Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 6:7 - Swahili Revised Union Version

7 Kama vile kisima kitoavyo maji yake, ndivyo utoavyo uovu wake; jeuri na kuharibu kwasikiwa ndani yake; ugonjwa na jeraha zi mbele zangu daima.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Kama kisima kinavyohifadhi maji yake yakabaki safi, ndivyo Yerusalemu unavyohifadhi uovu wako. Ukatili na uharibifu vyasikika ndani yake, magonjwa na majeraha yake nayaona daima.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Kama kisima kinavyohifadhi maji yake yakabaki safi, ndivyo Yerusalemu unavyohifadhi uovu wako. Ukatili na uharibifu vyasikika ndani yake, magonjwa na majeraha yake nayaona daima.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Kama kisima kinavyohifadhi maji yake yakabaki safi, ndivyo Yerusalemu unavyohifadhi uovu wako. Ukatili na uharibifu vyasikika ndani yake, magonjwa na majeraha yake nayaona daima.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Kama vile kisima kinavyomwaga maji yake, ndivyo anavyomwaga uovu wake. Ukatili na maangamizi vyasikika ndani yake, ugonjwa wake na majeraha yake viko mbele yangu daima.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Kama vile kisima kinavyomwaga maji yake, ndivyo anavyomwaga uovu wake. Ukatili na maangamizi yasikika ndani yake, ugonjwa wake na majeraha yake viko mbele yangu daima.

Tazama sura Nakili




Yeremia 6:7
24 Marejeleo ya Msalaba  

Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.


Toka wayo wa mguu hadi kichwani hamna uzima ndani yake; bali jeraha na machubuko na vidonda vitokavyo usaha; havikufungwa, havikuzongwazongwa, wala havikulainishwa kwa mafuta.


Bali wabaya wanafanana na bahari iliyochafuka; maana haiwezi kutulia, na maji yake hutoa tope na takataka.


Nyavu zao hazitakuwa mavazi, wala hawatajifunika kwa kazi zao; kazi zao ni kazi za uovu, na vitendo vya udhalimu vimo mikononi mwao.


Maana kila ninenapo napiga kelele, nalia, Dhuluma na uharibifu! Kwa kuwa neno la BWANA limefanywa shutumu kwangu, na dhihaka, mchana kutwa.


Maana BWANA asema hivi, Maumivu yako hayaponyeki, na jeraha lako ni kubwa.


Hapana mtu wa kukutetea; kwa jeraha lako huna dawa ziponyazo.


Mbona unalilia maumivu yako? Maumivu yako hayaponyeki; kwa sababu ya ukubwa wa uovu wako, kwa sababu dhambi zako zimeongezeka, nimekutenda haya.


Kwa kuwa mji huu umekuwa sababu ya kunitia hasira, na sababu ya ghadhabu yangu, tangu siku ile walipoujenga hata siku hii ya leo; ili niuondoe usiwe mbele za uso wangu;


Je! Hakuna marhamu katika Gileadi? Huko hakuna tabibu? Mbona, basi, haijarejea afya ya binti ya watu wangu?


wakati wanapokupa maono ya udanganyifu, wakati wanapokuagulia uongo, wanakuweka juu ya shingo zao wachukizao, na waovu, ambao siku yao imekuja, katika wakati wa adhabu ya mwisho.


Maana damu yake imo ndani yake; aliiweka juu ya jabali lililo wazi; hakuimwaga juu ya nchi, apate kuifunika kwa mavumbi;


Bwana MUNGU asema hivi; Na iwatoshe ninyi, enyi wakuu wa Israeli; ondoeni dhuluma na unyang'anyi; fanyeni hukumu na haki; acheni kutoza kwenu kwa nguvu katika watu wangu, asema Bwana MUNGU.


Udhalimu umeinuka, ukawa fimbo ya uovu; hapana mtu atakayesalia miongoni mwao, wala katika jamii yao, wala kitu katika utajiri wao; wala hakutakuwa kutukuka kati yao.


Ufue mnyororo; kwa maana nchi hii imejaa hukumu za damu, nao mji umejaa udhalimu.


Ole wake yeye aliyeasi na kutiwa unajisi, mji wa udhalimu!


Tufuate:

Matangazo


Matangazo