Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Walawi 4:18 - Swahili Revised Union Version

18 Kisha nyingine katika hiyo damu ataitia katika pembe za madhabahu iliyo mbele za BWANA, iliyoko ndani ya hema ya kukutania, kisha damu yote ataimwaga hapo chini ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo mlangoni pa hema ya kukutania.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Kisha, sehemu ya damu atazipaka pembe za madhabahu iliyoko katika hema la mkutano mbele ya Mwenyezi-Mungu. Damu inayobaki ataimwaga chini kwenye tako la madhabahu ya kuteketezea sadaka iliyo karibu na mlango wa hema la mkutano.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Kisha, sehemu ya damu atazipaka pembe za madhabahu iliyoko katika hema la mkutano mbele ya Mwenyezi-Mungu. Damu inayobaki ataimwaga chini kwenye tako la madhabahu ya kuteketezea sadaka iliyo karibu na mlango wa hema la mkutano.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Kisha, sehemu ya damu atazipaka pembe za madhabahu iliyoko katika hema la mkutano mbele ya Mwenyezi-Mungu. Damu inayobaki ataimwaga chini kwenye tako la madhabahu ya kuteketezea sadaka iliyo karibu na mlango wa hema la mkutano.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Atatia sehemu ya hiyo damu juu ya pembe za madhabahu yaliyo mbele za Mwenyezi Mungu katika Hema la Kukutania. Damu iliyobaki ataimwaga chini ya madhabahu ya kuteketezea sadaka, penye ingilio la Hema la Kukutania.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Atatia sehemu ya hiyo damu juu ya pembe za madhabahu yaliyo mbele za bwana katika Hema la Kukutania. Damu iliyobaki ataimwaga chini ya madhabahu ya kuteketezea sadaka, penye ingilio la Hema la Kukutania.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

18 Kisha nyingine katika hiyo damu ataitia katika pembe za madhabahu iliyo mbele za BWANA, iliyoko ndani ya hema ya kukutania, kisha damu yote ataimwaga hapo chini ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyo mlangoni pa hema ya kukutania.

Tazama sura Nakili

Walawi 4:18
11 Marejeleo ya Msalaba  

Basi wakawachinja ng'ombe, na makuhani wakaipokea damu, wakainyunyiza madhabahuni; wakawachinja kondoo dume, na kuinyunyiza damu madhabahuni; wakawachinja na wana-kondoo, na kuinyunyiza damu madhabahuni.

Kisha twaa baadhi ya damu ya ng'ombe, uitie katika pembe za madhabahu kwa kidole chako; na kuimimina damu yote chini ya madhabahu.

Naye Haruni atafanya upatanisho juu ya pembe zake mara moja kila mwaka; kwa damu ya ile sadaka ya dhambi ya kufanya upatanisho, mara moja kila mwaka ataifanyia upatanisho, katika vizazi vyenu vyote; ni takatifu sana kwa BWANA.

Kisha kuhani atatwaa baadhi ya damu ya hiyo sadaka ya dhambi kwa kidole chake, na kuitia katika pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, nayo damu yake ataimwaga hapo chini ya madhabahu ya kuteketeza.

Kisha kuhani atatwaa baadhi ya hiyo damu yake kwa kidole chake, na kuitia katika pembe za madhabahu ya kuteketeza na damu yake yote ataimwaga chini ya madhabahu.

Kisha kuhani atatwaa katika hiyo damu ya sadaka ya kuteketezwa kwa kidole chake na kuitia katika pembe za madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, kisha damu yake yote ataimwaga hapo chini ya madhabahu;

Kisha kuhani atatia baadhi ya hiyo damu juu ya pembe za madhabahu ya kufukizia uvumba mzuri mbele ya BWANA iliyo ndani ya hema ya kukutania; kisha damu yote ya huyo ng'ombe ataimwaga hapo chini ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyoko mlangoni pa hema ya kukutania.

kisha baadhi ya damu ya hiyo sadaka ya dhambi atainyunyiza katika ubavu wa madhabahu; na damu iliyosalia itachuruzishwa hapo chini ya madhabahu; ni sadaka ya dhambi.

Wala haitaliwa sadaka ya dhambi yoyote, ambayo damu yake yoyote ililetwa ndani ya hema ya kukutania, ili kufanya upatanisho katika mahali patakatifu; itateketezwa.

Kisha akamchinja; na Musa akaitwaa damu yake, akaitia katika pembe za madhabahu pande zote kwa kidole chake, akaitakasa madhabahu, kisha akaimwaga hiyo damu hapo chini ya madhabahu, na kuitakasa, ili afanye upatanisho kwa ajili yake.

Kisha wana wa Haruni wakamsogezea Haruni ile damu; naye akatia kidole chake katika damu, na kuitia katika pembe za madhabahu, kisha akaimwaga hiyo damu hapo chini ya madhabahu;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo