Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 48:12 - Swahili Revised Union Version

12 Basi, tazama, siku zinakuja, asema BWANA, ambazo nitatuma kwake wamiminao, nao watammimina, nao watamwaga vyote vilivyomo vyomboni mwake, na kuzivunja chupa zake vipande vipande.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 “Kwa hiyo, wakati waja, nasema mimi Mwenyezi-Mungu ambapo nitampelekea wamiminaji ambao wataimimina divai yake. Wataimwaga yote kutoka vyombo vyake na kuvivunja vipandevipande.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 “Kwa hiyo, wakati waja, nasema mimi Mwenyezi-Mungu ambapo nitampelekea wamiminaji ambao wataimimina divai yake. Wataimwaga yote kutoka vyombo vyake na kuvivunja vipandevipande.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 “Kwa hiyo, wakati waja, nasema mimi Mwenyezi-Mungu ambapo nitampelekea wamiminaji ambao wataimimina divai yake. Wataimwaga yote kutoka vyombo vyake na kuvivunja vipandevipande.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Lakini siku zinakuja,” asema Mwenyezi Mungu, “nitakapotuma watu wamiminao kutoka magudulia, nao watamimina; wataacha magudulia yake yakiwa matupu na kuvunja mitungi yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Lakini siku zinakuja,” asema bwana, “nitakapotuma watu wamiminao kutoka kwenye magudulia, nao watamimina; wataacha magudulia yake yakiwa matupu na kuvunja mitungi yake.

Tazama sura Nakili




Yeremia 48:12
14 Marejeleo ya Msalaba  

Utawaponda kwa fimbo ya chuma, Na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi.


Na binti za Moabu watakuwa kama ndege warukao huku na huko, kama kiota cha ndege waliotiwa hofu, kwenye vivuko vya Arnoni.


Naye atapavunja kama chombo cha mfinyanzi kivunjwavyo, kinavyovunjwavunjwa kikatili, hata hakipatikani katika vipande vyake kigae kitoshacho kutwaa moto jikoni, au kuteka maji kisimani.


Na wakuu wao huwatuma watoto wao kwenye maji; Nao hufika visimani wasipate maji; Hurudi, na vyombo vyao ni vitupu; Wametahayarika na kufadhaika, Na kuvifunika vichwa vyao.


Ndipo hapo utalivunja gudulia lile, mbele ya macho ya watu wale waendao pamoja nawe,


Ombolezeni, enyi wachungaji, na kulia; na kugaagaa katika majivu, enyi mlio hodari katika kundi; maana siku za kuuawa kwenu zimetimia kabisa, nami nitawavunja vipande vipande, nanyi mtaanguka kama chombo cha anasa.


angalieni, nitatuma watu na kuzitwaa jamaa zote za upande wa kaskazini, asema BWANA, nami nitatuma ujumbe kwa Nebukadneza, mfalme wa Babeli, mtumishi wangu, nami nitawaleta juu ya nchi hii, na juu yao wakaao ndani yake, na juu ya mataifa haya yote yaliyoko pande zote; nami nitawaangamiza kabisa, na kuwafanya kitu cha kushangaza, na kitu cha kuzomewa, na ukiwa wa daima.


Moabu amestarehe tangu ujana wake, naye ametulia juu ya sira zake, wala hakumiminwa kutoka chombo kimoja kutiwa chombo kingine, wala hakwenda kufungwa; kwa hiyo ladha yake anakaa nayo, wala harufu yake haikubadilika.


Na Moabu ataona haya kwa ajili ya Kemoshi, kama nyumba ya Israeli ilivyoona haya kwa ajili ya Betheli, tegemeo lao.


Moabu ameharibika, na moshi wa miji yake umepanda; na vijana wake wateule wameteremka kwenda kuchinjwa, asema Mfalme, ambaye jina lake ni BWANA wa majeshi.


Juu ya madari yote ya nyumba za Moabu, na katika njia kuu zake, pana maombolezo, kila mahali; kwa maana nimevunja Moabu kama chombo kisichopendeza, asema BWANA.


Naye mwenye kuteka nyara atakuja juu ya kila mji, wala hakuna mji utakaookoka; bonde nalo litaangamia, nayo nchi tambarare itaharibiwa; kama BWANA alivyosema.


Kwa maana BWANA anairudisha fahari ya Yakobo, kama fahari ya Israeli; maana watekao nyara wamewateka, na kuyaharibu matawi ya mizabibu yao.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo