Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Yeremia 12:12 - Swahili Revised Union Version

12 Watekao nyara wamepanda juu ya vilele vya milima katika nyika; kwa maana upanga wa BWANA utaangamiza toka upande mmoja wa nchi hata upande wa pili wa nchi; hapana mwenye mwili atakayekuwa na amani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

12 Juu ya milima yote jangwani, watu wamefika kuangamiza. Upanga wangu unapita kuiangamiza nchi, toka upande mmoja hadi mwingine, wala hakuna mtu atakayeishi kwa amani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

12 Juu ya milima yote jangwani, watu wamefika kuangamiza. Upanga wangu unapita kuiangamiza nchi, toka upande mmoja hadi mwingine, wala hakuna mtu atakayeishi kwa amani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

12 Juu ya milima yote jangwani, watu wamefika kuangamiza. Upanga wangu unapita kuiangamiza nchi, toka upande mmoja hadi mwingine, wala hakuna mtu atakayeishi kwa amani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

12 Juu ya miinuko yote ilivyo kama jangwani waangamizi watavamia, kwa maana upanga wa Mwenyezi Mungu utawala, kuanzia ncha moja ya nchi hadi nyingine; hakuna hata mmoja atakayekuwa salama.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

12 Juu ya miinuko yote ilivyo kama jangwani mharabu atajaa, kwa maana upanga wa bwana utawala, kuanzia ncha moja ya nchi hadi nyingine; hakuna hata mmoja atakayekuwa salama.

Tazama sura Nakili




Yeremia 12:12
31 Marejeleo ya Msalaba  

Upanga wa BWANA umeshiba damu, umejazwa mafuta, kwa damu ya wana-kondoo na mbuzi, kwa mafuta ya figo za kondoo dume; maana BWANA ana dhabihu huko Bozra, machinjo makubwa katika nchi ya Edomu.


Hapana amani kwa waovu; asema Mungu wangu.


Kisha itakuwa, hapo watakapokuambia, Tutoke, tuende wapi? Utawaambia, BWANA asema hivi, Walioandikiwa kufa, watakwenda kufa; au kufa kwa upanga, watakufa kwa upanga; au kufa kwa njaa, watakufa kwa njaa, au kutekwa nyara, watakuwa mateka.


Maana BWANA asema hivi, Usiingie ndani ya nyumba yenye matanga, wala usiende kuwaombolezea, wala kuwalilia; maana nimewaondolea watu hawa amani yangu, asema BWANA, hata fadhili zangu na rehema zangu.


Na nchi hii yote pia itakuwa ukiwa, na kitu cha kushangaza; nayo mataifa haya yatamtumikia mfalme wa Babeli miaka sabini.


Inua macho yako, ukavitazame vilele vya milima, ukaone; pako wapi mahali ambapo hawakulala nawe? Kando ya njia umeketi ili kuwangojea, kama vile Mwarabu jangwani; nawe umeitia nchi unajisi kwa ukahaba wako na uovu wako.


Sauti inasikiwa juu ya vilele vya milima, ni kulia kwao na maombi yao wana wa Israeli; kwa kuwa wameipotosha njia yao, wamemsahau BWANA, Mungu wao.


Maana BWANA asema hivi, Tumesikia sauti ya tetemeko, na ya hofu, wala si ya amani.


Basi BWANA asema hivi, Hamkunisikiliza kumtangazia uhuru kila mtu ndugu yake, na kila mtu jirani yake; tazama, mimi nawatangazieni uhuru, asema BWANA, yaani, wa upanga, na njaa, na tauni; nami nitawatoa ninyi mtupwe huku na huko katika falme zote za dunia.


Maana BWANA asema hivi, Nchi yote itakuwa ukiwa; lakini sitaikomesha kabisa.


Maana hiyo ni siku ya Bwana, BWANA wa majeshi, Siku ya kisasi, ili ajilipize kisasi juu ya adui zake; Nao upanga utakula na kushiba, Utakunywa damu yao hata kukinai; Maana Bwana, BWANA wa majeshi, ana sadaka yake Katika nchi ya kaskazini karibu na mto Frati.


Ee upanga wa BWANA, Siku ngapi zitapita kabla hujatulia? Ujitie katika ala yako; Pumzika, utulie.


Sifa za Moabu haziko tena; katika Heshboni wameazimia mabaya juu yake, Haya! Njooni, na tumkatilie mbali asiwe taifa. Wewe nawe, Ee Madmena, utanyamazishwa; upanga utakufuatia.


Tulitazamia amani, lakini hayakuja mema yoyote; tulitazamia wakati wa kupona, na tazama, kufadhaika tu!


Umeniweka nafsi yangu mbali na amani; Nikasahau kufanikiwa.


Au nikileta upanga juu ya nchi ile, na kusema, Upanga, pita kati ya nchi hii, hata nikawakatilia mbali na nchi hiyo wanadamu na wanyama;


Nawe, mwanadamu, tabiri useme, Bwana MUNGU asema hivi, kuhusu wana wa Amoni, na kuhusu aibu yao; Nena, Upanga; upanga umefutwa; umeng'arishwa, ili kuua, ili kuufanya uue sana, upate kuwa kama umeme;


Basi, kwa kuwa nitamkatilia mbali nawe mtu mwenye haki na mtu mwovu, upanga wangu utatoka alani mwake, uwe juu ya watu wote wenye mwili toka kusini hadi kaskazini,


Neno la BWANA likanijia, kusema,


Mwanadamu, tabiri, useme, BWANA asema hivi; Nena, Upanga, upanga, umenolewa na kusuguliwa,


Theluthi ya hizo utaiteketeza katikati ya mji, siku za kuzingirwa zitakapomalizika; nawe utatwaa theluthi, na kuipiga kwa upanga pande zote; nawe utatawanya theluthi ichukuliwe na upepo, nami nitafuta upanga nyuma yake.


Nanyi nitawatapanyatapanya katika mataifa, nami nitaufuta upanga nyuma yenu; na nchi yenu itakuwa ni ukiwa, na miji yenu maganjo.


Nao wajapokwenda kuwa mateka mbele ya adui zao, nitauagiza upanga huko, nao utawaua; nami nitawaelekezea macho yangu niwatende mabaya, wala si mema.


Na ninyi Wakushi pia, mtauawa kwa upanga wangu.


Nitailevya mishale yangu kwa damu, Na upanga wangu utakula nyama; Pamoja na damu ya waliouawa na waliotekwa nyara, Katika vichwa vya wakuu wa adui.


Akatoka farasi mwingine, mwekundu sana, na yeye aliyempanda aliruhusiwa kuiondoa amani katika nchi, ili watu wauane, naye akapewa upanga mkubwa.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo