Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yohana 11:38 - Swahili Revised Union Version

38 Basi Yesu, akiwa na huzuni tena moyoni mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

38 Basi, Yesu akiwa amehuzunika tena moyoni, akafika kaburini. Kaburi lenyewe lilikuwa pango, na lilikuwa limefunikwa kwa jiwe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

38 Basi, Yesu akiwa amehuzunika tena moyoni, akafika kaburini. Kaburi lenyewe lilikuwa pango, na lilikuwa limefunikwa kwa jiwe.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

38 Basi, Yesu akiwa amehuzunika tena moyoni, akafika kaburini. Kaburi lenyewe lilikuwa pango, na lilikuwa limefunikwa kwa jiwe.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

38 Isa akafika penye kaburi akiwa amefadhaika sana kwa mara nyingine. Hilo kaburi lilikuwa pango ambalo jiwe liliwekwa kwenye ingilio lake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

38 Isa kwa mara nyingine akiwa amefadhaika sana, akafika penye kaburi. Hilo kaburi lilikuwa pango ambalo jiwe lilikuwa limewekwa kwenye ingilio lake.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

38 Basi Yesu, akiwa na huzuni tena moyoni mwake, akafika kwenye kaburi. Nalo lilikuwa ni pango, na jiwe limewekwa juu yake.

Tazama sura Nakili




Yohana 11:38
12 Marejeleo ya Msalaba  

Basi baada ya hayo Abrahamu akamzika Sara mkewe katika pango la shamba la Makpela kuelekea Mamre, ndiyo Hebroni, katika nchi ya Kanaani.


Unafanyaje hapa? Nawe una nani hapa? Hata ukachimba kaburi hapa; ukamchimbia kaburi huko juu, na kumchongea makao katika jabali!


Piga kite, basi, Ee mwanadamu; kwa kuvunjika moyo na uchungu mwingi mbele ya macho yao.


BWANA akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaopiga kite na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake.


akauweka katika kaburi lake jipya, alilokuwa amelichonga mwambani; akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango wa kaburi, akaenda zake.


Wakaenda, wakalilinda kaburi salama, kwa kulitia lile jiwe mhuri, pamoja na kuwaweka wale askari walinzi.


Naye akanunua sanda ya kitani, akamteremsha, akamfungia ile sanda, akamweka katika kaburi lililochongwa mwambani; akavingirisha jiwe mbele ya mlango wa kaburi.


Akapiga kite rohoni mwake, akasema, Mbona kizazi hiki chatafuta ishara? Amin, nawaambieni, Hakitapewa ishara kizazi hiki.


Wakalikuta lile jiwe limevingirishwa mbali na kaburi,


Basi Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana naye wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake,


Hata siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalene alikwenda kaburini alfajiri, kukiwa bado giza; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo