Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 7:26 - Swahili Revised Union Version

26 Tena msiile damu yoyote, ama ya ndege, ama ya mnyama, katika nyumba zenu zote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 Tena, kamwe msile damu yoyote ile, iwe ya ndege au ya mnyama mahali popote mnapoishi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 Tena, kamwe msile damu yoyote ile, iwe ya ndege au ya mnyama mahali popote mnapoishi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 Tena, kamwe msile damu yoyote ile, iwe ya ndege au ya mnyama mahali popote mnapoishi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Popote mtakapoishi, kamwe msile damu ya ndege yeyote wala ya mnyama.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Popote mtakapoishi, kamwe msinywe damu ya ndege yeyote wala ya mnyama.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

26 Tena msiile damu yoyote, ama ya ndege, ama ya mnyama, katika nyumba zenu zote.

Tazama sura Nakili




Walawi 7:26
17 Marejeleo ya Msalaba  

Bali nyama pamoja na uhai, yaani, damu yake, msile.


Nawe utafanya vivyo hivyo katika ng'ombe wako, na kondoo wako; utamwacha siku saba pamoja na mama yake; siku ya nane utanipa mimi.


Basi, waambie, Bwana MUNGU asema hivi; Mnakula nyama pamoja na damu yake, na kuviinulia vinyago vyenu macho yenu, na kumwaga damu; je, mtaimiliki nchi hii?


Msile kitu chochote pamoja na damu yake; wala msifanye kuloga, wala kutumia utambuzi.


Neno hili litakuwa amri ya daima, katika vizazi vyenu vyote, ndani ya nyumba zenu zote, ya kwamba hamtakula mafuta wala damu kabisa.


Kwani huyo mtu atakayekula mafuta ya mnyama, ambaye ni katika wanyama ambao watu husongeza sadaka kwa BWANA kwa moto, mtu huyo atakayekula mafuta hayo atakatiliwa mbali na watu wake.


Mtu yeyote alaye damu, mtu huyo atatupiliwa mbali na watu wake.


Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu.


bali tuwaandikie kwamba wajiepushe na unajisi wa sanamu, na uasherati, na nyama zilizosongolewa, na damu.


yaani, mjiepushe na vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu, na damu, na nyama zilizosongolewa, na uasherati. Mkijizuia na hayo, mtafanya vema. Wasalamu.


Katika yeye huyo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, msamaha wa dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake.


Lakini msiile damu; imwageni juu ya nchi kama maji.


Ila ujihadhari kwamba usile damu, kwani ile damu ndiyo uhai; na uhai usile pamoja na nyama.


Pamoja na haya usile damu yake; uimwage nchi kama maji.


Kwa maana kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kukataliwa, kama kikipokewa kwa shukrani;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo