Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Waamuzi 8:10 - Swahili Revised Union Version

10 Basi hao kina Zebu na Salmuna walikuwa katika Karkori, na majeshi yao walikuwa pamoja nao, watu kama elfu kumi na tano hesabu yao, ni wote waliobaki wa hilo jeshi lote la hao wana wa mashariki; kwa sababu walianguka wapiganaji elfu mia moja na ishirini waliokuwa wakitumia upanga.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Zeba na Salmuna walikuwa huko Karkori pamoja na jeshi lao la watu 15,000 ambao ndio tu waliobaki kutoka jeshi la mashariki, maana wenzao 120,000 waliuawa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Zeba na Salmuna walikuwa huko Karkori pamoja na jeshi lao la watu 15,000 ambao ndio tu waliobaki kutoka jeshi la mashariki, maana wenzao 120,000 waliuawa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Zeba na Salmuna walikuwa huko Karkori pamoja na jeshi lao la watu 15,000 ambao ndio tu waliobaki kutoka jeshi la mashariki, maana wenzao 120,000 waliuawa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Wakati huu Zeba na Salmuna walikuwa Karkori, wakiwa na jeshi la watu wapatao elfu kumi na tano waliokuwa wamesalia wa mataifa ya mashariki, kwa kuwa watu wapatao elfu mia moja na ishirini wenye panga walikuwa wameuawa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Wakati huu Zeba na Salmuna walikuwa Karkori wakiwa na jeshi lenye watu wapatao 15,000 wale wote waliokuwa wamesalia wa mataifa ya mashariki, kwa kuwa watu wapatao 120,000 wenye panga walikuwa wameuawa.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

10 Basi hao kina Zebu na Salmuna walikuwa katika Karkori, na majeshi yao yalikuwa pamoja nao, watu kama elfu kumi na tano hesabu yao, ni wote waliobaki wa hilo jeshi lote la hao wana wa mashariki; kwa sababu walianguka wapiganaji elfu mia moja na ishirini waliokuwa wakitumia upanga.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 8:10
17 Marejeleo ya Msalaba  

Naye mfalme wa Moabu alipoona ya kwamba ameshindwa vitani, alitwaa pamoja naye watu mia saba wenye kufuta panga ili wapenye hata kwa mfalme wa Edomu; wala hawakudiriki.


Abiya na watu wake wakawapiga mapigo makuu; hata wakaanguka wameuawa wa Israeli elfu mia tano, watu wateule.


Peka mwana wa Remalia akawaua katika Yuda siku moja watu elfu mia moja na ishirini, mashujaa wote; kwa sababu walikuwa wamemwacha BWANA, Mungu wa baba zao.


Waisraeli wakachukua mateka ndugu zao wafungwa elfu mia mbili wakiwemo wanawake, watoto wa kiume na kike, pia wakachukua kwao nyara nyingi, wakazileta nyara Samaria.


Basi malaika wa BWANA alitoka, akaua watu elfu mia moja na themanini na tano katika kituo cha Waashuri, na watu walipoamka asubuhi na mapema, kumbe, hao walikuwa maiti wote pia.


Kwa maana umeivunja nira ya mzigo wake, na gongo la bega lake, na fimbo yake yeye aliyemwonea, kama katika siku ya Midiani.


Hao wana wa Benyamini walihesabiwa siku ile kutoka hiyo miji, wanaume elfu ishirini na sita waliokuwa na silaha, mbali na hao waliokaa Gibea, ambao walihesabiwa watu wateule mia saba.


Nao watu wa Israeli, mbali na hao wa Benyamini, walihesabiwa kuwa ni wanaume elfu mia nne, wenye silaha; hao wote walikuwa ni watu wa vita.


Wakuu wote wa makabila yote ya Israeli, wakahudhuria huo mkutano wa watu wa Mungu, wanaume elfu mia nne waendao kwa miguu, walio na silaha.


Benyamini alitoka kupigana nao kutoka Gibea siku ya pili, wakawaua watu elfu kumi na nane tena katika watu wa Israeli; hao wote walikuwa wamejihami.


BWANA akampiga Benyamini mbele ya Israeli; na wana wa Israeli waliangamiza wanaume elfu ishirini na tano na mia moja, wa Benyamini siku hiyo; wote hao waliokuwa wenye kutumia upanga.


Basi jumla ya watu wa Benyamini waliouawa siku ile walikuwa ni watu elfu ishirini na tano waliokuwa wapiganaji vita; wote hao walikuwa ni mashujaa.


Kwa maana walikwea na ng'ombe zao na hema zao, wakaja mfano wa nzige kwa wingi; wao na ngamia zao pia walikuwa hawana hesabu; nao waliingia katika hiyo nchi ili kuiharibu.


Nao Wamidiani na Waamaleki na, hao wana wa mashariki walikuwa wametua bondeni, mfano wa nzige kwa wingi; na ngamia wao walikuwa hawana hesabu; mfano wa mchanga wa ufuoni, kwa wingi.


Hata Gideoni alipofika, tazama, palikuwa na mtu mmoja aliyekuwa akimhadithia mwenziwe ndoto, akasema, Tazama, niliota ndoto, na tazama, mkate wa shayiri ulianguka katika kambi ya Wamidiani, ukafika katika hema moja, ukaipiga hadi ikaanguka, ukaipindua, hadi ikalala chini.


Wakazipiga zile tarumbeta mia tatu, naye BWANA akaufanya upanga wa kila mtu uwe juu ya mwenziwe, na juu ya jeshi lote, jeshi likakimbia mpaka Bethshita, kuelekea Serera, hadi mpaka wa Abel-Mehola, karibu na Tabathi.


Basi Gideoni alikwea kwa njia iliyotumiwa na misafara, ambayo ilikuwa mashariki mwa Noba na Yogbeha, akalishambulia hilo jeshi; kwa maana lile jeshi halikuwa na hadhari.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo