Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 3:2 - Swahili Revised Union Version

2 Inua macho yako, ukavitazame vilele vya milima, ukaone; pako wapi mahali ambapo hawakulala nawe? Kando ya njia umeketi ili kuwangojea, kama vile Mwarabu jangwani; nawe umeitia nchi unajisi kwa ukahaba wako na uovu wako.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Inua macho uvitazame vilele vya vilima! Pako wapi mahali ambapo hawajalala nawe? Uliwangoja wapenzi wako kando ya njia, kama bedui aviziavyo watu jangwani. Umeifanya nchi kuwa najisi, kwa ukahaba wako mbaya kupindukia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Inua macho uvitazame vilele vya vilima! Pako wapi mahali ambapo hawajalala nawe? Uliwangoja wapenzi wako kando ya njia, kama bedui aviziavyo watu jangwani. Umeifanya nchi kuwa najisi, kwa ukahaba wako mbaya kupindukia.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Inua macho uvitazame vilele vya vilima! Pako wapi mahali ambapo hawajalala nawe? Uliwangoja wapenzi wako kando ya njia, kama bedui aviziavyo watu jangwani. Umeifanya nchi kuwa najisi, kwa ukahaba wako mbaya kupindukia.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 “Inua macho utazame miinuko iliyo kame na uone. Je, pana mahali ambapo hawajalala nawe? Uliketi kando ya barabara ukiwasubiri wapenzi, ukakaa kama mtu anayehamahama jangwani. Umeinajisi nchi kwa ukahaba wako na uovu wako.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 “Inua macho utazame miinuko iliyo kame na uone. Je, pana mahali ambapo hawajalala nawe? Uliketi kando ya barabara ukiwasubiri wapenzi, ukakaa kama yeye ahamahamaye jangwani. Umeinajisi nchi kwa ukahaba wako na uovu wako.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

2 Inua macho yako, ukavitazame vilele vya milima, ukaone; pako wapi mahali ambapo hawakulala nawe? Kando ya njia umeketi ili kuwangojea, kama vile Mwarabu jangwani; nawe umeitia nchi unajisi kwa ukahaba wako na uovu wako.

Tazama sura Nakili




Yeremia 3:2
22 Marejeleo ya Msalaba  

Basi akavua nguo za ujane wake, akajivika utaji, akajifunika uso, akakaa mlangoni pa Enaimu, karibu na njia ya kuendea Timna. Maana aliona ya kwamba Shela amekuwa mtu mzima, ijapokuwa hakuozwa awe mkewe.


Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wake zake wakamgeuza moyo.


Na mahali pa juu palipokuwapo mbele ya Yerusalemu, palipokuwa upande wa kulia wa mlima wa uharibifu, alipopajenga Sulemani, mfalme wa Israeli, kwa Ashtorethi, chukizo la Wasidoni, na Kemoshi, chukizo la Moabu, na Milkomu, chukizo la wana wa Amoni, mfalme akapanajisi.


Wakamwaga damu isiyo na hatia, Damu ya wana wao na binti zao, Waliowatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani; Nchi ikatiwa unajisi kwa damu.


Naam, huotea kama mnyang'anyi; Huwaongeza wenye hila katika wanadamu.


Ana kelele, na ukaidi; Miguu yake haikai nyumbani mwake.


Watekao nyara wamepanda juu ya vilele vya milima katika nyika; kwa maana upanga wa BWANA utaangamiza toka upande mmoja wa nchi hata upande wa pili wa nchi; hapana mwenye mwili atakayekuwa na amani.


Kwa maana tangu zamani wewe umeivunja nira yako, na kuvipasua vifungo vyako; ukasema, Mimi sitatumika; kwa maana juu ya kila kilima kirefu, na chini ya kila mti wenye majani mabichi, umejiinamisha, ukafanya mambo ya ukahaba.


Wawezaje kusema, Sikutiwa unajisi, sikuwafuata Mabaali? Itazame njia yako bondeni, ujue uliyoyatenda; wewe u ngamia mwepesi, apitaye katika njia zake;


Nami nikawatia katika nchi ya shibe, mpate kula matunda yake na mema yake; lakini ninyi mlipoingia katika nchi ile, mliitia unajisi nchi yangu, na urithi wangu mliufanya kuwa chukizo.


Watu husema, Mtu akimwacha mkewe, naye akienda zake, akawa mke wa mtu mwingine, je! Mtu huyo atamrudia tena? Je! Nchi hiyo haitatiwa unajisi? Lakini wewe umefanya mambo ya ukahaba na wapenzi wengi; nawe, je! Utanirudia mimi? Asema BWANA.


Ungama uovu wako tu; ya kwamba umemwasi BWANA, Mungu wako, na njia zako zimekuwa nyingi kuwaendea wageni chini ya kila mti wenye majani mabichi, wala hamkuitii sauti yangu, asema BWANA.


Sauti inasikiwa juu ya vilele vya milima, ni kulia kwao na maombi yao wana wa Israeli; kwa kuwa wameipotosha njia yao, wamemsahau BWANA, Mungu wao.


Hata ikawa, kwa sababu alikuwa mwepesi wa kufanya ukahaba, nchi ikatiwa unajisi, naye akazini na mawe na miti.


Zikate nywele zako, Ee Yerusalemu, uzitupe, Ukafanye maombolezo juu ya vilele vya milima; Kwa maana BWANA amekikataa na kukitupa Kizazi cha ghadhabu yake.


Ukatwaa baadhi ya mavazi yako, ukajifanyia mahali palipoinuka, palipopambwa kwa rangi mbalimbali, ukafanya mambo ya kikahaba juu yake; mambo kama hayo hayatakuja wala hayatakuwako.


Kwa maana nilipokuwa nimekwisha kuwaingiza katika nchi ile, ambayo niliuinua mkono wangu kuwapa, wakati huo walipoona kila mlima mrefu, na kila mti wenye majani mengi, walitoa matoleo yao huko, na huko walitoa chukizo la sadaka zao, na huko walifukiza manukato ya kupendeza, na huko walimimina sadaka zao za kunywewa.


Maana mama yao amezini; yeye aliyewachukua mimba ametenda mambo ya aibu; maana alisema, Nitafuatana na wapenzi wangu, wanipao chakula changu na maji yangu, sufu yangu na kitani yangu, mafuta yangu na vileo vyangu.


Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Abrahamu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake.


Vunjeni kabisa mahali pote walipokuwa wakiitumikia miungu yao mataifa mtakayoyamiliki, juu ya milima mirefu, na juu ya vilima, na chini ya kila mti wenye majani mabichi;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo