Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yoshua 11:20 - Swahili Revised Union Version

20 Kwa kuwa lilikuwa ni la BWANA kuifanya mioyo yao kuwa migumu, hata wakatoka kupigana na Israeli, ili apate kuwaangamiza kabisa, wasihurumiwe lakini apate kuwaangamiza, kama vile BWANA alivyomwamuru Musa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Ilikuwa ni matakwa ya Mwenyezi-Mungu mwenyewe kuishupaza mioyo ya watu wa mataifa hayo ili wapigane. Alikusudia wasihurumiwe ila wateketezwe. Ndivyo Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Ilikuwa ni matakwa ya Mwenyezi-Mungu mwenyewe kuishupaza mioyo ya watu wa mataifa hayo ili wapigane. Alikusudia wasihurumiwe ila wateketezwe. Ndivyo Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Ilikuwa ni matakwa ya Mwenyezi-Mungu mwenyewe kuishupaza mioyo ya watu wa mataifa hayo ili wapigane. Alikusudia wasihurumiwe ila wateketezwe. Ndivyo Mwenyezi-Mungu alivyomwamuru Mose.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Kwa maana Mwenyezi Mungu mwenyewe ndiye aliifanya mioyo yao iwe migumu, ili kupigana vita dhidi ya Israeli, ili apate kuwaangamiza kabisa, awafutilie mbali pasipo huruma, kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Kwa maana bwana mwenyewe ndiye aliifanya mioyo yao iwe migumu, ili kupigana vita dhidi ya Israeli ili apate kuwafutilia mbali pasipo huruma, kama bwana alivyomwagiza Musa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

20 Kwa kuwa lilikuwa kusudi la BWANA kuifanya mioyo yao kuwa migumu, hata wakatoka kupigana na Israeli, ili apate kuwaangamiza kabisa, wasihurumiwe lakini apate kuwaangamiza, kama vile BWANA alivyomwamuru Musa.

Tazama sura Nakili




Yoshua 11:20
24 Marejeleo ya Msalaba  

Naye Absalomu na watu wote wa Israeli wakasema, Ushauri wa Hushai, Mwarki, ni mwema kuliko ushauri wa Ahithofeli. Kwa maana BWANA alikuwa amekusudia kuuvunja ushauri mwema wa Ahithofeli, ili BWANA alete mabaya juu ya Absalomu.


Basi mfalme hakuwasikia wale watu; maana jambo hili lilitoka kwa BWANA, ili alitimize neno lake, BWANA alilomwambia Yeroboamu mwana wa Nebati kwa kinywa cha Ahiya Mshiloni.


Basi kuangamia kwake Ahazia kulitokana na Mungu, kwa vile alivyomwendea Yoramu; kwa kuwa alipofika, akatoka pamoja na Yoramu juu ya Yehu mwana wa Nimshi, ambaye BWANA alimtia mafuta ili awakatilie mbali nyumba ya Ahabu.


Ikawa, aliposema naye, mfalme akamwambia, Je! Tumekutia wewe kuwa mshauri wa mfalme? Nyamaza; kwa nini upigwe? Ndipo yule nabii akaacha, akasema, Najua ya kuwa Mungu amekusudia kukuangamiza, kwa sababu umeyafanya haya, wala hukulisikiliza shauri langu.


BWANA akamwambia Musa, Ingia wewe kwa Farao; kwa kuwa mimi nimeufanya moyo wake mzito, nipate kuzionesha ishara zangu hizi kati yao;


Musa na Haruni walifanya ajabu hizo zote mbele ya Farao; BWANA akaufanya moyo wa Farao kuwa mgumu, asiwape wana wa Israeli ruhusa watoke nchi yake.


Nami, tazama, nitaifanya mioyo ya Wamisri kuwa migumu, nao wataingia na kuwafuatia, nami nitajipatia utukufu kwa Farao, na kwa jeshi lake lote, kwa magari yake na kwa wapanda farasi wake.


Nami nitaufanya uwe mgumu moyo wa Farao, naye atafuata nyuma yao; nami nitajipatia utukufu kwa Farao, na kwa jeshi lake lote; na Wamisri watajua ya kuwa mimi ndimi BWANA. Basi wakafanya hivyo.


Na BWANA akaufanya moyo wake Farao mfalme wa Misri kuwa mgumu, naye akawafuata wana wa Israeli; kwa sababu wana wa Israeli walitoka kwa jeuri.


BWANA akamwambia Musa, Hapo utakaporudi Misri, angalia ukazifanye mbele ya Farao zile ajabu zote nilizozitia mkononi mwako; lakini nitaufanya mgumu moyo wake, naye hatawapa ruhusa hao watu waende zao.


BWANA akaufanya mgumu moyo wa Farao, asiwasikize; vile vile kama BWANA alivyomwambia Musa.


lakini, nilikusimamisha wewe kwa sababu ii hii, ili nikuoneshe uweza wangu, tena kwamba jina langu litangazwe katika dunia yote.


BWANA wa majeshi ameapa, akisema, Hakika yangu kama vile vilivyoazimia, ndivyo itakavyokuwa; na kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyotokea;


Maana BWANA ana ghadhabu juu ya mataifa yote, na hasira kali juu ya jeshi lao lote; amewaangamiza kabisa, amewatoa waende kuchinjwa.


Basi, kama ni hivyo, atakaye kumrehemu humrehemu, na atakaye kumfanya mgumu humfanya mgumu.


Lakini Sihoni mfalme wa Heshboni hakutuacha kupitia kwake; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, alifanya roho yake kuwa ngumu, akamtia ukaidi moyoni mwake, apate kumtia mkononi mwako kama alivyo hivi leo.


Nawe angamiza mataifa yote atakayokupa BWANA, Mungu wako; jicho lako lisiwahurumie, wala usiitumikie miungu yao; kwani jambo hilo litakuwa ni mtego kwako.


Lakini baba yake na mama yake hawakujua ya kuwa jambo hili ni la BWANA; maana alitaka kisa juu ya Wafilisti. Basi wakati ule Wafilisti walikuwa wakiwatawala Israeli.


Mtu mmoja akimkosea mwenzake, Mungu atamhukumu; lakini mtu akimkosea BWANA, ni nani atakayemtetea? Lakini hawakuisikia sauti ya baba yao, kwa sababu BWANA amekusudia kuwaua.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo