Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 4:9 - Swahili Revised Union Version

9 Na katika siku hiyo itakuwa, asema BWANA, moyo wa mfalme utapotea, na moyo wa wakuu wake; na makuhani watastaajabu, na manabii watashangaa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Siku hiyo, mfalme na wakuu watakufa moyo; makuhani watapigwa na bumbuazi, na manabii watashangaa.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Siku hiyo, mfalme na wakuu watakufa moyo; makuhani watapigwa na bumbuazi, na manabii watashangaa.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Siku hiyo, mfalme na wakuu watakufa moyo; makuhani watapigwa na bumbuazi, na manabii watashangaa.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 “Katika siku ile,” asema Mwenyezi Mungu “mfalme na maafisa watakata tamaa, makuhani watafadhaika, na manabii watashangazwa mno.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 “Katika siku ile,” asema bwana “mfalme na maafisa watakata tamaa, makuhani watafadhaika, na manabii watashangazwa mno.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

9 Na katika siku hiyo itakuwa, asema BWANA, moyo wa mfalme utapotea, na moyo wa wakuu wake; na makuhani watastaajabu, na manabii watashangaa.

Tazama sura Nakili




Yeremia 4:9
20 Marejeleo ya Msalaba  

Ndipo mahali pakabomolewa katika ukuta wa mji, watu wote wa vita wakakimbia usiku kwa njia ya lango lililokuwa kati ya zile kuta mbili, karibu na bustani ya mfalme; (basi wale Wakaldayo walikuwa wakiuzuia mji pande zote;) mfalme akaenda kwa njia ya Araba.


Moyo wangu umepigwa kama majani na kukauka, Naam, ninasahau kula chakula changu.


Katika siku hiyo Misri itakuwa kama wanawake; itatetemeka na kuogopa kwa sababu ya kutikiswa kwa mkono wa BWANA wa majeshi, autikisao juu yake.


Na roho yao Misri itaondolewa, nami nitaiharibu mipango yao, nao watakwenda kwa sanamu zao, na kwa waganga, na kwa wapiga ramli na kwa wachawi.


Kila wakati litakapopita litawachukueni. Maana litapita asubuhi baada ya asubuhi, wakati wa mchana na wakati wa usiku; na kuifahamu habari ile kutakuwa kitisho tu.


Kama mwizi aonavyo haya akamatwapo, ndivyo waonavyo haya nyumba ya Israeli; wao, na wafalme wao, na wakuu wao, na makuhani wao, na manabii wao;


Ombolezeni, enyi wachungaji, na kulia; na kugaagaa katika majivu, enyi mlio hodari katika kundi; maana siku za kuuawa kwenu zimetimia kabisa, nami nitawavunja vipande vipande, nanyi mtaanguka kama chombo cha anasa.


Wako wapi sasa manabii wenu waliowatabiria, wakisema, Mfalme wa Babeli hatakuja juu yenu, wala juu ya nchi hii?


Miji imetwaliwa, ngome zimeshambuliwa, na mioyo ya mashujaa wa Moabu siku hiyo itakuwa kama moyo wa mwanamke akiwa katika uchungu wa kujifungua.


Manabii wanatabiri uongo, na makuhani wanatawala kwa msaada wa hao; na watu wangu wanapenda mambo yawe hivyo. Nanyi mtafanya nini mwisho wake?


Ukuta wa mji ukabomolewa, watu wote wa vita wakakimbia, wakatoka mjini usiku, kwa njia ya lango lililokuwa kati ya zile kuta mbili, karibu na bustani ya mfalme; (basi wale Wakaldayo walikuwa wameuzunguka mji pande zote;) wakaenda zao kwa njia ya Araba.


Tazameni, enyi mnaodharau, kastaajabuni, mkatoweke; kwa kuwa natenda kazi mimi siku zenu, kazi ambayo msingeisadiki kabisa, ijapo mtu akiwasimulia sana.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo