Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 9:6 - Swahili Revised Union Version

6 Makao yako ya katikati ya hadaa; kwa hadaa wanakataa kunijua mimi, asema BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 Wanarundika dhuluma juu ya dhuluma, na udanganyifu juu ya udanganyifu. Wanakataa kunitambua mimi. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 Wanarundika dhuluma juu ya dhuluma, na udanganyifu juu ya udanganyifu. Wanakataa kunitambua mimi. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 Wanarundika dhuluma juu ya dhuluma, na udanganyifu juu ya udanganyifu. Wanakataa kunitambua mimi. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 Unakaa katikati ya udanganyifu; katika udanganyifu wao wanakataa kunitambua mimi,” asema Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 Unakaa katikati ya udanganyifu; katika udanganyifu wao wanakataa kunitambua mimi,” asema bwana.

Tazama sura Nakili




Yeremia 9:6
21 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa kuwa nimeita, nanyi mkakataa; Nimeunyosha mkono wangu, wala hakuna aliyeangalia;


Kwa kuwa walichukia maarifa, Wala hawakuchagua kumcha BWANA.


nami nitakuelekezea wewe mkono wangu, na kukutakasa takataka zako kabisa, na kukuondolea bati lako lote;


Ng'ombe amjua bwana wake, Na punda ajua kibanda cha bwana wake; Bali Israeli hajui, watu wangu hawafikiri.


hapo Bwana atakapokuwa ameuosha uchafu wa hao binti za Sayuni na kuisafisha damu ya Yerusalemu kati yake, kwa roho ya hukumu na kwa roho ya kuteketeza.


Wameyarudia maovu ya baba zao, waliokataa kusikia maneno yangu; wamewafuata miungu mingine na kuwatumikia; nyumba ya Israeli, na nyumba ya Yuda, wameyavunja maagano yangu niliyoyafanya na baba zao.


Lakini mimi nilikuwa kama mwana-kondoo mpole, achukuliwaye kwenda kuchinjwa; wala sikujua ya kuwa wamefanya mashauri kinyume changu, wakisema, Na tuuharibu mti pamoja na matunda yake, na tumkatilie mbali atoke katika nchi ya walio hai, ili jina lake lisikumbukwe tena.


Watu hawa waovu, wanaokataa kusikiliza maneno yangu, wanaokwenda kwa ushupavu wa mioyo yao, na kufuata miungu mingine ili kuitumikia na kuiabudu, watakuwa hali moja na kitambaa hiki kisichofaa kwa lolote.


Hapo ndipo waliposema, Njooni na tufanye mashauri juu ya Yeremia; maana sheria haitampotea kuhani, wala shauri halitampotea mwenye hekima, wala neno halitampotea nabii. Njooni, na tumpige kwa ndimi zetu, wala tusiyaangalie maneno yake yoyote.


Maana nimesikia shutuma za watu wengi; hofu ziko pande zote. Rafiki zangu wote, wanaonivizia nisite, husema, Mshitaki, nasi tutamshitaki, huenda akahadaika, nasi tutamshinda, tutajilipiza kisasi kwake.


Kama tundu lijaavyo ndege, kadhalika nyumba zao zimejaa hila; kwa hiyo wamekuwa wakuu, wamepata mali.


Mbona, basi, watu hawa wa Yerusalemu wamegeuka waende nyuma, wasikome kugeuka hivyo? Hushika udanganyifu sana, hukataa kurudi.


Niwezeje kukuacha, Efraimu? Niwezeje kukuachilia Israeli? Niwezeje kukufanya kama Adma? Niwezeje kukuweka kama Seboimu? Moyo wangu umegeuka ndani yangu, huruma zangu zimewaka pamoja.


Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwa kuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, mimi nami nitawasahau watoto wako.


Nami nitalileta fungu lile la tatu na kulipitisha kati ya moto, nami nitawasafisha kama fedha isafishwavyo, nami nitawajaribu kama dhahabu ijaribiwavyo; wataliitia jina langu, nami nitawasikia; mimi nitasema, Watu hawa ndio wangu; nao watasema, BWANA ndiye Mungu wangu.


Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.


Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe.


Basi, hao wana wa Eli walikuwa watu wasiofaa kitu; hawakumjali BWANA,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo