Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 25:5 - Swahili Revised Union Version

5 Hicho kimeacho chenyewe katika mavuno yako, usikivune, wala zabibu za mizabibu isiyopelewa usizitunde; utakuwa mwaka wa kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Chochote kinachoota peke yake msikivune wala kuchuma zabibu kutoka miti isiyopogolewa. Huo utakuwa mwaka wa kuipumzisha ardhi rasmi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Chochote kinachoota peke yake msikivune wala kuchuma zabibu kutoka miti isiyopogolewa. Huo utakuwa mwaka wa kuipumzisha ardhi rasmi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Chochote kinachoota peke yake msikivune wala kuchuma zabibu kutoka miti isiyopogolewa. Huo utakuwa mwaka wa kuipumzisha ardhi rasmi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Msivune chochote kinachoota chenyewe, wala kuvuna zabibu zenu ambazo hamkuzihudumia. Nchi lazima iwe na mwaka wa mapumziko.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Msivune na kuweka akiba kinachoota chenyewe, wala kuvuna na kusindika zabibu ambayo hamkuhudumia mashamba yake. Nchi lazima iwe na mwaka wa mapumziko.

Tazama sura Nakili




Walawi 25:5
5 Marejeleo ya Msalaba  

Na kwako wewe hii ndiyo dalili; mwaka huu mtakula vitu viotavyo vyenyewe; na mwaka wa pili mtakula mazao ya vitu hivyo; na mwaka wa tatu pandeni mbegu, kavuneni; mkapande mashamba ya mizabibu, mkale matunda yake.


Na kwako wewe dalili ndiyo hii; mwaka huu mtakula vitu vimeavyo vyenyewe; na mwaka wa pili mtakula mazao ya mbegu za vitu hivyo; na mwaka wa tatu pandeni mbegu, kavuneni; mkapande mizabibu katika mashamba, mkale matunda yake.


Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni jubilii kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabibu za mizabibu isiyopelewa.


lakini katika mwaka wa saba itakuwa ni Sabato ya kustarehe kabisa kwa ajili ya hiyo nchi, ni Sabato kwa BWANA; usipande shamba lako, wala usipelee shamba lako la mizabibu.


Na hiyo Sabato ya nchi itakuwa chakula kwenu; kwako wewe, na kwa mtumishi wako, na kwa mjakazi wako, na kwa mtumishi aliyeajiriwa, na kwa mgeni wako akaaye pamoja nawe;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo