Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 24:5 - Swahili Revised Union Version

5 Nawe utatwaa unga mwembamba, na kuoka mikate kumi na miwili ya huo unga; sehemu za kumi mbili za efa, zitakuwa katika mkate mmoja.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 “Chukua unga laini, kilo kumi na mbili na kuoka mikate kumi na miwili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 “Chukua unga laini, kilo kumi na mbili na kuoka mikate kumi na miwili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 “Chukua unga laini, kilo kumi na mbili na kuoka mikate kumi na miwili.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 “Chukua unga laini, uoke mikate kumi na miwili, ukitumia sehemu mbili za kumi ya efa ya unga kwa kila mkate.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 “Chukua unga laini, uoke mikate kumi na miwili, ukitumia sehemu mbili za kumi za efa za unga kwa kila mkate.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

5 Nawe utatwaa unga mwembamba, na kuoka mikate kumi na miwili ya huo unga; sehemu za kumi mbili za efa, zitakuwa katika mkate mmoja.

Tazama sura Nakili




Walawi 24:5
18 Marejeleo ya Msalaba  

Eliya akatwaa mawe kumi na mawili, kwa hesabu ya makabila ya wana wa Yakobo, aliyejiliwa na neno la BWANA na kuambiwa, Jina lako litakuwa Israeli.


tena kazi ya mikate ya wonyesho, na ya unga mwembamba wa sadaka ya unga; ikiwa ni wa maandazi yasiyochachwa, au wa yale yaliyotokoswa, au wa yale yaliyookwa; na kazi ya kila namna ya kipimo na cheo;


Na baadhi ya ndugu zao, wa wana wa Wakohathi, waliwajibika kusimamia mikate ile ya wonyesho, ili kuiandaa kila sabato.


nao humtolea BWANA kila asubuhi, na kila jioni, sadaka za kuteketezwa na fukizo la manukato; mikate ya wonyesho pia huiweka kwa taratibu yake juu ya meza takatifu, na kinara cha dhahabu chenye taa zake, kuwaka kila jioni; kwa maana sisi tunayatunza maagizo ya BWANA, Mungu wetu; bali ninyi mmemwacha.


kwa mikate mitakatifu, na kwa sadaka ya unga ya daima, na kwa sadaka ya kuteketezwa ya daima, ya sabato, na ya siku za mwezi mpya, na ya sikukuu, tena kwa vitu vile vitakatifu, na kwa sadaka za dhambi, za kuwafanyia Israeli upatanisho, na kwa ajili ya kazi yote ya nyumba ya Mungu wetu.


Kisha tukapiga kura, makuhani, na Walawi, na watu, juu ya matoleo ya kuni, ili kuzileta nyumbani kwa Mungu wetu, kwa kadiri ya mbari za baba zetu, kwa nyakati zilizoamriwa, mwaka kwa mwaka, kukoka moto madhabahuni mwa BWANA, Mungu wetu, kama ilivyoandikwa katika torati;


Nawe utaiweka mikate ya wonyesho juu ya meza mbele yangu daima.


na meza, na vyombo vyake vyote, na mikate ya wonyesho;


Akaipanga ile mikate juu yake mbele za BWANA; kama BWANA alivyomwamuru Musa.


Nawe utaleta meza na kuitia ndani, na kuviweka sawasawa vile vitu juu yake; kisha utakileta ndani kile kinara cha taa, na kuziwasha taa zake.


Tena juu ya meza ya mikate ya madhabahuni watatandika nguo ya rangi ya samawati, na kuweka juu yake sahani, na miiko, na mabakuli, na vikombe vya kumiminia; na hiyo mikate ya daima itakuwa juu yake;


Jinsi alivyoingia katika nyumba ya Mungu, akaila mikate ile ya wonyesho, ambayo si halali kwake kuila wala kwa wale wenziwe, ila kwa makuhani peke yao?


ambayo kabila zetu kumi na mbili wanataraji kuifikia, wakimwabudu Mungu kwa bidii mchana na usiku. Nami ninashitakiwa na Wayahudi kwa ajili ya tumaini hilo, Ee Mfalme.


Maana hema ilitengenezwa, ile ya kwanza, mlimokuwa na kinara cha taa, na meza, na mikate mitakatifu; ndipo palipoitwa, Patakatifu.


Yakobo, mtumwa wa Mungu, na wa Bwana Yesu Kristo, kwa makabila kumi na mawili waliotawanyika; salamu.


Ndipo kuhani akampa ile mikate mitakatifu; kwa maana hapakuwa na mikate ila ile ya wonyesho, nayo imekwisha kuondolewa mbele za BWANA, ili itiwe mikate ya moto siku ile ilipoondolewa.


Basi siku ile palikuwapo na mtu mmoja wa watumishi wa Sauli, amezuiwa hapo mbele za BWANA jina lake akiitwa Doegi, Mwedomi, mkubwa wa wachungaji wa Sauli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo