Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 13:56 - Swahili Revised Union Version

56 Huyo kuhani ataangalia, ikiwa hilo pigo limeanza kufifia, baada ya kufuliwa kwake, ndipo atalirarua hilo pigo litoke katika vazi, au katika ngozi, au katika lililofumwa, au katika lililosokotwa;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

56 “Kama kuhani ataona kuwa ile alama imefifia baada ya kufuliwa, basi atararua ile sehemu iliyo na namna ya upele wa ukoma.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

56 “Kama kuhani ataona kuwa ile alama imefifia baada ya kufuliwa, basi atararua ile sehemu iliyo na namna ya upele wa ukoma.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

56 “Kama kuhani ataona kuwa ile alama imefifia baada ya kufuliwa, basi atararua ile sehemu iliyo na namna ya upele wa ukoma.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

56 Kama kuhani ataona kuwa ile alama imefifia baada ya kuoshwa, basi atararua sehemu iliyoambukizwa ya vazi, au ngozi, au vazi lililofumwa au kusokotwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

56 Kama kuhani ataona kuwa ile alama imefifia baada ya kuoshwa, basi atararua sehemu iliyo ambukizwa ya nguo au ngozi au kifaa kilichofumwa au kusokotwa.

Tazama sura Nakili




Walawi 13:56
3 Marejeleo ya Msalaba  

likiwa limefumwa, au kusokotwa; likiwa ni la kitani au la sufu; liwe katika ngozi, au kitu chochote kilichofanywa cha ngozi;


kisha kuhani ataangalia, baada ya kuoshwa hilo pigo; ikiwa hilo pigo halikugeuka rangi yake, wala halikuenea, ni najisi; utaliteketeza; ni uharibifu likiwa lina doa ndani au nje.


kisha, likionekana liko vile vile katika hilo vazi, katika lililofumwa, au katika lililosokotwa, au katika kitu chochote cha ngozi, ni pigo lenye kuenea; nawe vazi hilo lenye pigo utaliteketeza.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo