Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Waamuzi 3:16 - Swahili Revised Union Version

16 Ehudi alijifanyia upanga uliokuwa na makali kuwili, urefu wake ulipata dhiraa moja; akaufunga huo upanga ndani ya nguo yake katika paja lake la mkono wa kulia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Ehudi akajitengenezea upanga wenye makali kuwili; urefu wake sentimita hamsini. Akaufunga kiunoni mwake upande wa kulia ndani ya mavazi yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Ehudi akajitengenezea upanga wenye makali kuwili; urefu wake sentimita hamsini. Akaufunga kiunoni mwake upande wa kulia ndani ya mavazi yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Ehudi akajitengenezea upanga wenye makali kuwili; urefu wake sentimita hamsini. Akaufunga kiunoni mwake upande wa kulia ndani ya mavazi yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Basi Ehudi alikuwa ametengeneza upanga ukatao kuwili, ukiwa na urefu wa kama dhiraa moja, naye akaufunga upanga huo ndani ya nguo yake, kwenye paja lake la mkono wa kuume.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Basi Ehudi alikuwa ametengeneza upanga wenye ukatao kuwili, urefu wake ni kama dhiraa moja, akaufunga upanga huo ndani ya nguo yake kwenye paja lake la mkono wa kuume.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 3:16
10 Marejeleo ya Msalaba  

Basi walipokuwako kwenye lile jiwe kubwa lililoko Gibeoni, Amasa akaja kuwalaki. Naye Yoabu alikuwa amefungwa mavazi yake ya vita aliyoyavaa, na juu yake alikuwa na mshipi, na upanga uliotiwa viunoni mwake ndani ya ala yake; naye alipokuwa akienda, ukaanguka.


Sifa kuu za Mungu na ziwe vinywani mwao, Na upanga mkali kuwili mikononi mwao.


Jifungie upanga wako pajani, wewe uliye hodari, Utukufu ni wako na fahari ni yako.


Wote wameshika upanga, Wamehitimu kupigana; Kila mtu anao upanga wake pajani Kwa hofu ya kamsa za usiku.


Maana neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena ni jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.


Naye alikuwa na nyota saba katika mkono wake wa kulia; na upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake; na uso wake kama jua liking'aa kwa nguvu zake.


Na kwa malaika wa kanisa lililoko Pergamo andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na huo upanga mkali, wenye makali kuwili.


Lakini wana wa Israeli walipomlilia BWANA, BWANA akawainulia mwokozi, Ehudi, mwana wa Gera, Mbenyamini, mtu aliyekuwa mwenye shoto; nao wana wa Israeli walimpelekea Egloni mfalme wa Moabu tunu mkononi mwa huyo Ehudi.


Kisha akamsogezea Egloni, mfalme wa Moabu, hiyo tunu; basi Egloni alikuwa ni mtu aliyenenepa sana.


Ehudi akaunyosha mkono wake wa kushoto, akaushika huo upanga kuutoa hapo katika paja lake la kulia, akamtia tumboni mwake;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo