Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Waamuzi 16:3 - Swahili Revised Union Version

3 Basi Samsoni akalala hadi usiku wa manane, akaamka katikati ya usiku, akaishika milango ya lango la mji, na miimo yake miwili, akaing'oa pamoja na komeo lake, akajitwika mabegani, akavichukua hadi katika kilele cha mlima ule unaokabili Hebroni.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Lakini Samsoni akabaki mjini mpaka usiku wa manane. Wakati wa usiku wa manane akaamka akashika miimo miwili ya malango, akaingoa pamoja na makomeo yake akaibeba na kwenda nayo mpaka karibu na Hebroni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Lakini Samsoni akabaki mjini mpaka usiku wa manane. Wakati wa usiku wa manane akaamka akashika miimo miwili ya malango, akaingoa pamoja na makomeo yake akaibeba na kwenda nayo mpaka karibu na Hebroni.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Lakini Samsoni akabaki mjini mpaka usiku wa manane. Wakati wa usiku wa manane akaamka akashika miimo miwili ya malango, akaing'oa pamoja na makomeo yake akaibeba na kwenda nayo mpaka karibu na Hebroni.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Samsoni akalala tu hadi usiku wa manane. Akaamka, na kushika milango ya lango la mji, na miimo yake miwili, akaing’oa pamoja na makomeo yake. Akaviweka mabegani mwake na kuvipeleka hadi kilele cha mlima unaokabili Hebroni.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Samsoni akalala mpaka usiku wa manane. Akaondoka katikati ya usiku, akashika milango ya lango la mji pamoja na miimo yake miwili, akaing’oa, makomeo yake na vyote. Akaviweka mabegani mwake na kuvipeleka mpaka kwenye kilele cha mlima ule unaokabili Hebroni.

Tazama sura Nakili




Waamuzi 16:3
6 Marejeleo ya Msalaba  

Maana ameivunja milango ya shaba, Ameyakata mapingo ya chuma.


Avunjaye amekwea juu mbele yao; Wamebomoa mahali, wakapita mpaka langoni, Wakatoka nje huko; Mfalme wao naye amepita akiwatangulia, Naye BWANA ametangulia mbele yao.


ambaye Mungu alimfufua, akiufungua uchungu wa mauti, kwa sababu haikuwezekana ashikwe nao.


Watu wa Gaza wakaambiwa, ya kwamba, huyo Samsoni amekuja huku. Wakamzingira, wakamvizia usiku kucha, penye lango la mji, wakanyamaza kimya usiku kucha, wakisema, Na tungoje mpaka mapambazuko, ndipo tutamwua.


Ikawa baada ya hayo akampenda mwanamke mmoja katika bonde la Soreki, jina lake akiitwa Delila.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo