu huko Kadesh-Barnea kukuhusu wewe na mimi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Kisha watu wa Yuda wakamwendea Yoshua huko Gilgali, naye Kalebu mwana wa Yefune yule Mkenizi, akamwambia, “Unajua jambo ambalo bwana alimwambia Musa mtu wa Mungu huko Kadesh-Barnea kukuhusu wewe na mimi.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

6 Wakati huo wana wa Yuda walimwendea Yoshua hapo Gilgali; na Kalebu, mwana wa Yefune, huyo Mkenizi, akamwambia, Wewe wajua hilo neno BWANA alilomwambia Musa, huyo mtu wa Mungu, katika habari zangu, na katika habari zako wewe, tulipokuwa katika Kadesh-barnea.

Tazama sura Nakili




Yoshua 14:6
30 Marejeleo ya Msalaba  

Na tazama, akatoka mtu wa Mungu katika Yuda kwa neno la BWANA, akafika Betheli. Naye Yeroboamu alikuwa akisimama penye madhabahu, afukize uvumba.


Akamfuata mtu wa Mungu, akamkuta ameketi chini ya mwaloni, akamwambia, Je! Wewe ndiwe yule mtu wa Mungu aliyetoka katika Yuda? Akamwambia, Mimi ndiye.


Akasema, Panapo wakati huu mwakani, utamkumbatia mwana. Akasema, La! Bwana wangu, wewe mtu wa Mungu, usiniambie mimi mjakazi wako uongo.


Tena, akaja mtu kutoka Baal-shalisha, akamletea mtu wa Mungu chakula cha malimbuko, mikate ishirini ya shayiri, na masuke mabichi ya ngano guniani. Akasema, Uwape watu, ili wale.


Yule mwanamke akamwambia mumewe, Tazama, mimi naona ya kuwa mtu huyu apitaye kwetu mara kwa mara ni mtu mtakatifu wa Mungu.


Akamkazia macho hata akatahayari; na yule mtu wa Mungu akalia machozi.


Kisha, Elisha akaenda Dameski; na Ben-hadadi, mfalme wa Shamu, alikuwa mgonjwa; akaambiwa ya kwamba, Yule mtu wa Mungu amefika hapa.


Lakini kwa habari za Musa, mtu wa Mungu, wanawe hutajwa miongoni mwa kabila la Lawi.


Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, Kizazi baada ya kizazi.


nikawaleta ndani ya nyumba ya BWANA, ndani ya chumba cha wana wa Hanani, mwana wa Igdalia, mtu wa Mungu, kilichokuwa karibu na chumba cha wakuu, nacho kilikuwa juu ya chumba cha Maaseya, mwana wa Shalumu, bawabu;


Wakaenda wakafika kwa Musa, na kwa Haruni, na kwa mkutano wote wa wana wa Israeli, katika jangwa la Parani, huko Kadeshi; wakawaletea habari, wao na mkutano wote, wakawaonesha matunda ya nchi.


Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa, akasema, Na tupande mara moja tukaimiliki; maana twaweza kushinda bila shaka.


Katika kabila la Yuda, Kalebu mwana wa Yefune.


lakini mtumishi wangu Kalebu, kwa kuwa alikuwa na roho nyingine ndani yake, naye amenifuata kwa moyo wote, nitamleta yeye mpaka nchi hiyo aliyoingia; na wazao wake wataimiliki.


hakika yangu hamtaingia ninyi katika nchi, ambayo niliapa kwa kuinua mkono wangu, kwamba nitawafanyia makao humo, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni.


Na Yoshua mwana wa Nuni, na Kalebu mwana wa Yefune, waliokuwa miongoni mwao walioipeleleza nchi, wakararua nguo zao;


Kwa kuwa BWANA alisema juu yao, Hapana budi watakufa nyikani. Napo hapakusalia mtu mmoja miongoni mwao, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni.


ila Kalebu mwana wa Yefune, Mkenizi, na Yoshua mwana wa Nuni; kwa kuwa wao wamemwandama BWANA kwa moyo wote.


Hii ndiyo baraka ya Musa, huyo mtu wa Mungu, aliyowabarikia wana wa Israeli kabla ya kufa kwake.


Wala hajainuka tena katika Israeli nabii kama Musa, ambaye BWANA alimjua uso kwa uso;


Basi Musa, mtumishi wa BWANA, akafa huko, katika nchi ya Moabu, kwa neno la BWANA.


Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, subira, upole.


ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.


Kisha Yoshua akarudi, na Israeli wote pamoja naye, hata kambi yao huko Gilgali.


Kwa hiyo Hebroni ukawa urithi wa Kalebu, mwana wa Yefune, Mkenizi hata hivi leo, kwa sababu, alikuwa mwaminifu kwa BWANA, Mungu wa Israeli.


Naye Othnieli mwana wa Kenazi, nduguye Kalebu, aliutwaa; basi akampa Aksa binti yake awe mkewe.


Na hao watu wakakwea kutoka Yordani siku ya kumi ya mwezi wa kwanza, wakapiga kambi Gilgali, katika mpaka wa mashariki wa Yeriko.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo