Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yohana 20:9 - Swahili Revised Union Version

9 Kwa maana hawajalifahamu bado andiko, ya kwamba imempasa kufufuka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Walikuwa bado hawajaelewa Maandiko Matakatifu yaliyosema kwamba ilikuwa lazima afufuke kutoka kwa wafu).

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Walikuwa bado hawajaelewa Maandiko Matakatifu yaliyosema kwamba ilikuwa lazima afufuke kutoka kwa wafu).

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Walikuwa bado hawajaelewa Maandiko Matakatifu yaliyosema kwamba ilikuwa lazima afufuke kutoka kwa wafu).

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 (Kwa kuwa hadi wakati huo walikuwa bado hawajaelewa kutoka Maandiko kwamba ilikuwa lazima Isa afufuke kutoka kwa wafu.)

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 (Kwa kuwa mpaka wakati huo walikuwa bado hawajaelewa kutoka Maandiko kwamba ilikuwa lazima Isa afufuke kutoka kwa wafu).

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

9 Kwa maana hawajalifahamu bado andiko, ya kwamba imempasa kufufuka.

Tazama sura Nakili




Yohana 20:9
22 Marejeleo ya Msalaba  

Maana hutaitupa kuzimu nafsi yangu, Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu.


Nguvu zangu zimekauka kama gae, Ulimi wangu waambatana na taya zangu; Unaniweka katika mavumbi ya mauti


Amemeza mauti hata milele; na Bwana MUNGU atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana BWANA amenena hayo.


Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa.


Nitawakomboa kwa nguvu za kaburi; nitawaokoa kutoka kwa mauti; ewe mauti, ya wapi mapigo yako? Ewe kaburi, ku wapi kuharibu kwako? Huruma itafichika machoni mwangu.


Yesu akajibu, akawaambia, Mnapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa Mungu.


Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake?


Lakini hawakulifahamu neno lile, likafichwa kwao wasilitambue; wakaogopa kumwuliza maana yake neno lile.


Basi alipofufuka katika wafu, wanafunzi wake wakakumbuka ya kuwa alisema hivi, wakaliamini lile andiko na lile neno alilolinena Yesu.


akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kwamba, Yesu huyu ninayewaambia ninyi habari zake ndiye Kristo.


ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao.


na ya kuwa alizikwa; na ya kuwa alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo Maandiko;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo