Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yobu 11:8 - Swahili Revised Union Version

8 Ni juu mno kama mbingu; waweza kufanya nini wewe? Ni wenye kina kuliko kuzimuni; waweza kujua nini wewe?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Ukuu wake wapita mbingu, wewe waweza nini? Kimo chake chapita Kuzimu, wewe waweza kujua nini?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Ukuu wake wapita mbingu, wewe waweza nini? Kimo chake chapita Kuzimu, wewe waweza kujua nini?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Ukuu wake wapita mbingu, wewe waweza nini? Kimo chake chapita Kuzimu, wewe waweza kujua nini?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Ni juu mno kuliko mbingu: unaweza kufanya nini? Kina chake ni kirefu kuliko Kuzimu: wewe unaweza kujua nini?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Ni juu mno kuliko mbingu: waweza kufanya nini? Kina chake ni kirefu kuliko kuzimu: wewe waweza kujua nini?

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 Ni juu mno kama mbingu; waweza kufanya nini wewe? Ni wenye kina kuliko kuzimuni; waweza kujua nini wewe?

Tazama sura Nakili




Yobu 11:8
17 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini Mungu je! Yamkini atakaa na watu duniani? Tazama, mbingu na mbingu za mbingu za mbingu hazikutoshi; seuze nyumba hii niliyoijenga!


Cheo chake ni kirefu kuliko dunia, Ni kipana zaidi ya bahari.


Je! Mungu hayuko mbinguni juu? Tena tazama umbali wa nyota, jinsi zilivyo juu!


Kaburi li wazi mbele yake, Uharibifu nao hauna kifuniko.


Ziangalie mbingu ukaone; Na mawingu yaangalie, yaliyo juu kuliko wewe.


Yeye Mwenyezi hamwezi kumwona; Yeye ni mkuu mwenye uweza; Tena mwenye hukumu, na mwingi wa haki, hataonea.


Je! Umefunuliwa malango ya mauti, Au umeyaona malango ya kuzimu?


Kama vile wingu likomavyo na kutoweka, Ndivyo alivyo huyo ashukaye kuzimuni, hatazuka tena kabisa.


Maana, kama mbingu zilivyoinuka juu ya nchi, Ndivyo fadhili zake zilivyo kuu kwa wamchao.


Na walisifu jina la BWANA, Maana jina lake peke yake limetukuka; Adhama yake i juu ya nchi na mbingu.


Haki yako ni kama milima ya Mungu, Hukumu zako ni vilindi vikuu, Ee BWANA, unawalinda wanadamu na wanyama.


Ni nani aliyepanda mbinguni na kushuka chini? Ni nani aliyekamata upepo kwa makonzi yake? Ni nani aliyeyafunga maji ndani ya nguo yake? Ni nani aliyefanya imara ncha zote za nchi? Jina lake ni nani? Na ni nani jina la mwanawe, kama wajua?


Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, ndivyo njia zangu zilivyo juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.


Wajapochimba waingie katika kuzimu, mkono wangu utawatoa huko; nao wajapopanda hata mbinguni, nitawateremsha toka huko.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo