Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 4:2 - Swahili Revised Union Version

2 nawe utaapa hivi, Kama BWANA aishivyo, katika kweli, na katika hukumu, na katika haki ndipo mataifa watabarikiwa na yeye, nao watajitukuza katika yeye.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 ukiapa kwa ukweli, unyofu na uadilifu, kwa kusema, ‘Kama Mwenyezi-Mungu aishivyo’, ndipo mataifa yatakapopata baraka kwangu, na kutukuka kwa sababu yangu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 ukiapa kwa ukweli, unyofu na uadilifu, kwa kusema, ‘Kama Mwenyezi-Mungu aishivyo’, ndipo mataifa yatakapopata baraka kwangu, na kutukuka kwa sababu yangu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 ukiapa kwa ukweli, unyofu na uadilifu, kwa kusema, ‘Kama Mwenyezi-Mungu aishivyo’, ndipo mataifa yatakapopata baraka kwangu, na kutukuka kwa sababu yangu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 ikiwa utaapa katika kweli, kwa haki na kwa unyofu, ‘Hakika kama Mwenyezi Mungu aishivyo,’ ndipo mataifa yatakapobarikiwa naye, na ndani yake watajitukuza.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 ikiwa kwa kweli, kwa haki na kwa unyofu utaapa, ‘Kwa hakika kama vile bwana aishivyo,’ ndipo mataifa yatakapobarikiwa naye na katika yeye watajitukuza.”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

2 nawe utaapa hivi, Kama BWANA aishivyo, katika kweli, na katika hukumu, na katika haki ndipo mataifa watabarikiwa na yeye, nao watajitukuza katika yeye.

Tazama sura Nakili




Yeremia 4:2
30 Marejeleo ya Msalaba  

na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.


Sulemani akasema, Umemfanyia mtumwa wako Daudi baba yangu fadhili kuu, kadiri alivyoenenda mbele zako katika kweli, na katika haki, na katika unyofu wa moyo pamoja nawe; nawe umemwekea na fadhili hii kubwa, maana umempa mwana wa kuketi kitini pake kama ilivyo leo.


Jina lake na lidumu milele, Pindi ling'aapo jua, umaarufu wake uwepo; Mataifa yote na wabarikiwe katika yeye, Na kumwita heri.


Mfalme mkuu upendaye hukumu kwa haki; Umeiimarisha haki; Umefanya hukumu na haki katika Israeli.


Kwa nafsi yangu nimeapa, neno hili limetoka kinywani mwangu katika haki, wala halitarudi, ya kwamba mbele zangu kila goti litapigwa, kila ulimi utaapa.


Katika BWANA wazao wote wa Israeli watapewa haki, na kutukuka.


Hata itakuwa yeye atakayejibariki duniani, atajibariki kwa Mungu wa kweli; naye atakayeapa duniani, ataapa kwa Mungu wa kweli. Kwa kuwa taabu za kwanza zimesahauliwa, na kwa kuwa zimefichwa machoni pangu.


Bali BWANA ndiye Mungu wa kweli; Ndiye Mungu aliye hai, Mfalme wa milele; Mbele za ghadhabu yake nchi yatetemeka, Wala mataifa hawawezi kustahimili hasira yake.


Tena itakuwa, baada ya kuwang'oa, nitarudi na kuwahurumia; nami nitawaleta tena, kila mtu aingie katika urithi wake, na kila mtu aingie katika nchi yake.


Kisha itakuwa, ikiwa watajifunza kwa bidii njia za watu wangu, kuapa kwa jina langu, Kama BWANA aishivyo, vile vile kama walivyowafundisha watu wangu kuapa kwa Baali, ndipo watakapojengwa kati ya watu wangu.


Ee BWANA, nguvu zangu, ngome yangu, na kimbilio langu siku ya taabu, kwako wewe watakuja mataifa yote toka ncha za dunia, wakisema, Baba zenu hawakurithi kitu ila uongo, naam, ubatili na vitu visivyofaa.


Wakati ule watauita Yerusalemu kiti cha enzi cha BWANA; na mataifa yote yatakusanyika huko Yerusalemu, kwa ajili ya jina la BWANA; wala hawatakwenda tena kwa ukaidi wa moyo wao mbaya.


Na mji huu utakuwa kwangu jina la furaha, na sifa na utukufu, mbele ya mataifa yote ya dunia, watakaosikia habari ya mema yote niwatendeayo, nao wataogopa na kutetemeka, kwa sababu ya mema yote na amani nitakaoupatia mji huo.


Na wajaposema, Kama BWANA aishivyo, hakika waapa kwa uongo.


Maana kama mkitengeneza kabisa njia zenu na matendo yenu; kama mkihukumu hukumu ya haki kati ya mtu na jirani yake;


bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni BWANA, nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo hayo, asema BWANA,


Nami nitakuposa uwe wangu wa milele; naam, nitakuposa kwa haki, na kwa hukumu, na kwa ufadhili, na kwa rehema.


Lakini hata sasa, asema BWANA, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuomboleza;


nami nitawaleta, nao watakaa katikati ya Yerusalemu; nao watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao, katika kweli na katika haki.


Kwa maana tokea maawio ya jua hata machweo yake jina langu ni kuu katika mataifa; na katika kila mahali unatolewa uvumba na dhabihu safi kwa jina langu; maana jina langu ni kuu katika mataifa, asema BWANA wa majeshi.


kusudi, kama ilivyoandikwa, Yeye aonaye fahari na aone fahari juu ya Bwana.


Lakini, Yeye ajisifuye, na ajisifu katika Bwana.


Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiria Abrahamu Habari Njema zamani, kusema, Katika wewe Mataifa yote watabarikiwa.


Mche BWANA, Mungu wako, umtumikie yeye; ambatana naye, na kuapa kwa jina lake.


Na wakati uwapo katika mashaka, ukiisha kupatwa na mambo haya yote, siku za mwisho, utamrudia BWANA, Mungu wako, na kuisikiza sauti yake;


Mche BWANA, Mungu wako; ndiye utakayemtumikia, na kuapa kwa jina lake.


Maana sisi tu tohara, tumwabuduo Mungu kwa Roho, na kuona fahari juu ya Kristo Yesu, wala hatuutumainii mwili.


Wewe ungoje usiku huu; kisha, asubuhi, kama akikubali kukufanyia impasavyo jamaa, haya, na akufanyie; lakini ikiwa hataki yeye, basi mimi nitakufanyia impasavyo jamaa; BWANA aishivyo. Ulale wewe hadi asubuhi.


Daudi akaapa, akasema, Baba yako anajua sana ya kuwa nimeona kibali machoni pako, naye asema, Yonathani asilijue neno hili, asije akahuzunika; lakini ni kweli, aishivyo BWANA, na iishivyo roho yako, iko hatua moja tu kati ya mimi na mauti.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo