Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 8:7 - Swahili Revised Union Version

7 Kisha akamvika Haruni ile kanzu, na kumfunga mshipi, na kumvika joho, na kumvika naivera, na kumfunga huo mshipi wa kazi ya stadi wa naivera na kumfunga naivera kwa huo mshipi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Kisha akamvika Aroni joho na kuifunga kwa mkanda, akamvika kanzu, akamvalisha kizibao na kukifunga kiunoni mwake kwa mkanda uliofumwa kwa ustadi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Kisha akamvika Aroni joho na kuifunga kwa mkanda, akamvika kanzu, akamvalisha kizibao na kukifunga kiunoni mwake kwa mkanda uliofumwa kwa ustadi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Kisha akamvika Aroni joho na kuifunga kwa mkanda, akamvika kanzu, akamvalisha kizibao na kukifunga kiunoni mwake kwa mkanda uliofumwa kwa ustadi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Akamvika Haruni koti, akamfunga mshipi, akamvika joho, na kumvalisha kizibau. Pia akamfunga hicho kizibau kiunoni mwake kwa mshipi uliofumwa kwa ustadi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Akamvika Haruni koti, akamfunga mshipi, akamvika joho na kumvalisha kisibau. Pia akafunga kisibau juu yake na kukifunga kiunoni mwake kwa mshipi wake uliosokotwa kwa ustadi.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

7 Kisha akamvika Haruni ile kanzu, na kumfunga mshipi, na kumvika joho, na kumvika naivera, na kumfunga huo mshipi wa kazi ya stadi wa naivera na kumfunga naivera kwa huo mshipi.

Tazama sura Nakili




Walawi 8:7
12 Marejeleo ya Msalaba  

Nawe utamfanyia Haruni ndugu yako mavazi matakatifu, kwa utukufu na kwa uzuri.


Na mavazi watakayoyafanya ni haya; kifuko cha kifuani, na naivera, na joho, na kanzu ya kazi ya urembo; na kilemba, na mshipi; nao watawafanyia Haruni nduguyo, na wanawe, mavazi matakatifu ili anitumikie katika kazi ya ukuhani.


Nao waifanye naivera kwa nyuzi za dhahabu, buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa kwa ustadi.


Kisha twaa hayo mavazi na kumvika Haruni; itie kanzu, na joho la naivera, na naivera, na kifuko cha kifuani, na kumkaza kwa huo mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi;


Nitafurahi sana katika BWANA, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu.


kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji la maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na BWANA, ili atukuzwe.


Makuhani watakapoingia ndani, hawatatoka mahali patakatifu kwenda hadi katika ua wa nje; lakini wataweka mavazi yao katika mahali wahudumiapo; maana ni matakatifu; nao watavaa mavazi mengine, na kupakaribia mahali pa wazi kwa watu.


Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake.


ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti;


Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo.


Je! Sikumchagua yeye katika kabila zote za Israeli, ili awe kuhani wangu, apande madhabahuni kwangu; na kufukiza uvumba, na kuvaa naivera mbele zangu? Nami sikuwapa watu wa koo za baba yako dhabihu zote za wana wa Israeli zilizotolewa kwa moto?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo