Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 20:3 - Swahili Revised Union Version

3 Mimi nami nitamkazia uso wangu mtu huyo, na nitamtenga na watu wake; kwa kuwa ametoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, ili kupatia unajisi patakatifu pangu, na kulinajisi jina langu takatifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Mimi mwenyewe nitamkabili mtu huyo na kumtenga na watu wake kwa sababu alimtoa mmoja wa watoto wake sadaka kwa mungu Moleki na hivyo kupachafua mahali pangu patakatifu na jina langu takatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Mimi mwenyewe nitamkabili mtu huyo na kumtenga na watu wake kwa sababu alimtoa mmoja wa watoto wake sadaka kwa mungu Moleki na hivyo kupachafua mahali pangu patakatifu na jina langu takatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Mimi mwenyewe nitamkabili mtu huyo na kumtenga na watu wake kwa sababu alimtoa mmoja wa watoto wake sadaka kwa mungu Moleki na hivyo kupachafua mahali pangu patakatifu na jina langu takatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Mimi nitauelekeza uso wangu dhidi ya mtu huyo, nami nitamkatilia mbali na watu wake. Kwa maana kwa kumtoa kafara mmoja wa watoto wake kwa Moleki, amenajisi madhabahu yangu na kulinajisi Jina langu takatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Mimi nitauelekeza uso wangu dhidi ya mtu huyo, nami nitamkatilia mbali na watu wake. Kwa maana kwa kumtoa mmoja wa watoto wake kwa mungu Moleki, amenajisi madhabahu yangu na kulinajisi Jina langu takatifu.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 Mimi nami nitamkazia uso wangu mtu huyo, na nitamtenga na watu wake; kwa kuwa ametoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, ili kupatia unajisi patakatifu pangu, na kulinajisi jina langu takatifu.

Tazama sura Nakili




Walawi 20:3
16 Marejeleo ya Msalaba  

Mtu yeyote atakayechanganya mafuta mfano wa haya, au mtu yeyote atakayetia mafuta haya juu ya mgeni, mtu huyo atatengwa mbali na watu wake.


Na katika habari zenu, enyi nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi, Nendeni, mkavitumikie vinyago vyenu kila mmoja wenu; na wakati wa baadaye pia, kama hamtaki kunisikiliza; lakini jina langu takatifu hamtalitia unajisi tena, kwa matoleo yenu, na kwa vinyago wenu.


Kwa sababu hiyo, kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, hakika kwa kuwa umepatia unajisi patakatifu pangu, kwa matendo yako yote niyachukiayo, na kwa machukizo yako yote, kwa sababu hiyo mimi nami nitakupunguza; wala jicho langu halitaachilia, wala sitaona huruma.


Ni hivi mtakavyowatenga wana wa Israeli na unajisi wao; ili wasife katika unajisi wao, hapo watakapoitia unajisi maskani yangu iliyo katikati yao.


Kisha mtu yeyote wa nyumba ya Israeli, au miongoni mwa hao wageni wakaao kati yao, atakayekula damu, ya aina yoyote, nitamkataa mtu huyo alaye damu, na nitamtenga na watu wake.


Usimtoe kafara mzawa wako yeyote kwa Moleki na ulinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi BWANA.


Msiape uongo kwa jina langu, na ukalinajisi jina la Mungu wako; Mimi ndimi BWANA.


Tena kama wenyeji wa nchi wakimfumbia macho mtu huyo kwa njia yoyote, hapo atoapo katika kizazi chake na kumpa Moleki, wasimwue;


Watakuwa watakatifu kwa Mungu wao, wala wasilinajisi jina la Mungu wao; kwa kuwa wao ndio wasongezao sadaka za BWANA kwa njia ya moto, chakula cha Mungu wao; kwa ajili ya hayo watakuwa watakatifu.


lakini mtu huyo atakayekula katika nyama ya sadaka za amani, ambazo ni za BWANA, na unajisi wake akiwa nao juu yake, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake.


Kisha mtu awaye yote atakapogusa kitu chochote kilicho najisi, uchafu wa binadamu, au mnyama aliye najisi, au machukizo yoyote yaliyo najisi, kisha akala nyama ya dhabihu ya sadaka za amani, ambazo ni za BWANA, mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake.


Mtu yeyote yule agusaye maiti ya mtu aliyekufa, asijitakase, analitia unajisi maskani ya BWANA; na mtu huyo atatupiliwa mbali na Israeli; maana, hayo maji ya farakano hayakunyunyizwa juu yake, atakuwa najisi; unajisi wake ungali upo juu yake.


Lakini mtu atakayekuwa najisi, naye hataki kujitakasa, mtu huyo atakatiliwa mbali katika mkutano, kwa sababu amepatia unajisi mahali patakatifu pa BWANA; hayo maji ya farakano hayakunyunyizwa juu yake; yeye yuko najisi.


Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.


Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana uko juu ya watenda mabaya.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo