Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni
- Matangazo -




Waamuzi 15:4 - Swahili Revised Union Version

4 Samsoni akaenda akakamata mbweha mia tatu; kisha akatwaa mienge ya moto akawafunga mbweha mkia kwa mkia, akatia mwenge kati ya kila mikia miwili.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Basi, Samsoni akaenda, akawakamata mbweha 300 na akawafunga mikia yao pamoja wawiliwawili. Kisha akaweka mwenge katika kila jozi ya mbweha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Basi, Samsoni akaenda, akawakamata mbweha 300 na akawafunga mikia yao pamoja wawiliwawili. Kisha akaweka mwenge katika kila jozi ya mbweha.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Basi, Samsoni akaenda, akawakamata mbweha 300 na akawafunga mikia yao pamoja wawiliwawili. Kisha akaweka mwenge katika kila jozi ya mbweha.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Hivyo Samsoni akaondoka na kuwakamata mbweha mia tatu, akawafunga wawili wawili, mikia kwa mikia. Kisha akafungia mwenge wa moto kwenye kila jozi la mikia hiyo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Hivyo Samsoni akatoka akawakamata mbweha 300 na kuwafunga wawili wawili kwa mikia yao kila mmoja kwa mwingine. Kisha akafungia mwenge wa moto, kwenye mikia ya kila jozi moja ya mbweha aliyokuwa ameifunga,

Tazama sura Nakili




Waamuzi 15:4
8 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa hiyo akawaambia watumishi wake, Tazameni, shamba la Yoabu liko karibu na shamba langu, naye ana shayiri huko; nendeni mkalitie moto. Basi watumishi wa Absalomu wakalitia moto lile shamba.


Watatolewa wafe kwa nguvu za upanga, Watakuwa riziki za mbwamwitu.


Kama mtu mwenye wazimu atupaye mienge, Na mishale, na mauti;


Tukamatie mbweha, Wale mbweha wadogo, Waiharibuo mizabibu, Maana mizabibu yetu yachanua.


ukamwambie, Hadhari, tulia; usiogope wala usife moyo, kwa sababu ya mikia hii miwili ya vinga hivi vitokavyo moshi; kwa sababu ya hasira kali ya Resini na Shamu, na mwana wa Remalia.


Kwa ajili ya mlima Sayuni ulio ukiwa, Mbweha hutembea juu yake.


Samsoni akasema, Safari hii nitakuwa sina hatia kwa hawa Wafilisti, hapo nitakapowadhuru.


Alipokwisha kuiwasha moto ile mienge, akawaachia mbweha kati ya ngano ya Wafilisti, akayateketeza matita, na ngano, hata na mashamba ya mizeituni.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo