Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 17:15 - Swahili Revised Union Version

15 Tena kila mtu atakayekula nyamafu, au nyama ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama, awe ni mzalia au mgeni, atafua nguo zake, na kuoga majini naye atakuwa najisi hadi jioni; ndipo atakapokuwa safi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 “Mtu yeyote awe ni mwenyeji au mgeni, anayekula chochote kilichokufa chenyewe au kilichouawa na mnyama wa porini, lazima ayafue mavazi yake na kuoga; naye atakuwa najisi mpaka jioni. Baada ya hapo atakuwa safi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 “Mtu yeyote awe ni mwenyeji au mgeni, anayekula chochote kilichokufa chenyewe au kilichouawa na mnyama wa porini, lazima ayafue mavazi yake na kuoga; naye atakuwa najisi mpaka jioni. Baada ya hapo atakuwa safi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 “Mtu yeyote awe ni mwenyeji au mgeni, anayekula chochote kilichokufa chenyewe au kilichouawa na mnyama wa porini, lazima ayafue mavazi yake na kuoga; naye atakuwa najisi mpaka jioni. Baada ya hapo atakuwa safi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 “ ‘Mtu yeyote, awe mzawa au mgeni, ambaye atakula mzoga wa kitu chochote ama kilichouawa na wanyama mwitu ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi hadi jioni; kisha atakuwa ametakaswa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 “ ‘Mtu yeyote, awe mzawa au mgeni, ambaye atakula mzoga wa kitu chochote ama kilichouawa na wanyama mwitu ni lazima afue nguo zake na aoge kwa maji, naye atakuwa najisi kwa kawaida ya ibada mpaka jioni, kisha atakuwa safi.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

15 Tena kila mtu atakayekula nyamafu, au nyama ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama, awe ni mzaliwa au mgeni, atafua nguo zake, na kuoga majini naye atakuwa najisi hadi jioni; ndipo atakapokuwa safi.

Tazama sura Nakili




Walawi 17:15
22 Marejeleo ya Msalaba  

Nawe utafanya vivyo hivyo katika ng'ombe wako, na kondoo wako; utamwacha siku saba pamoja na mama yake; siku ya nane utanipa mimi.


Nanyi mtakuwa watu watakatifu kwangu mimi; kwa hiyo msiile nyama yoyote iliyoraruliwa huko kondeni na mnyama wa mwitu; mtawatupia mbwa nyama hiyo.


Ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, tazama, roho yangu haikutiwa unajisi; maana tangu ujana wangu hata sasa sijala nyamafu, wala iliyoraruliwa na wanyama; wala nyama ichukizayo haikuingia kinywani mwangu.


Makuhani hawatakula nyamafu, au iliyoraruliwa, ikiwa ya ndege au ya mnyama.


Nanyi mtakuwa najisi kwa wanyama hao; kila atakayegusa mzoga wao atakuwa ni najisi hata jioni;


na mtu awaye yote atakayechukua chochote cha mizoga yao atafua nguo zake, naye atakuwa najisi hata jioni.


Tena kila mnyama aendaye kwa vitanga vyake, katika hao wanyama wote waendao kwa miguu minne, hao ni najisi kwenu; awaye yote atakayegusa mizoga yao, atakuwa ni najisi hata jioni.


Na huyo atakayechukua mzoga wa wanyama hao atafua nguo zake, naye atakuwa ni najisi hata jioni; hao ni najisi kwenu.


Wanyama hao ndio walio najisi kwenu katika hao watambaao; yeyote atakayewagusa, wakiisha kuwa mgoza, atakuwa ni najisi hata jioni.


Tena kitu chochote, wanyama hao mmojawapo atakachokiangukia, wakiisha kufa, kitakuwa ni najisi; cha mti, nguo, ngozi, gunia, chombo chochote cha kufanyia kazi yoyote, lazima kitiwe ndani ya maji, nacho kitakuwa ni najisi hadi jioni; ndipo kitakapokuwa ni safi.


Mnyama yeyote ambaye mna ruhusa kumla akifa, yeye anayeugusa mzoga wake atakuwa najisi hadi jioni.


Na yeye atakayekula nyama ya mzoga wake atafua nguo zake, naye atakuwa najisi hata jioni; yeye atakayeuchukua mzoga wake atafua nguo zake, naye atakuwa ni najisi hadi jioni.


Mtu yeyote atakayegusa kitu chochote kilichokuwa chini yake huyo atakuwa najisi hadi jioni; na mtu atakayevichukua vitu vile atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hadi jioni.


Mtu yeyote atakayekigusa kitanda chake huyo mwanamke atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hadi jioni.


Mtu yeyote atakayekigusa kitanda chake huyo, atazifua nguo zake, na kuoga mwili wake majini, naye atakuwa najisi hadi jioni.


Nyamafu au mnyama aliyeraruliwa na wanyama asile, asijitie unajisi kwa hiyo nyama; mimi ndimi BWANA.


Tena mafuta ya mnyama afaye mwenyewe, na mafuta ya mnyama aliyeraruliwa na wanyama, mna ruhusa kuyatumia kwa matumizi mengine; lakini msiyale kamwe.


na yule aliye safi atamnyunyizia huyo aliye najisi siku ya tatu, na siku ya saba; na katika siku ya saba atamtakasa; naye atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa safi jioni.


Nayo itakuwa amri ya siku zote kwao; na yeye anyunyizaye maji ya farakano atazifua nguo zake; naye ayagusaye hayo maji ya farakano atakuwa najisi hadi jioni.


Na huyo aliyemchoma moto ng'ombe atazifua nguo zake majini, na kuoga mwili wake majini, naye atakuwa najisi hadi jioni.


Msile nyamafu yoyote; waweza kumpa mgeni aliye ndani ya malango yako, ili apate kula; au kumliza mtu wa mataifa; kwa kuwa wewe u taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mamaye.


Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo