Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Waamuzi 16:4 - Swahili Revised Union Version

4 Ikawa baada ya hayo akampenda mwanamke mmoja katika bonde la Soreki, jina lake akiitwa Delila.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Baada ya hayo, Samsoni alimpenda mwanamke mmoja aitwaye Delila ambaye aliishi katika bonde la Soreki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Baada ya hayo, Samsoni alimpenda mwanamke mmoja aitwaye Delila ambaye aliishi katika bonde la Soreki.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Baada ya hayo, Samsoni alimpenda mwanamke mmoja aitwaye Delila ambaye aliishi katika bonde la Soreki.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Baada ya hayo akampenda mwanamke mmoja katika Bonde la Soreki aliyeitwa Delila.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Baada ya hayo akampenda mwanamke mmoja katika Bonde la Soreki aliyeitwa Delila.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 16:4
9 Marejeleo ya Msalaba  

Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti,


Je! Sulemani, mwana wa Daudi, hakufanya dhambi kwa kutenda hayo? Lakini katika mataifa mengi hapakuwa na mfalme mwingine mfano wake. Tena alipendwa na Mungu wake, naye Mungu akamfanya mfalme juu ya Israeli; lakini wanawake wageni walimkosesha hata yeye.


Kinywa cha malaya ni shimo refu; Anayechukiwa na BWANA atatumbukia ndani yake.


Kwa maana kahaba ni shimo refu; Na malaya ni mtego wa shimo jembamba.


Kama vile mbwa arudiavyo matapiko yake; Kadhalika mpumbavu afanya upumbavu tena.


Hata ukimtwanga mpumbavu kwa mchi kinuni pamoja na ngano; Upumbavu wake hautamtoka.


Basi mambo hayo yalikuwa mifano kwetu, kusudi sisi tusiwe watu wa kutamani mabaya, kama wale nao walivyotamani.


Basi Samsoni akalala hadi usiku wa manane, akaamka katikati ya usiku, akaishika milango ya lango la mji, na miimo yake miwili, akaing'oa pamoja na komeo lake, akajitwika mabegani, akavichukua hadi katika kilele cha mlima ule unaokabili Hebroni.


Nao wakuu wa Wafilisti wakamwendea, wakamwambia, Mbembeleze, upate kujua asili ya nguvu zake nyingi, na jinsi tutakavyoweza kumshinda, tupate kumfunga na kumtesa; nasi tutakupa kila mtu fedha elfu na mia moja.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo