Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 5:6 - Swahili Revised Union Version

6 naye atamletea BWANA sadaka yake ya hatia kwa ajili ya hiyo dhambi yake aliyoifanya, mwana-kondoo wa kike, au mbuzi mke, kutoka katika kundi lake, kuwa ni sadaka ya dhambi; kisha kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya hiyo dhambi yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

6 na kumletea Mwenyezi-Mungu sadaka yake ya kuondoa hatia. Kwa ajili ya dhambi aliyotenda ataleta kondoo jike au mbuzi jike kutoka kundi lake amtoe sadaka kwa ajili ya kuondoa dhambi. Naye kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

6 na kumletea Mwenyezi-Mungu sadaka yake ya kuondoa hatia. Kwa ajili ya dhambi aliyotenda ataleta kondoo jike au mbuzi jike kutoka kundi lake amtoe sadaka kwa ajili ya kuondoa dhambi. Naye kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

6 na kumletea Mwenyezi-Mungu sadaka yake ya kuondoa hatia. Kwa ajili ya dhambi aliyotenda ataleta kondoo jike au mbuzi jike kutoka kundi lake amtoe sadaka kwa ajili ya kuondoa dhambi. Naye kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya dhambi yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

6 na kama adhabu ya dhambi aliyoitenda, ni lazima alete kwa Mwenyezi Mungu kondoo jike au mbuzi jike kutoka kundi lake kuwa sadaka ya dhambi; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

6 na kama adhabu ya dhambi aliyoitenda, lazima alete kwa bwana kondoo jike au mbuzi jike kutoka kwenye kundi lake kama sadaka ya dhambi; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake kwa dhambi yake.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

6 naye atamletea BWANA sadaka yake ya hatia kwa ajili ya hiyo dhambi yake aliyoifanya, mwana-kondoo jike, au mbuzi jike, kutoka katika kundi lake, kuwa ni sadaka ya dhambi; kisha kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya hiyo dhambi yake.

Tazama sura Nakili




Walawi 5:6
13 Marejeleo ya Msalaba  

Na katika ukumbi wa lango palikuwa na meza mbili upande huu, na meza mbili upande huu, ili kuichinja sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya dhambi, na sadaka ya hatia.


Kisha akaniambia, Vyumba vya upande wa kaskazini, na vyumba vya upande wa kusini, ambavyo vyaelekea mahali palipotengeka, ni vyumba vitakatifu; humo makuhani, wamkaribiao BWANA, watakula vitu vilivyo vitakatifu sana; humo wataviweka vitu vilivyo vitakatifu sana, na sadaka ya unga, na sadaka ya dhambi, na sadaka ya hatia; kwa maana mahali hapo ni patakatifu.


Na katika siku atakayoingia ndani ya patakatifu, katika ua wa ndani, ili kuhudumu ndani ya patakatifu, atatoa sadaka yake ya dhambi, asema Bwana MUNGU.


Ndivyo atakavyomfanyia huyo ng'ombe; kama alivyomfanyia huyo ng'ombe wa sadaka ya dhambi, atamfanyia na huyu hivyo; naye kuhani atawafanyia upatanisho, nao watasamehewa.


akijulishwa hiyo dhambi yake aliyoifanya, ndipo atakapoleta mbuzi wa kike mkamilifu, awe matoleo yake kwa ajili ya dhambi yake aliyoifanya.


Kisha atayaondoa mafuta yake yote, kama vile mafuta yanavyoondolewa katika hizo sadaka za amani; kisha kuhani atayateketeza juu ya madhabahu, iwe harufu ya kupendeza kwa BWANA; na kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake, naye atasamehewa.


Naye akileta mwana-kondoo kuwa sadaka ya dhambi, ataleta wa kike mkamilifu.


kisha atayaondoa mafuta yake yote, kama mafuta ya mwana-kondoo yalivyoondolewa katika hizo sadaka za amani; kisha kuhani atayateketeza juu ya madhabahu, kwa desturi ya hizo sadaka za BWANA zilizosongezwa kwa njia ya moto; na kuhani atamfanyia upatanisho kwa ajili ya hiyo dhambi yake aliyoifanya, naye atasamehewa.


Kisha ataleta sadaka yake ya hatia kwa BWANA, ni kondoo dume wa katika kundi lake, mkamilifu, sawasawa na hesabu utakayomwandikia, kuwa sadaka ya hatia, na kumpa kuhani;


Kisha ataziweka kwa BWANA hizo siku za kujitenga kwake, naye ataleta mwana-kondoo wa kiume wa mwaka mmoja, kuwa sadaka ya hatia; lakini hizo siku za kwanza hazitahesabiwa, kwa kuwa kule kujitenga kwake kulitiwa unajisi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo