Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 27:25 - Swahili Revised Union Version

25 Na hesabu zako zote zitaandamana shekeli ya mahali patakatifu; gera ishirini zitakuwa shekeli moja.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

25 Kila thamani itapimwa kwa kipimo cha uzito cha shekeli kulingana na kipimo cha mahali patakatifu: Uzito wa gera 20 ni sawa na uzito wa shekeli moja.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

25 Kila thamani itapimwa kwa kipimo cha uzito cha shekeli kulingana na kipimo cha mahali patakatifu: Uzito wa gera 20 ni sawa na uzito wa shekeli moja.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

25 Kila thamani itapimwa kwa kipimo cha uzito cha shekeli kulingana na kipimo cha mahali patakatifu: uzito wa gera 20 ni sawa na uzito wa shekeli moja.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

25 Kila thamani lazima iwekwe kulingana na shekeli ya mahali patakatifu: gera ishirini kwa shekeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

25 Kila thamani lazima iwekwe kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, gera ishirini kwa shekeli.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

25 Na hesabu zako zote zitalingana na shekeli ya mahali patakatifu; gera ishirini, sawa na shekeli moja.

Tazama sura Nakili




Walawi 27:25
9 Marejeleo ya Msalaba  

Nacho watakachotoa ni hiki, kila mtu apitaye kwa wale waliohesabiwa atatoa nusu shekeli kwa kuiandama shekeli ya mahali patakatifu; (shekeli ni gera ishirini;) nusu shekeli kwa sadaka ya BWANA.


Dhahabu yote iliyotumiwa kwa ajili ya hiyo kazi, katika kazi hiyo yote ya mahali patakatifu, hiyo dhahabu ya matoleo, ilikuwa ni talanta ishirini na tisa, na shekeli mia saba na thelathini, kwa kadiri ya shekeli ya mahali patakatifu.


Nayo shekeli itakuwa gera ishirini; shekeli tano zitakuwa shekeli tano, shekeli kumi zitakuwa kumi, na shekeli hamsini zitakuwa mane yenu.


Mwaka wa jubilii shamba hilo litarejea kwake huyo ambaye lilinunuliwa kwake, yaani, huyo ambaye nchi hiyo ni milki yake.


Na hesabu yako itakuwa kwa mwanamume, tokea aliye na umri wa miaka ishirini hata umri wa miaka sitini, hesabu yako itakuwa shekeli hamsini za fedha, kwa shekeli ya mahali patakatifu.


Mtu awaye yote akiasi na kufanya dhambi naye hakukusudia, katika mambo matakatifu ya BWANA; ndipo atakapomletea BWANA sadaka yake ya hatia, kondoo dume mkamilifu katika kundi lake; sawasawa na hesabu utakayomwandikia katika shekeli za fedha, kwa shekeli ya mahali patakatifu, kuwa sadaka ya hatia;


Na hao watakaokombolewa katika wanyama hao, tangu aliyepata umri wa mwezi mmoja utamkomboa, kama utakavyohesabu kima chake, kwa fedha ya shekeli tano, kwa shekeli ya mahali patakatifu (nayo ni gera ishirini).


utatwaa shekeli tano kwa kichwa cha kila mtu kwa hiyo shekeli ya mahali patakatifu (shekeli ni gera ishirini);


matoleo yake yalikuwa sahani moja ya fedha, uzani wake ni shekeli mia moja na thelathini, na bakuli moja ya fedha, uzani wake shekeli sabini, kwa shekeli ya mahali patakatifu; vyombo hivyo vyote viwili vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta, kuwa sadaka ya unga;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo