Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Walawi 1:5 - Swahili Revised Union Version

5 Naye atamchinja huyo ng'ombe mbele ya BWANA; kisha wana wa Haruni, hao makuhani, wataileta karibu hiyo damu, na kuinyunyiza damu yake kandokando katika madhabahu iliyo hapo mlangoni pa hema ya kukutania

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Kisha, atamchinja huyo ng'ombe mbele ya Mwenyezi-Mungu. Nao makuhani, wazawa wa Aroni, wataichukua damu na kuinyunyizia madhabahu mlangoni mwa hema la mkutano, pande zake zote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Kisha, atamchinja huyo ng'ombe mbele ya Mwenyezi-Mungu. Nao makuhani, wazawa wa Aroni, wataichukua damu na kuinyunyizia madhabahu mlangoni mwa hema la mkutano, pande zake zote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Kisha, atamchinja huyo ng'ombe mbele ya Mwenyezi-Mungu. Nao makuhani, wazawa wa Aroni, wataichukua damu na kuinyunyizia madhabahu mlangoni mwa hema la mkutano, pande zake zote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Atamchinja yule fahali mchanga mbele za Mwenyezi Mungu, kisha wana wa Haruni walio makuhani wataleta damu na kuinyunyiza pande zote za madhabahu yaliyo penye ingilio la Hema la Kukutania.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Atamchinja yule fahali mchanga mbele za bwana, kisha wana wa Haruni walio makuhani wataleta damu na kuinyunyiza pande zote za madhabahu yaliyo penye ingilio la Hema la Kukutania.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

5 Naye atamchinja huyo ng'ombe mbele za BWANA; kisha wana wa Haruni, hao makuhani, wataileta karibu hiyo damu, na kuinyunyiza damu yake kandokando katika madhabahu iliyo hapo mlangoni pa hema ya kukutania.

Tazama sura Nakili




Walawi 1:5
25 Marejeleo ya Msalaba  

Wakachinja Pasaka, nao makuhani wakamimina damu waliyopokea mikononi mwao, Walawi wakachuna.


Kisha utamchinja huyo ng'ombe mbele ya BWANA, mlangoni pa hema ya kukutania.


Kisha utamchinja huyo kondoo dume, na kuitwaa damu yake, na kuinyunyiza katika madhabahu kuizunguka kandokando.


Kisha utaweka madhabahu ya kuteketeza sadaka mbele ya mlango wa maskani ya hema ya kukutania.


ndivyo atakavyowastusha mataifa mengi; wafalme watamfumbia vinywa vyao; maana mambo wasiyoambiwa watayaona; na mambo wasiyoyasikia watayafahamu.


Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni kutoka kwa uchafu wenu wote, na kutoka kwa vinyago vyenu vyote.


Kisha akaniambia, Mwanadamu, Bwana MUNGU asema hivi; Hizi ndizo sheria za madhabahu katika siku ile watakapoifanya, ili watoe sadaka za kuteketezwa juu yake, na kunyunyiza damu juu yake.


Naye atamchinja hapo upande wa madhabahu ulioelekea kaskazini mbele za BWANA; na wana wa Haruni, hao makuhani, watainyunyiza damu yake juu ya madhabahu pande zote.


Kisha kuhani atamleta karibu na madhabahu, naye atamkongonyoa kichwa, na kumteketeza kwa moto juu ya madhabahu; na damu yake itachuruzishwa kando ya madhabahu;


Kisha atamchinja yule mbuzi wa sadaka ya dhambi, aliye kwa ajili ya watu, na kuileta damu yake ndani ya pazia, na kwa damu hiyo atafanya kama alivyofanya kwa damu ya ng'ombe, na kuinyunyiza juu ya kiti cha rehema, na mbele ya kiti cha rehema,


Kwa kuwa uhai wa mwili uko katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi.


naye ataweka mkono wake kichwani mwake, na kumchinja hapo mbele ya hema ya kukutania; na wana wa Haruni watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote.


Naye ataweka mkono wake kichwani mwake huyo aliyemtoa, na kumchinja mlangoni pa hema ya kukutania; na wana wa Haruni, hao makuhani, watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote.


Na kuweka mkono wako katika kichwa cha mwana-kondoo yule, atachinjwa mbele ya hema ya kukutania; na wana wa Haruni watainyunyiza damu yake katika madhabahu pande zote.


Naye ataweka mkono wake kichwani mwake hiyo sadaka ya dhambi, na kumchinja sadaka ya dhambi mahali hapo pa sadaka ya kuteketezwa.


Naye ataweka mkono wake kichwani mwake sadaka ya dhambi, kisha atamchinja awe sadaka ya dhambi, mahali hapo wachinjapo sadaka ya kuteketezwa.


Kisha kuhani atatia baadhi ya hiyo damu juu ya pembe za madhabahu ya kufukizia uvumba mzuri mbele ya BWANA iliyo ndani ya hema ya kukutania; kisha damu yote ya huyo ng'ombe ataimwaga hapo chini ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, iliyoko mlangoni pa hema ya kukutania.


Nimwendee BWANA na kitu gani, na kuinama mbele za Mungu aliye juu? Je! Nimwendee na sadaka za kuteketezwa, na ndama wa umri wa mwaka mmoja?


Lakini mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe, au mzaliwa wa kwanza wa kondoo, au mzaliwa wa kwanza wa mbuzi, hutawakomboa hao; maana, ni watakatifu hao; utanyunyiza damu yao katika madhabahu, na kuyateketeza mafuta yao kuwa sadaka iliyosongezwa kwa BWANA kwa moto, iwe harufu ya kupendeza.


Na kila kuhani husimama kila siku akifanya ibada, na kutoa dhabihu zile zile mara nyingi; ambazo haziwezi kabisa kuondoa dhambi.


na Yesu mjumbe wa agano jipya, na damu ya kunyunyizwa, inenayo mema kuliko ile ya Habili.


kama vile Mungu Baba alivyotangulia kuwajua katika kutakaswa na Roho, hata mkapata kutii na kunyunyiziwa damu ya Yesu Kristo. Neema na amani na ziongezwe kwenu.


Nao wakamchinja huyo ng'ombe, wakamleta mtoto kwa Eli.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo