Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -

Waamuzi 21:3 - Swahili Revised Union Version

3 Wakasema, Ee BWANA, Mungu wa Israeli, kwa nini jambo hili kuwa katika Israeli, ya kwamba hivi leo kabila moja limepunguka katika Israeli?

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Wakasema “Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, kwa nini jambo hili limetukia hata tupungukiwe na kabila katika Israeli?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Wakasema “Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, kwa nini jambo hili limetukia hata tupungukiwe na kabila katika Israeli?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Wakasema “Ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, kwa nini jambo hili limetukia hata tupungukiwe na kabila katika Israeli?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Wakasema, “Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli, kwa nini jambo hili limewapata Waisraeli? Kwa nini kabila moja la Israeli limekosekana?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Wakasema, “Ee bwana, Mungu wa Israeli, kwa nini jambo hili limewapata Waisraeli? Kwa nini kabila moja la Israeli limekosekana?”

Tazama sura Nakili

BIBLIA KISWAHILI

3 Wakasema, Ee BWANA, Mungu wa Israeli, kwa nini jambo hili kuwa katika Israeli, ya kwamba hivi leo kabila moja limepunguka katika Israeli?

Tazama sura Nakili

Waamuzi 21:3
9 Marejeleo ya Msalaba  

Ee Mungu, mbona umetutupa milele? Kwa nini hasira yako inatoka moshi Juu ya kondoo wa malisho yako?

Kwa nini umezibomoa kuta zake, Wakauchuma wote wapitao njiani?

Upumbavu wa mtu hupotosha njia yake; Na moyo wake hununa juu ya BWANA.

Ee BWANA, mbona umetukosesha njia zako, ukatufanya kuwa na mioyo migumu hata tusikuogope? Urudi kwa ajili ya watumishi wako, makabila ya urithi wako.

Wewe u mwenye haki, Ee BWANA, nitetapo nawe, lakini nitasema nawe katika habari ya haki. Mbona njia ya wabaya inasitawi? Mbona wote watendao hila wanakaa salama?

mataifa yote watasema, Mbona BWANA ameifanyia hivi nchi hii? Ni nini maana yake joto la hasira hizi kubwa?

Basi hao watu wakafika Betheli, wakaketi huko mbele ya Mungu hadi jioni, nao wakainua sauti zao na kulia sana.

Kisha kesho yake, hao watu wakaamka asubuhi na mapema, wakajenga madhabahu huko, wakasongeza sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo