Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 27:26 - Swahili Revised Union Version

26 Mzaliwa wa kwanza tu katika wanyama, aliyewekwa kuwa mzaliwa wa kwanza kwa BWANA, mtu yeyote hatamweka kuwa mtakatifu; kama ni ng'ombe, kama ni kondoo, huyo ni wa BWANA.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 “Hairuhusiwi kumweka wakfu mzaliwa wa kwanza wa wanyama; kisheria huyo ni wake Mwenyezi-Mungu; awe ni ng'ombe au kondoo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 “Hairuhusiwi kumweka wakfu mzaliwa wa kwanza wa wanyama; kisheria huyo ni wake Mwenyezi-Mungu; awe ni ng'ombe au kondoo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 “Hairuhusiwi kumweka wakfu mzaliwa wa kwanza wa wanyama; kisheria huyo ni wake Mwenyezi-Mungu; awe ni ng'ombe au kondoo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 “ ‘Hata hivyo, hakuna mtu atakayemweka wakfu mzaliwa wa kwanza wa mnyama, kwa kuwa mzaliwa wa kwanza tayari ni mali ya Mwenyezi Mungu; awe ng’ombe au kondoo, ni wa Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 “ ‘Lakini hakuna mtu atakayeweka wakfu mzaliwa wa kwanza wa mnyama, kwa kuwa mzaliwa wa kwanza tayari ni mali ya bwana; awe ng’ombe au kondoo, ni wa bwana.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

26 Mzaliwa wa kwanza tu katika wanyama, aliyewekwa kuwa mzaliwa wa kwanza kwa BWANA, mtu yeyote hatamweka kuwa mtakatifu; kama ni ng'ombe, kama ni kondoo, huyo ni wa BWANA.

Tazama sura Nakili




Walawi 27:26
9 Marejeleo ya Msalaba  

Basi wakaondoka kabla ya mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha Washami; na walipofika mwanzo wa kambi ya Washami, kumbe! Hapakuwa na mtu.


tena wazaliwa wa kwanza wa wana wetu, na wa wanyama wetu, kama ilivyoandikwa katika torati, na wazaliwa wa kwanza wa ng'ombe wetu na kondoo wetu, ili kuwaleta nyumbani mwa Mungu wetu, kwa makuhani watumikao nyumbani mwa Mungu wetu;


Nitakasie mimi wazaliwa wa kwanza wote, kila afunguaye tumbo katika wana wa Israeli, wa binadamu na wa mnyama; ni wangu huyo.


Nawe utafanya vivyo hivyo katika ng'ombe wako, na kondoo wako; utamwacha siku saba pamoja na mama yake; siku ya nane utanipa mimi.


Na kama ni wa mnyama asiye safi, ndipo atamkomboa kama hesabu yako ilivyo, naye ataongeza sehemu ya tano ya bei yake; au asipokombolewa, ndipo atauzwa kama hesabu yako ilivyo.


Lakini mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe, au mzaliwa wa kwanza wa kondoo, au mzaliwa wa kwanza wa mbuzi, hutawakomboa hao; maana, ni watakatifu hao; utanyunyiza damu yao katika madhabahu, na kuyateketeza mafuta yao kuwa sadaka iliyosongezwa kwa BWANA kwa moto, iwe harufu ya kupendeza.


kwa kuwa hao wazaliwa wa kwanza wote ni wangu; katika siku ile niliyowapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri nikajiwekea wakfu wazaliwa wa kwanza wote wa Israeli, wa wanadamu na wa wanyama; watakuwa wangu; mimi ndimi BWANA.


Wazaliwa wa kwanza wa kiume wote wazaliwao katika kundi lako la ng'ombe na la kondoo, uwatakase kwa BWANA, Mungu wako; usifanye kazi kwa mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe wako, wala usimkate manyoya mzaliwa wa kwanza wa kundi lako la kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo