Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Waamuzi 7:8 - Swahili Revised Union Version

8 Basi Gideoni akachukua vyakula vyao na tarumbeta zao, kisha akawaaga watu wote wa Israeli, kila mtu hemani mwake; akabaki na watu mia tatu; na kambi ya Wamidiani ilikuwa chini yake, bondeni.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 Basi, Gideoni akachukua vyakula vya wale waliokuwa wanaondoka na tarumbeta, akawaaga waende makwao. Yeye akabaki na wale watu 300. Kambi ya Wamidiani ilikuwa bondeni upande wao wa chini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 Basi, Gideoni akachukua vyakula vya wale waliokuwa wanaondoka na tarumbeta, akawaaga waende makwao. Yeye akabaki na wale watu 300. Kambi ya Wamidiani ilikuwa bondeni upande wao wa chini.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 Basi, Gideoni akachukua vyakula vya wale waliokuwa wanaondoka na tarumbeta, akawaaga waende makwao. Yeye akabaki na wale watu 300. Kambi ya Wamidiani ilikuwa bondeni upande wao wa chini.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Hivyo Gideoni akawaruhusu wale Waisraeli wengine kila mmoja aende kwenye hema lake. Akabakia na wale mia tatu, nao wakachukua vyakula na tarumbeta za wenzao. Basi kambi ya Wamidiani ilikuwa chini yake bondeni.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

8 Hivyo Gideoni akawaacha wale Waisraeli wengine kila mmoja aende kwenye hema yake. Akabakia na wale 300, ambao walichukua vyakula na tarumbeta za wale wenzao. Basi kambi ya Wamidiani ilikuwa chini yake bondeni.

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

8 Basi Gideoni akachukua vyakula vyao na tarumbeta zao, kisha akawaaga watu wote wa Israeli, kila mtu hemani mwake; akabaki na watu mia tatu; na kambi ya Wamidiani ilikuwa chini yake, bondeni.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 7:8
11 Marejeleo ya Msalaba  

Tena itakuwa katika siku hiyo, tarumbeta kubwa itapigwa, nao waliokuwa karibu kuangamia katika nchi ya Ashuru watakuja; na hao waliotupwa katika nchi ya Misri; nao watamsujudu BWANA katika mlima mtakatifu huko Yerusalemu.


Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mwezi wa saba, siku ya kwanza ya mwezi, kutakuwa na kustarehe kabisa kwenu, ni ukumbusho wa kuzipiga baragumu, ni kusanyiko takatifu.


Ndipo utakapoipeleka pande zote hiyo baragumu yenye sauti kuu, siku ya kumi ya mwezi wa saba; katika siku hiyo ya upatanisho mtaipeleka baragumu katika nchi yenu yote.


Tena hapo mtakapokwenda kupiga vita katika nchi yenu, kupigana na adui awaoneaye ninyi, ndipo mtakapopiga sauti ya kugutusha kwa tarumbeta; nanyi mtakumbukwa mbele za BWANA, Mungu wenu, nanyi mtaokolewa na adui zenu.


kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, nasi tutabadilika.


Basi watu wakapiga kelele, na makuhani wakazipiga tarumbeta; hata ikawa, hapo watu waliposikia mlio wa mabaragumu hao watu wakapiga kelele kwa sauti kuu sana, na ule ukuta wa mji ukaanguka chini kabisa, hata watu wakapanda juu, wakaingia katika mji, kila mtu akisonga mbele kukabili; wakautwaa huo mji.


Na makuhani saba watachukua baragumu saba za pembe za kondoo dume, watatangulia mbele za hilo sanduku; na siku ya saba mtauzunguka mji mara saba, nao makuhani watapiga baragumu zao.


Ikawa, hapo alipofika akapiga tarumbeta katika nchi ya vilima vilima ya Efraimu, ndipo wana wa Israeli wakateremka pamoja naye kutoka huko milimani, naye akawatangulia.


Wakati huo Wamidiani na Waamaleki, na hao wana wa mashariki walikutana pamoja; wakavuka na kupanga hema zao katika bonde la Yezreeli.


BWANA akamwambia Gideoni, Kwa watu hawa mia tatu walioyaramba maji nitawaokoa, nami nitawatia Wamidiani katika mikono yako; lakini watu hawa wote wengine na waende zao, kila mtu mahali pake.


Ikawa usiku uo huo BWANA akamwambia, Ondoka, shuka kambini; maana nimeitia katika mikono yako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo